Masikini, wavivu na watu wenye roho mbaya walikuwa wakifurahia hatua za Magufuli kuturudisha kwenye UJAMAA

Masikini, wavivu na watu wenye roho mbaya walikuwa wakifurahia hatua za Magufuli kuturudisha kwenye UJAMAA

Kuanzia Nyerere mpaka sasa ni unyonyaji na ufukarishaji.

Vyama vya Ushirika vimekufa, majirani zetu kenya wamejifunza kwetu ushirika, sasa hivi vyama vya ushirika ke vina nguvu kubwa sana kiuchumi.

Nyerere angeacha vikastawi tz tungekuwa wapi?

Nyerere ilitakiwa achukue mazuri ya wakoloni ndio aendelee nayo.Yeye aliacha hata mazuri ya wakoloni
 
Maisha ni kama sarafu yana pande mbili. Hata kwa sasa wapo wanaofurahia kufukuzwa kwa machinga mjini na kupanda kwa bei ya bidhaa kwa kisingizio cha vita.
Najua angekuwepo asingeruhusu utetezi huu. Kg moja ya unga wa mahindi tsh 2000 kutoka tsh 1000/-

Machinga wamepelekwa huko kusikojulikana. Nani kweli anaweza kwenda kununua kitana cha 500/_ kwa kupanda boda au dalalada kwa sh 2000?

Na ukweli ni kwamba wakati wa yule baba, watu walipiga kazi. Slogan ya hapa kazi tu iliwahamasisha sana!
Na kauli yake ya hakuna cha bure. Tofauti na sasa wanakula kwa urefu wa kamba! Wanatoa visingizio visivyo na tija na vinakubalika! Tofauti ya wenye nacho na wasionacho inazidi kuwa kubwa.
Nchi imegeuka kuwa uwanja wa michezo ya kubahatisha. Kila mahali cheza ushinde! Na hapo no hela zinakatwa pamoja na kodi. Na mtaani bado hali ni tete.

Hizo fedha zinakwenda wapi? Walahi, natamani huyu mama ajiuzulu hata leo na sio kwa chuki wala ubaya, bali kwa nia njema tu ya kuokoa taifa!

Wanadanganya watumishi nyongeza 23% kisha wanakuja na utetezi wa kima cha chini na kima cha juu. PAYE imeongezeka.
Yaani mtu anayeusifia huu utawala huenda yuko nje ya nchi au ni mlamba asali.

Japo hata walamba asali wapo wanaoisoma namba manaake mfumuko wa bei unagusa wote!
Hakuna kipindi nilikuwa mzalendo kwa nchi yangu kama kwenye utawala wa JPM nlikuwa na wivu na nchi yangu hatari. Kila aliyehujumu choxhote nlikuwa mkali as if ananiibia mimi
 
Ndo mda pekee nlianza kufanya kazi za ofisi hadi usiku bila kuchoka. Ila sasa ikifika saa tisa na usu naondoka wjether imeisha ama la
 
Maisha ni kama sarafu yana pande mbili. Hata kwa sasa wapo wanaofurahia kufukuzwa kwa machinga mjini na kupanda kwa bei ya bidhaa kwa kisingizio cha vita.
Najua angekuwepo asingeruhusu utetezi huu. Kg moja ya unga wa mahindi tsh 2000 kutoka tsh 1000/-

Machinga wamepelekwa huko kusikojulikana. Nani kweli anaweza kwenda kununua kitana cha 500/_ kwa kupanda boda au dalalada kwa sh 2000?

Na ukweli ni kwamba wakati wa yule baba, watu walipiga kazi. Slogan ya hapa kazi tu iliwahamasisha sana!
Na kauli yake ya hakuna cha bure. Tofauti na sasa wanakula kwa urefu wa kamba! Wanatoa visingizio visivyo na tija na vinakubalika! Tofauti ya wenye nacho na wasionacho inazidi kuwa kubwa.
Nchi imegeuka kuwa uwanja wa michezo ya kubahatisha. Kila mahali cheza ushinde! Na hapo no hela zinakatwa pamoja na kodi. Na mtaani bado hali ni tete.

Hizo fedha zinakwenda wapi? Walahi, natamani huyu mama ajiuzulu hata leo na sio kwa chuki wala ubaya, bali kwa nia njema tu ya kuokoa taifa!

Wanadanganya watumishi nyongeza 23% kisha wanakuja na utetezi wa kima cha chini na kima cha juu. PAYE imeongezeka.
Yaani mtu anayeusifia huu utawala huenda yuko nje ya nchi au ni mlamba asali.

Japo hata walamba asali wapo wanaoisoma namba manaake mfumuko wa bei unagusa wote!
upo Sawa mkuu lakini tujadili hili la nyongeza ya Kima cha chini asilimia 23% je yule mzalendo aliweza kuongeza Ata senti 5 jibu ni hapana alishindwa

je ajila kipindi cha huyu mzalendo zilikuaje jibu ni holaaa

ukija kweny point ya vitu kupanda bei huu ni mfumuko wa dunia nzima kweny Biashara Kuna demand and supply kitu kikiwa hadimu obviously kita kua na thamani
unajua uzalishaji ulipungua kwa asilimia ngapi kipindi cha Korona? bidhaa nyingi na chakula tunategemea kuingiza kutoka nje Leo unalalamika Unga kununua 2000Tsh per kg je unajua viuatilifu mbegu mbolea na madawa tunaagiza nje na vyote vimepanda bei kutoka na athari za Korona? ujajua mfuko mmoja wa mbolea ni 130k bado unataka mkulima auze debe 5000 Tsh.?
vip kuhusu kupanda bei kwa mafuta kutokana na mgogoro wa Russia? na unajua bidhaa zote Zina tegemea mafuta kwenye transportation mafuta yakiwa juu na bidhaa nyingine lazima zipande bei mkuu je Tanzania tuna visima vyetu vya mafuta? hahaha jibu unalo

OK vitu vingine tumia uhalisia vipi kilimo cha msimu huu kulikua na uzalishaji wa kutosheleza.? jibu ni nope kwa sababu tunategemea kilimo cha msimu wa mvua je huko kwenu hamkulia mvua hamna? jibu unalo vitu vingine tusitumie chuki tumia logic mkuu
 
Habari!
Watu maskini, wajinga (waliokosa elimu), na wavivu ndio makundi ya watu waliokuwa wakifurahia harakati za Magufuli kutupeleka kwenye UJAMAA.

Hata.
UJAMAA hauwezi kufurahiwa na watu wenye bidii na vipawa katika utafutaji. Hata Wachina wanaukacha UJAMAA na kuanza kuishi kibepari, kila mmoja anakula kipawa na juhudi zake. Magufuli alipotumbua viongozi ilikuwa faraja kwa makundi hayo niliyoyataja, alipowafilisi mabosi kundi hili walishangilia.

Kundi hili kila siku linaishi likiamini kuwa matajiri wote ni mafisadi na wezi wa pesa zao. Kundi hili furaha yao ni kuona wa juu anashuka chini hata kama wao hawatapanda juu.

Umaskini mbaya wakuu.
Mwenyewe una utajiri gani? Vibajaji viwili na banda unajiweka kundi la tajiri😂. Magufuli aliungwa mkono na wasomi na watu wako vizuri tu sio unawaita maskini.
Mnajidai kupenda ubepari wakati wala sio ubepari mnafanya ila kufanya magendo kuibia umma na kutumikia maslahi ya ubeberu wa kimataifa. Kwa msingi huo kamwe nchi haiwezi kuendelea.
Isitoshe itikadi rasmi ya ccm ni ujamaa na kujitegemea. Ccm ilishabadili mkakati jinsi ya kujenga ujamaa. Badala ya kutumia sekta ya umma sasa ni kutumia sekta binafsi.
Ili kufanikiwa sekta binafsi lazima kudhibitiwa na serikali. Kilichotokea kikawa tofauti Ikawa sekta binafsi kudhibiti serikali kutokana na ufisadi wa viongozi.
Jpm alirejesha hali kuelekea nchi kujenga ujamaa kwa kudhibiti sekta binafsi.
Sasa fisadi na wapiga dili mnafurahia hali ya sekta binafsi kudhibiti serikali kurejea.
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
tukuone basi wewe ukitajirika kwa kupiga hela ya umma. Huyo muovu lake kubwa ilikua kupambana na ufisadi serikalini, kukusanya kodi na kusimamia miradi ya maendeleo. Kama wewe uliona ni uovu bila shaka utakua mtu fisadi.
 
Mwenyewe una utajiri gani? Vibajaji viwili na banda unajiweka kundi la tajiri😂. Magufuli aliungwa mkono na wasomi na watu wako vizuri tu sio unawaita maskini.
Mnajidai kupenda ubepari wakati wala sio ubepari mnafanya ila kufanya magendo kuibia umma na kutumikia maslahi ya ubeberu wa kimataifa. Kwa msingi huo kamwe nchi haiwezi kuendelea.
Isitoshe itikadi rasmi ya ccm ni ujamaa na kujitegemea. Ccm ilishabadili mkakati jinsi ya kujenga ujamaa. Badala ya kutumia sekta ya umma sasa ni kutumia sekta binafsi.
Ili kufanikiwa sekta binafsi lazima kudhibitiwa na serikali. Kilichotokea kikawa tofauti. Ikawa sekta binafsi kudhibiti serikali.
Jpm alirejesha hali kuelekea nchi kujenga ujamaa kwa kudhibiti sekta binafsi. Sasa fisadi na wapiga dili mnafurahia hali ya sekta binafsi kudhibiti serikali kurejea.
Thus alishindwa,sekta binafsi ndio nguzo ya uchumi.Ujamaa ubakie kwenye mgawanyo wa huduma za Jamii na sio kwenye msingi wa uzalishaji.
 
Hakuna kipindi nilikuwa mzalendo kwa nchi yangu kama kwenye utawala wa JPM nlikuwa na wivu na nchi yangu hatari. Kila aliyehujumu choxhote nlikuwa mkali as if ananiibia mimi
hukuawai kuwa mzalendo unajua maana ya uzalendo ww? kupenda nchi na sio mtu nachukua watu wa dizaini yako walio jipa uzalendo wakizani mfalme ni mungu ataishi milele ungekua mzalendo ungeonesha saiz jinsi unavyo fanya iyo Kazi ambayo ulikua unafanya mpaka usiku ili ulete tija na kuongeza ufanisa wazalendo wapo mpakani hawalali ili wewe ulale Salama huu ujinga nimeusoma kwako Zaid ya Mara moja (sorry kama nimetumia lugha mbaya no hard feelings dude)
 
Kipindi cha magu niliusika kwenye ujenzi wa majengo ya hospital ela ilikuwa on time ushindwe wewe na uvivu wako, now tangu mwezi wa sita tunazungushana pesa as if hazipo hadi zimerudi kisa kuombana rushwa na maengineer,procurement officers na uzembe wa DED yaan hadi kero.

Nashangaa hili bandiko lako kuna uwezekano mkubwa utakuwa wapenda shortcuts sana
 
Wajinga sana hawa watu.
Brain washed personel
hukuawai kuwa mzalendo unajua maana ya uzalendo ww? kupenda nchi na sio mtu nachukua watu wa dizaini yako walio jipa uzalendo wakizani kafalme ni mungu ataishi milele ungekua mzalendo ungeonesha saiz jinsi unavyo fanya iyo Kazi ambayo ulikua unafanya mpaka usiku ili ulete tija na kuongeza ufanisa wazalendo wapo mpakani hawalali ili ww ulaze matter ko yako Salama huu ujinga nimeusoma kwako Zaid ya Mala moja (sorry kama nimetumia lugha mbaya no hard feelings dude)
 
Habari!
Watu maskini, wajinga (waliokosa elimu), na wavivu ndio makundi ya watu waliokuwa wakifurahia harakati za Magufuli kutupeleka kwenye UJAMAA.

Hata.
UJAMAA hauwezi kufurahiwa na watu wenye bidii na vipawa katika utafutaji. Hata Wachina wanaukacha UJAMAA na kuanza kuishi kibepari, kila mmoja anakula kipawa na juhudi zake. Magufuli alipotumbua viongozi ilikuwa faraja kwa makundi hayo niliyoyataja, alipowafilisi mabosi kundi hili walishangilia.

Kundi hili kila siku linaishi likiamini kuwa matajiri wote ni mafisadi na wezi wa pesa zao. Kundi hili furaha yao ni kuona wa juu anashuka chini hata kama wao hawatapanda juu.

Umaskini mbaya wakuu.
Wewe ni ndezi sababu hasa watu tuliompendea Magufuli ilikuwa ni kuleta usawa. Haijalishi mlimchukia kiasi gani ila kila mtu aliefanya kazi alikuwa anaiona hela na kulikuwa na boost ya watu kufanya kazi hasa wa hali ya chini.

Huduma za kijamii zilikuwa zina tija hata ukienda maofisi ya serikalini ulikuwa unasikilizwa na kutatuliwa shida zako kwa wakati. Nidhamu ya kazi ilirejeshwa.

Msichanganye ubepari mnaotetea ni wizi na ubadhirifu wa mali za umma. Yani kwakuwa mlibaniwa mianya ya kudokoa ndio mnamuita Magufuli mjamaa sijui dikteta. Huo ujinga utawatesa kwa sababu tunahitaji kiongozi mwenye calibre ya Magufuli kututoa hapa tulipo. Gari imekwama bila 4-wheel drive!

Sahizi mmeruhusiwa ku edit mikataba kujiwekea 1O% maana boss hafatilii, tozo kibao, semina na warsha za kujiachia mnaandikia tu. Huku mtaani hali tete wanyonge wamefanywa wanyonge kweli kwa inflation za hali ya juu.
 
Zamu ya masikini kuisoma namba kupitia gharama za maisha na vitu bei juu, maana mlitucheka Sana sisi matajiri na wapinzani tulipokuwa tukishughulikiwa. Eti mnasema mbona wapinzani kina Lisu, Mbowe, zitto wapo kimya vitu bei juu, pambaneni na hali zenu , maana hata na sisi tulipokuwa motoni tukiteswa mlikaa kimya.
 
Kipindi cha magu niliusika kwenye ujenzi wa majengo ya hospital ela ilikuwa on time ushindwe wewe na uvivu wako, now tangu mwezi wa sita tunazungushana pesa as if hazipo hadi zimerudi kisa kuombana rushwa na maengineer,procurement officers na uzembe wa DED yaan hadi kero.

Nashangaa hili bandiko lako kuna uwezekano mkubwa utakuwa wapenda shortcuts sana
Jamaa walichukia sababu hio hela ya rushwa ilikuwa ngumu kuipata, yani walilazimika kuishi kwa mishahara tofauti na kwa JK ambako mtu mwenye nafasi alikuwa anafisadi hadi analewa na mipesa. Anaishi maisha yasio yake kwa kutesa wengine ila kwao freshi. Huu ndio ujinga wanahisi ni ubepari.
 
Back
Top Bottom