Masikini wanaishi maisha ghali kuliko matajiri

Masikini wanaishi maisha ghali kuliko matajiri

Matajiri wanagharamia sana papuchi, sie masikini tunapewa hata bure
 
Matumizi yote ya nyumbani ya maskini kwa mwaka hayafiki hata ada ya muhula wa kwanza anayolipa tajiri kwa mwanae, sasa sijui unawaongelea matajiri wa kiwango kipi?
 
Badalaya kupanda bajaji ya buku ili awahi elfu 10+, anapanda daladala ya 600 anachelewa na kukosa hela
Noma sana mkuu...anapunguza matumizi but anaingia gharama Zaidi...kuna jamaa alishawahi chelewa interview akiwa kwenye daladala za Mbagala.
 
Matumizi yote ya nyumbani ya maskini kwa mwaka hayafiki hata ada ya muhula wa kwanza anayolipa tajiri kwa mwanae,,,sasa sijui unawaongelea matajiri wa kiwango kipi?
Hayo matumizi ya masikini anayapata kwa bei ghali kuliko matajiri.. Mfano mche mmoja wa sabuni wenye vipande vitano unauza kwa 3000, but kwa kuwa masikini Hana ela atanunua kipande kimoja kimoja kwa sh.800, so vipande vinne atanunua kwa 4000.
 
Kaka ni vizuri kusoma kabla ya kuandika, usipingane na laws za uchumi ambapo kadri kipato kinavyokuwa kikubwa na spending yako nayo lazima kuongezeka.
 
Hayo matumizi ya masikini anayapata kwa bei ghali kuliko matajiri.. Mfano mche mmoja wa sabuni wenye vipande vitano unauza kwa 3000, but kwa kuwa masikini Hana ela atanunua kipande kimoja kimoja kwa sh.800, so vipande vinne atanunua kwa 4000.
Utofauti manunuzi ya jumla na rejareja kwenye ununuzi wa bidhaa hakuhalalishi ughali wa maisha baina ya masikini na tajiri.Masikini akinunua Kg ya mchele wa kiwango cha kati 2000 jua fika tajiri atanunua mchele wa quality ya juu wa kg 3500.

Maskini atanunua mchele kwa kg 1 kwa tshs 2000 kutokana na bajeti yake ndogo yamkini usitosheleleze familia yake,but tajiri atanunua mchele wa quality ya Juu utakaotosheleza mahitaji yake kwa kilo 2.
 
Nashukuru kwa kunielewa...mwalimu akikopa anawekewa riba ya 35% wakati Bakhresa anapaswa mkopo wa riba ya .2% tena kwa kubembelezwa
Riba ya Mkopo inategemeana na muda wa mkopo na sio vinginevyo, matajiri na wafanyabishara wakubwa kukopa ni lazima sio kubebembelezwa.
 
Unamaanisha tunaelewa vibaya Kuwa matajiri ndio masikini na masikini ndio matajiri ni vilee dunia tu haieleweki na sisi ndio hatuelewi.
 
Kwa hiyo unataka kusema maskini anayekula kwa Mamalishe mfano ugali Mbogamboga Kwa buku ana nafuu sana kuliko tajiri anayekula ugali huo huo kwa shilingi 5,000 -10,000 kwenye hotel/restaurant ?

Je hapo nimekuelewa?

Sasa kama ndivyo nikuulize;
Je unafahamu risks (hatari) zinazoambatana na maskini kwenda kula kwa Mamalishe?

Uchafu huleta magonjwa na kutibiwa ni hela hapo gharama .

Kwa Mamalishe mazingira huwa sio rasmi, maji haba, ufahamu wa mambo ya hygien related issues hawajui na hawako tayari kujua wabishi !

Ushirikina Je ?

Uwezekano ni mkubwa wa kununua inferior products sababu ya Mtaji wao kuwa Mdogo Kwa kudunduliza.

Utakuta mafuta wananunua yale ya ubora wa chini kabisa. Sasa kwa mlaji hiyo ni hatari kubwa sana kiafya.

Umetumia gharama ndogo kula kwa Mamalishe lakini risks zake zitaweza kukugharimu pakubwa!

Buyer beware
Mimi ndo maana niliamua niwe nakula nyumbani tu

Juisi nakunywa nilizotengeneza mimi, hizi za mitaani hawajali usafi wala tunda kuharibika.

Juisi ya miwa nazo nimeachana nazo, sababu ni usafi mdogo sana.

Matajiri wengi hujali afya.

Wanapangilia muda wa chakula

Hawali ugali mkubwa usiku
 
Kihalisia ukiambiwa uthibitishe hizo risk ni vigumu sana, ni kama kuthibitisha madhara yaliyosababishwa na mionzi ya minara ya simu (tuliaminishwa kuwa minara kuwa karibu na makazi inaleta mionzi yenye madhara makubwa sana).



Mmnh!

Inaonekana hujapata kujifunza na kufahamu kwa mapana yake kuhusu “ risks “

Iko wazi kabisa kitaalam kuwa “ Risks must be calculated “

Kutegemeana na nature ya tasnia.

Mfano kwenye biashara kuna risks za aina yake kati ya biashara moja na nyingine,

N.k.
 
Back
Top Bottom