Upungufu wa mafuta upo lakini sio Kwa kiwango cha kutisha, Meli zinapita kama kawaida lakini sio nyingi kama zamani, Mabeberu wameona wavuruge kidogo ili wapandishe kidogo Tu wapige pesa na watu watazoea Tu.
Iran anajijua kabisa kuwa Hana uwezo mkubwa wa kiteknolojia kushinda Israel & US, Alichofanya ni kutafuta udhaifu wao na kuwapiga Kwa kusaidiwa hasa kimiundombinu na Urusi, Hakuna mfumo perfect hata siku moja lazima Tu kutakuwa na loopholes.
Ukiangalia in reality Israel anaonekana anajua na anaweza kufikia vitu vingi ndani ya Iran kuliko Iran anavyojua ndani ya Israel, Licha ya udanganyifu wa Netanyahu lakini ukisikiliza baadhi ya hotuba zake utaona kabisa ni mtu anayejiamini Sana na hii inatokana na kupata taarifa za Moto Sana ndani ya Iran, Mfano Khamenei alipouawa, Netanyahu alisema Kwa kujiamini Sana kuwa Khamenei ana uwezekano mkubwa wa Kutokuwa Hai means deep kabisa kwenye level za juu kabisa za usalama za Iran wako Mossad ambao wanatoa taarifa field kabisa, yaani real time information before hata Iran wenyewe.
Kampeni ya regime change imekuwa ngumu Sana Kwani imeshindikana namna ya Ku organize watu waingie barabarani, waandame na kuleta vurugu za muda mrefu, wale Jamaa Basij forces Kwa kiasi Fulani wamejitahidi, IRGC wamezidi kubaki imara Kwa namna Fulani. Ili uangushe utawala lazima upate support ya wananchi wenyewe sasa kama wananchi wamenyoosha mikono nyie kina US mtafanya nini?,
Hebu jiulize sasa hizi Iran ukisema upigane nae hata hujui unapigana na Nani coz IRGC sio mtu mmoja ni mamilioni ya wanajeshi, Ayatollah hajulikana alipo, unakutana na Abasi Aragchi na Yule Ghalibaf, Masoud Pezekshan na hao Jamaa watatu huwezi kuwaua sababu ndio watu watakao wezesha majadiliano ukiwaua hao mambo ndio yanazidi kuwa mabaya,Yaani hata namna ya Kujadiliana nao inabidi uwe makini, wale Iran walijipanga Sana na kufanya Ugatuzi wa madaraka mapema kiasi ambacho Kuna layers mbalimbali zinazoweza kuendesha nchi Kwa namna yake hata Ayatollah akifa sasa hivi...
Ishu ya Urusi ni kwamba yeye anapiga na NATO kabisa, Urusi anapigana na nchi nyingi pale...