Masikini wasipewe vibali kujenga mjini. Huchafua miji na vijumba vyao

Nakubaliana na wewe by 100%. Masikini pia wasiruhusiwe kuzaa, wahasiwe maana tutaendeleza ile kitu wanaita viscious cycle ie masikini kuzaa masikini na huyo masikini kuzaa masikini mpaka kijiji kinajaa masikini tupu. I am also poor, let us be pushed outside the town and live wherever befits us , not in civilised societies
 
Mungu akiwa upande wako huwa tunajawa viburi, majivuno na kejeli za kila aini. Amini amini nakwambia Mungu akigeuza shingo na asikutazame tena, huwa nimajuto yasio na ukomo.

Hekima, busara na utu ndio Jambo jema kuliko pesa.
 
Chanzo Cha maovu yote duniani ni umasikini maana umasikini ni laana.Kwenye umasikini ndo Kuna vyanzo vya dhambi .Uzinzi na umalaya chanzo chake ni umasikini,mtu anaenda kijiuza ili apate hela ya kula mwisho wa siku anapata ukimwi anakufa ,Hapo Kuna kitu kinaitwa mshahara wa dhambi ni mauti

Serikali ya Tanzania inatoa elimu bila malipo je hizo pesa zinatoka wapi?Ni hela za matajili kutokana na kodi.kuna kanuni ya kiasili inasema ukitoa unapata zaidi na kubarikiwa,Kwa hiyo basi matajili ndo wanawasomesha watoto wa masikini na wanazidi kubarikiwa.
Pia Kumbukeni kazi ya Mungu inaendeshwa na Matajili kwa kujenga Makanisa na Misikiti.
Pia mnitajie Mtume yeyote wa MUNGU ambae alikua masikini,hayupo na hatakuwepo.
Mleta mada yupo sahihi 100%.
Nina uhakika hata mbinguni wataenda matajili kwa maana ndo wanawafanya masikini waishi hivo wanamsaidia Mungu kazi . MUNGU NI ALAMA YA UTAJILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia matako kulia mbwata ndio hivi sasa kwa huyu masikini mwenzetu anayejiita taikoni wa fasihi.

Hizo nyumba za NHC naona mmeamua kuishi mabwanyeye na kuanza kututukana sie makabwela.
 
Unahoja ya nguvu sana ila wengi hawatakuelewa kwani hawataki kutafakari. Labda ungetumia lugha ya kidiplomasia zaidi na kusema ujenzi kwenye miji utungiwe kanuni na sheria ya nyumba za aina na gharama gani zinatakiwa kujengwa. BTW hivi mnadhani kaburu alipoamua kuwa waafrika watengewe sehemu yao ya kuishi na wazungu wawe na sehemu yao alikosea sana?
 
Asante sana Bill luga o a.k.a Kiduku Lilo
 
Miji ilianzishwa na maskini , nadhani hao matajiri wangeanzisha miji yao ili wakae mbali na maskini. Kariakoo ilikuwa ya maskini matajiri wakaja, sio maskini waliofuata matajiri mijini
 
Uzuri wote tunaweza kuwa matajiri pia wote tunaweza kuwa maskini je wewe utakuwa upande upi tusubiri
 
Na wale wanao jenga vijumba vya gorofa 1 mjini kati nao ni wale wale tu
 
Kama nimekuelewa Hivi Mkuu
Umeandika fact ila Kwa sababu ya masikini hua hatukubali ukweli mchungu na tuna roho mbaya
Ngoja nikoment kimasikini Zaidi hapo chini

Acha kujiona bwege wewe u anajiona una akili Sana mtoa mada ulitaka tuishi wapi na tulishawahi kuja kukuomba Hela ya kula?

(In Masikini wa akili voices)
 
Tatizo la miji kuwa michafu, na watu kujenga pasipo mpangilio linasababishwa na Masikini. Unajua masikini ni mashetani hivyo hawanaga mipangilio, wapo rafu wanajenga hovyo hovyo.
Kwani nani anagawa viwanja na kupanga mji? Kuna mamlaka zenye kazi hio. Hizi mamlaka zina uwezo wa kutenga maeneo na kuwauzia matajiri au masikini. Unafikiri kwanini Masaki,Mbezi beach kuna watu wa aina yenu?! Mamlaka zina uwezo wa kutenga maeneo na kupanga zijengwe nyumba za aina gani kama huwezi unaachia eneo ni mali ya serikali.
Mamlaka hizo hizo zina uwezo wa kuwaondoa/kuwabomolea waliojenga kiholela bila kufuata utaratibu wa mipango miji. Nashangaa wewe Bwana Tajiri Taikon wa Fasihi unashindwa kuelewa kitu rahisi kama hiki?!
 
Kauli mbaya sana hii kuisikia, kwaiyo kama tunaishi mara moja ndio tuishi kijinga jinga si ndio?
Maskini na matajiri wote nyumba yetu ni moja nayo nikaburi kuna haja gani yakupamba dunia ambayo hakuna atakaye iishi milele
 
Kauli mbaya sana hii kuisikia, kwaiyo kama tunaishi mara moja ndio tuishi kijinga jinga si ndio?
Maskini na matajiri wote nyumba yetu ni moja nayo nikaburi kuna haja gani yakupamba dunia ambayo hakuna atakaye iishi milele
 


Sisi masikini tukibomolewa vibanda vyetu tunapiga mayowe na kulaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…