Maswali kwa Profesa Musa Assad kuhusu mkataba wa Bandari

Ninakubali, yote mawili yanaenda sambamba, "njaa", na hilo la uluvi wa imani zao.
Profesa wa mahesabu anaongelea masuala ya sheria tena za mikataba ya kimataifa kana kwamba hilo ndo eneo lake la ubobezi...

Shida inakuja pale ambapo wataaluma wa sheria ndani na nje wanaukosoa huo mkataba kwa minajili ya urekebishwe na kadhalika lakini dah!
 
Huyu mbona anaongela HGA ambayo bado haijafikiwa?
 
Huyu mzee kaiharibu kwa sekunde
Harafu anapenda kutumia hilo neno kuwa watu hawana uelewa! Ha ha ha! Anajionaga anaakiliiiii! Ha ha ha! Kuwa profesa si kwamba utaelewa kila kitu.

Tena uprofesa unakuwa unaelewa jambo moja kiundani si mengi. Mfano kadri mtu anavyosoma na kuanza kupata shahada ya pili huyu anapunguza wingi wa kozi. Akipata Udaktari maana yake kafanya utafiti juu ya jambo fulani analolijua.

Uprofesa si kusoma darasani na kupewa maksi. Usomi mwisho ni Udaktari. Uprofesa unakuja mtu kesha andika makala, vitabu, na kufanya tafiti mbali mbali kisha unatunukiwa. Je kutunukiwa huku ndo kutakufanya ujione una akili ya kuwa mtaalamu wa kila kitu?

Prof. Assad uliheshimika acha ushabiki utakao kushushia heshima yako. Unajifanya mwanasheria wakati hujui tasfsiri za sheria. Ulitakiwa uje na hoja kutuonesha kiuchumi uwekezaji huu wa bandari utafaidisha nchi kwa asilimia ngapi na baada ya miaka kumi Tanzania uchumi wetu utainuka kwa kiasi gani. Huu ndo utaalamu wako. Ungeeleza hicho tungekuelewa sana. sasa hata utaalamu wako hujautumia katika tafsiri ya kiuchumi ya huu mkataba.

Si kuja unajifanya unajua mno sheria wakati wataalam wa sheria wameongea.
 
Maprofesa ni akina MO, GSM, Rostam, Marehemu Mengi hawa wengine ni matapeli tu
 
Maprofesa ni akina MO, GSM, Rostam, Marehemu Mengi hawa wengine ni matapeli tu
 
Hilo swali la kwanza ni la kinafiki sana, kuna miradi mingapi imekua implemented Tanzania Bara na haijawahi kuulizwa mbona Zanzibar haipo.!

Msingi wa hilo swali ni personal attacks na si linginelo.
Jamaa wanafik Sana,, hiv kweli DP World ikawekeze visiwani?
 
Kw Sasa Do world ikawekeze Bandari iliyo kisiwani? Nchi gani inategemea kusafirisha mizigo yake kupitia ZANZIBAR?
 
Nilichojifunza hawa wenzetu mtu wa upande wao hata akiharibu huwa hawajihangaishi nae.
wako brainwashed sana na imani yao.
 
Maprofesa ni akina MO, GSM, Rostam, Marehemu Mengi hawa wengine ni matapeli tu
Leo nitofautiane nawe, ingawaje najua unacholenga wewe.

Hao wote uliowataja hapo, mimi ningwaita "majizi". Wengi wao hawakulipa kodi stahiki, wengine ndio waliotufikisha huku kwenye rushwa za kipumbavu kila mahala; na mambo mengine maovu tu mengi yanayowahusu na kuwawezesha kufika hapo.

Kama huo ndio u-profesa, nitakubaliana nawe.
 
Unadhani waliopo ofisni hawaibi? huwezi kuiba bila kuwa na watu serikalini, kama ni hivyo maprofesa ni akina JK, Chenge, Mwigulu, Makamba, Mbarawa, Ummy n.k sina tatizo kama mtu anaiba anawekeza hapa hapa nchini angalau ndugu zetu wanapata ajira n.k hawa niliowataja wameiba na kuficha nje
 
Nimemsikia huyu mwanasheria wa Ujerumani. Anasema huu Mkataba tunaoujadili sasa ni wa Host Government Agreement (HGA). Wenzangu mmeuona huo mkataba nimetafuta sijauona. Umeingiwa lini halikuwa mazungumzo ya HGA yalikuwa yakisubiri kuridhiwa kwa IGA?
 
Waliopofanyia wanajua wenyewe mimi nimenukuu kauli ya Makamo wa pili wa Raisi wa Zanzibar mh Hemed na sio hilo tu kuna kero nyingi tu washazitolea maamuzi hayo ya katika labda kwa vile katiba sio msahafu kumbuka hata jecha alifuta uchaguzi na hiyo katiba haimpi mamlaka hayo
 
Baadhi ya majibu ya maswali yako haya hapa:

Profesa Issa Shivji anasema Mkataba huu ni treaty yaani mkataba baina ya nchi na nchi na nchi hiyo ni Tanzania na nchi nyingine ambayo ni ngumu kusema kama ni nchi au la.

Ila kuna jambo ambalo limejitokeza katika hilo maana katika treaty lazima kuwepo nipe na nikupe baina ya wawili katika mkataba. Hilo halipo bali haki zote amepewa Dubai huku wajibu wote amepewa Tanzania bila haki. Yaani mkataba umekuwa uwekezaji ingawa unaitwa ni mashirikiano. Ila ushirikiano huo si wa kijumla bali ni wa bandari na mwekezaji ametajwa ni DP World siyo wawekezaji wa kijumla wa kuhesabika kwa namba makampuni au wafanyabiashara kutoka Dubai.
 
Mkuu 'Benjamin', kama "huna tatizo nakama mtu anaiba...', basi wewena mimi tupo mbalimbali kabisa. Kwangu mwizi ni mwizi tu, nina tatizo naye, hata kama utampa sifa ya ziada ya huko anakowekeza.

Sijawahi kusikia sheria yoyote dunani ikitoa hukumu tofauti, kati ya wezi wa ndani, na hao wengine wa nje.
Najua hiyo dhana yako inashawishi wengi kuona hivyo, unavyoona wewe, lakini wote mbele za sheria ni wezi tu.
 
Upo sahihi mkuu lakini kwa mfumo wa Tanzania wizi hautaisha, niambie mara ya mwisho tangazo la ajira za bandari, TANAPA, BOT, Ikulu, mambo ya nje n.k uliona lini? je watu hawaajiriwi hizo sehemu? jibu ni kwamba sehemu nono zote wamewekwa watoto wa kubwa na ndugu, pia wanafundishwa wizi tangu siku ya kwanza, wezi wa kubwa Tanzania ni wale wanafunga tai na kulindwa na vyombo vya dola 24hrs badala ya kukamatwa. Hakuna namna acha yaibe mpk sisi wananchi tupate akili tuyakatae haya majangili
 
Je, Profesa Assad kayaona haya na kuyatolea majibu anayoyajua yeye kwa uelewa wake wa kitaalam?

Tuache kuzungukazunguka na mambo mengine ya pambani, kama hilo la "Bandari kuuzwa" wanalopenda sasana kulitolea ufafanuzi.

Haya hapa ndiyo yanayohitaji ufafanuzi wa kina kabisa kwa utaalam wao.
 
Katika hili prof Assad asingetoa comment yeyote na asingepungukiwa na kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…