Sema ujamaa WA kisasa kama WA Kule Denmark ,Sweden ,Norway na Finland .Mi naona ule ndio unafaa Maana hata watu wanaishi hizi nchi tajiri za kibepari kama France na Germany wanatamani kuishi Kule Scandinavia ,lakini si ujamaa WA kizamani Ile WA akina Mao ,Stallin na Lenin ,Castro ule hapana .
Modern socialism kama ya Kule Scandinavia imelenga kutengeneza maisha mazuri Kwa raia WA kawaida pia kucreate opportunity ya mtu kutengeneza utajiri lakini bila kumkandamiza au kunyonya wengine . Haina Maana ya kuwa na utajiri WA matrilioni ili Hali unaishi katikati ya mamilioni ya watu masikini WA kutupwa na ombaomba , Huu ni ukosefu WA utu , ni utovu WA maadili ya kiutu .
Watu wengi wakiwa na maisha Bora ndio quality ya life itakuwepo , ndio Maana hizo nchi ni kawaida kabisa mtu kuwa milionea yet ni mfanyakazi WA kampuni husika ni kwasababu ya better payment na welfare system inayokuwa inforced na serikali za hizo nchi contrary na huku Africa ambapo unyonyaji Kwanza umerasimishwa na serikali ,kanjibai na mchina wanawatumikisha watu kama manamba ,mazingira mabovu ya kazi + malipo duni kabisa yasiyomwezesha mtu kuishi maisha Bora . Hili ni tatizo kubwa .
Sasa hizo nchi za Scandinavia hata crime rate ni ndogo Sana nearly zero mtu milionea lakini unaishi bila kuhofia kuvamiwa ,kukabwa au kudhurika ,Kwa sababu kila mtu anamaisha Bora hivyo hata uhalifu unakuwa Chini Sana .
Haya ndio maisha Bora sasa