Maswali 5 ya kujiuliza ktk Final submission ya Lissu

Maswali 5 ya kujiuliza ktk Final submission ya Lissu

Jibu rahisi: hata hizi habari ya migomo stendi ya Magufuli na kupotea kwa Nchimbi anazipata wapi? Jela hawanaga ITV? Ni wale mabeberu utawaona mahakamani kila siku. Wana mtu wao katika wafungwa mmoja wao akishirikuana na mmoja timu ya Lissu iliyo ndani anamfanyia research kimya kimya na kumfeed kila asubuhi.
Hizi sio fikisi kweli
 
1. Alipata wapi internet na kwa muda gani?
Ili kufanya research ya kina, kusoma hukumu, sheria, nyaraka na maamuzi mbalimbali, internet au chanzo kingine cha taarifa kingehitajika. Ikiwa alikuwa chini ya ulinzi, ni muhimu kujua alipataje na lini fursa hiyo.

2. Alipata muda gani wa kufanya research na kuandika?
Ikiwa muda mwingi wa mchana ulitumika mahakamani na alifika mahabusu usiku, ni muda gani halisi uliobaki kwa ajili ya kusoma, kufanya research, kuchambua hoja na kuandika submission?

3. Alipata muda gani wa kupumzika?
Submission yenye uchambuzi wa kina inahitaji muda wa kusoma na kufikiri. Ikiwa kazi hiyo ilifanyika zaidi wakati wa usiku, swali linabaki: alitumia muda gani kulala na kupumzika?

4. Siku nne zilitosha kwa kazi hiyo kwa mazingira hayo?
Si suala la kusema kwamba haiwezekani kuandika submission ndani ya siku nne. Inawezekana. Lakini mazingira ya mtu aliye nje ya ulinzi na mwenye kompyuta, internet, maktaba na muda wa kutosha ni tofauti na ya mtu anayehudhuria mahakamani siku nzima na kurejea mahabusu usiku.

5. Tofauti na upande wa serikali
Upande wa serikali ulikuwa na zaidi ya mawakili saba. Baadhi walionekana mahakamani huku wengine wakiwa nje wakifanya research na maandalizi. Hivyo, kazi inaweza kugawanywa kati ya watu kadhaa. Pamoja na rasilimali hizo, submission yao ilikuwa takribani kurasa tano tofauti na ya Lissu iliojikita ktk analysis.

Ndugu Malaria 2,
Kuhusu hoja zako tano ulizozivua kwa kina kuhusiana na mazingira ya Tundu Lissu kuandaa submission yake akiwa mahabusu, kuna mambo ya kisheria, kiutendaji, na kimfumo ya magereza (ndani na nje ya nchi) unayopaswa kuyazingatia ili kupata picha kamili ya jinsi suala hili lilivyowezekana:

1. Kuhusu kupata Internet na Chanzo cha Taarifa
Malaria 2, ni muhimu kutofautisha kati ya mfungwa na mtuhumiwa aliyepo mahabusu (remandee). Chini ya sheria za magereza na misingi ya Haki za Binadamu, mtuhumiwa anachukuliwa kuwa hana hatia mpaka ithibitike vinginevyo.
Lissu, kama wakili anayejitetea mwenyewe (Pro Se Litigant), anayo haki ya kisheria ya kupewa vifaa na fursa za kutosha kuandaa utetezi wake (Right to adequate facilities for the preparation of defense). Hata kama gerezani hakuna internet ya wazi, sheria inaruhusu mahabusu kuletewa nyaraka, vitabu vya sheria, na machapisho ya kisheria na mawakili wake au wasaidizi wake kutoka nje ili kujisomea.

2 & 3. Kuhusu Muda wa Research, Kuandika, na Kupumzika
Kwanza kabisa, unapaswa kutambua kuwa Tundu Lissu si mwanafunzi wa sheria anayeanza kujifunza vifungu au kutafuta sheria tangu mwanzo. Kama wakili mzoefu na nguli wa miongo mingi, anao uwezo mkubwa wa kiakili na kumbukumbu ya kichwani ya maamuzi mbalimbali ya mahakama (precedents na Legal Matrix). Anajua dondoo na kesi anazozihitaji, hivyo kazi yake kubwa inakuwa ni kuziunganisha na kuzidondosha kwenye karatasi (drafting), jambo linalochukua muda mfupi kwa mtu wa haiba yake.
Pili, Lissu hayuko peke yake; ana jopo la mawakili wasaidizi na wabobezi wanaoshirikiana naye bega kwa bega. Wakati yeye akiwa mahakamani mchana, jopo lake liko nje likifanya research ya kina na kukusanya maamuzi hayo ya kisheria.
Kisheria, kuna kitu kinaitwa Uhuru wa Mawasiliano kati ya Wakili na Mteja (Attorney-Client Privilege). Chini ya sheria za magereza na mikataba ya kimataifa, maafisa wa gereza hawatakiwi kabisa kusoma nyaraka za kisheria, kusikiliza mazungumzo, wala kufungua barua na makabrasha yanayotoka kwa mawakili kwenda kwa mtuhumiwa gerezani.
Hii ina maana kwamba mawakili wake wanapofika gerezani kumwona, wanamkabidhi makabrasha yaliyokamilika ya research na hata rasimu za awali (drafts) za submission hiyo. Kazi iliyobaki kwake usiku ni kupitia, kuweka marekebisho, na kuongeza uchambuzi wake mkuu. Kwa mfumo huu wa kazi, Lissu hahitaji kutumia usiku mzima kufanya kazi tangu mwanzo, na anapata muda wa kutosha wa kulala na kupumzika.

4. Je, Siku Nne Zilitosha Katika Mazingira Hayo?
Malaria 2, jibu ni ndiyo, zilitosha kabisa. Mazingira ya mahabusu kwa mtu anayejitetea mwenyewe yanatofautiana na mfungwa wa kawaida. Katika mifumo ya magereza duniani kote—ikiwemo magereza ya nje (kama Marekani na Ulaya chini ya misingi ya kesi maarufu ya Bounds v. Smith)—mahabusu wanaojitetea wenyewe hutengewa chumba maalumu, meza, viti, na muda wa ziada hata nyakati za jioni (nje ya masaa ya kawaida ya wafungwa wengine) ili kupitia maktaba ya gereza au nyaraka zao ili kulinda kanuni ya haki ya kupata mapambano sawa ya kisheria (equality of arms). Magereza ya Tanzania pia yanatambua haki hii na viongozi wa magereza huwapa fursa hiyo ili kutoingilia uhuru wa mahakama.

5. Tofauti na Upande wa Serikali (Mawakili Saba)
Ni kweli serikali ilikuwa na jopo kubwa la mawakili saba na rasilimali zote, lakini kwenye sheria, ubora wa hoja (substance) haupimwi kwa wingi wa watu au idadi ya kurasa.
Wakati jopo la serikali likiandika kurasa tano zilizojikita kwenye taratibu za kawaida, Lissu alisimama kama mchambuzi mkuu akisaidiwa na timu yake ya nje. Mwanasheria makini na mzoefu anajua udhaifu wa kesi na anajua wapi pa kugusa ili kubomoa hoja za upande wa pili. Ndiyo maana submission yake ilijaa uchambuzi wa kina (deep analysis) uliotokana na uzoefu wake binafsi na msaada wa timu yake, kitu ambacho hakihitaji mawakili saba kuonekana mahakamani ili kikamilike bali ushirikiano mzuri wa kisheria.
 
TAL ni moja ya baraka iliyojaliwq nchi hii kama vile Tanzanite,Mlima Kilimanjaro,Gas ya asili,Bahari na Maziwa,na kwa binadamu ndio anaingia TAL yeye hata Mwalimu angekuwepo leo hii angesimama nae
 
Yeye ndio alisema, Tena mahakamani. Walitaka afupishe, ndipo akadai anakesha kwa ajili ya hiyo kazi atafupishaje?.
Anaweza ongopa si malaika,najua jela ambako kibongobongo mahabusu huwekwa, kulala ni saa Tisa unusu
 
1. Alipata wapi internet na kwa muda gani?
Ili kufanya research ya kina, kusoma hukumu, sheria, nyaraka na maamuzi mbalimbali, internet au chanzo kingine cha taarifa kingehitajika. Ikiwa alikuwa chini ya ulinzi, ni muhimu kujua alipataje na lini fursa hiyo.

2. Alipata muda gani wa kufanya research na kuandika?
Ikiwa muda mwingi wa mchana ulitumika mahakamani na alifika mahabusu usiku, ni muda gani halisi uliobaki kwa ajili ya kusoma, kufanya research, kuchambua hoja na kuandika submission?

3. Alipata muda gani wa kupumzika?
Submission yenye uchambuzi wa kina inahitaji muda wa kusoma na kufikiri. Ikiwa kazi hiyo ilifanyika zaidi wakati wa usiku, swali linabaki: alitumia muda gani kulala na kupumzika?

4. Siku nne zilitosha kwa kazi hiyo kwa mazingira hayo?
Si suala la kusema kwamba haiwezekani kuandika submission ndani ya siku nne. Inawezekana. Lakini mazingira ya mtu aliye nje ya ulinzi na mwenye kompyuta, internet, maktaba na muda wa kutosha ni tofauti na ya mtu anayehudhuria mahakamani siku nzima na kurejea mahabusu usiku.

5. Tofauti na upande wa serikali
Upande wa serikali ulikuwa na zaidi ya mawakili saba. Baadhi walionekana mahakamani huku wengine wakiwa nje wakifanya research na maandalizi. Hivyo, kazi inaweza kugawanywa kati ya watu kadhaa. Pamoja na rasilimali hizo, submission yao ilikuwa takribani kurasa tano tofauti na ya Lissu iliojikita ktk analysis.
Bula shaka yoyote ile Sheikh Mwaipopo umeukubali mziki wa Lissu. Tukiwaambia yule Mwamba ana akili kupitiliza muwe mnatuamini. Lissu mmoja ni sawa na mawakili wote wa serikali.
 
Unaweza kesha mahabusu,au ana special privilege?.. maana saa Tisa alasiri ni kulala
Acha kuishi kwa kukariri wewe. Tangu lini gerezani wameanza kulala saa tisa alasiri? Au unamaanisha lile gereza lenu la siri mnalowapeleka wakosoaji wenu kabla ya kuwaua?
 
Dude Lissu achana nalo, IQ ile siyo ya dunia hii. Usimuone Magu fala kukimbilia bunduki japo na kwenyewe alidunda.

Mimi na wewe tungekuwa tumepigwa tu risasi ya kuparua sikiko bila shaka madishi yangekuwa yameyumba ila mwamba bado yuko njema kichwani.
 
Mbona unavyojibu ni kama vile wewe ndiye anayesemwa kuwa ni mbumbumbu?
😁😁 Mkuu, sasa ukisema watanzania milioni sitini ni mambumbumbu mtu mmoja unajitoaje?
 
Kwakifupi Tundu Lissu ni smart zaidi ya Allah na kipenzichake marehemu Muhammad.
Siyo vizuri hivo ndugu waheshimu mitume na manabii.

Kwenye biblia kuna watu waliadhibiwa na Mungu kwasababu walimpinga nabii Musa
 
Ndugu zangu Mungu yupo naye ni mkuu sana anatawala ulimwengu kwa haki, huruma na upendo.

Yeye ndiye mwenye hukumu ya mwisho.

Wote tutetemeke kwa hofu mbele zake.
Amina
 
Back
Top Bottom