Bado ninatofautiana nawe kabisa mkuu 'Benjamin'.Upo sahihi mkuu lakini kwa mfumo wa Tanzania wizi hautaisha, niambie mara ya mwisho tangazo la ajira za bandari, TANAPA, BOT, Ikulu, mambo ya nje n.k uliona lini? je watu hawaajiriwi hizo sehemu? jibu ni kwamba sehemu nono zote wamewekwa watoto wa kubwa na ndugu, pia wanafundishwa wizi tangu siku ya kwanza, wezi wa kubwa Tanzania ni wale wanafunga tai na kulindwa na vyombo vya dola 24hrs badala ya kukamatwa. Hakuna namna acha yaibe mpk sisi wananchi tupate akili tuyakatae haya majangili
Mimi ninaamini kabisa kwa dhati ya moyo wangu, kwamba haya matakataka tunayoyaona na kuyafanya kuwa ndiyo kawaida ya maisha yetu, inawezekana kabisa kuyapunguza sana (hata kama si kuyamaliza kabisa).
Ni swala la kupata viongozi sahihi tu wenye dhamira ya dhati kufanya hivyo.
Michina ni mijitu mizi sana ile. Nchi ile inao watu bilioni na zaidi..., huko kwao hawafanyi mambo kama unayoyaeleza hapo juu. Hawa watu wanapokuja hapa, wanatabia za kutaka kukwapuakwapua kila kitu, kama meno ya tembo, n.k..
Hata inafikia kwenye baadhi ya nchi, wachina wenyewe wamejiwekea polisi wao na jela zao, ili kuwadhibiti mijizi yao.
Hizo nchi za huko Mashariki ya mbali, tunakoambiwa uchumi wao unaenda vizuri, na kupata maendeleo ya haraka.
Usidhani hata mara moja kwamba hawana mijizi huko, hata kwenye serikali zao, lakini wamejiwekea taratibu za kuwabana hawa washenzi.
Hapa kwetu, CCM yenyewe ndiyo inayorutubisha yote hayo uliyoyaeleza kwenye andiko lako hapo juu.
Kwa hiyo, waTanzania wanajua kabisa wapi pa kuanzia, kuondoa uozo huo uliouelezea vizuri sana wewe hapo juu.
Bila kuwashughulikia CCM, usitegemee mabadiliko yoyote.