Maswali muhimu kwa chanjo ya COVID-19


Maswali yako mawili yaikuwa wazi:



Majibu yangu kwenye red pia yalikuwa wazi na cha mno nikakutaarifu wapi unaweza kusoma zaidi:



Kweli sikujibu maswali yako au una maswali mapya? Au majibu yanayoashiria mafanikio wewe huyapendi kwa sababu zako tu?

Kama una mapya haya je, tumemalizana nayo? Nitafurahi kuyajibu mapya lakini kwanza nijue if we are making progress.

Au vipi mjomba?
 
Check out mataifa makubwa Africa... India, South Africa etc wamekubali chanjo... lakini kinachoendelea Virus wamebadilisha tabia.... Hiyo Vaccine ya C-19, yenyewe ni virus.... Bill Gate na wenzake wanajua ukweli wote..... Tuendelee kutumia dawa zetu za asili... kupambana na mafua..... Hii ni World New Order... tuwe makini sana wa Tz....
 
Hiyo taarifa ni ya lini maana sijaisikia ikitangazwa
Au ni hisia tu za yule bos wa who ambae alisema afrika watu watakufa kama mizoga bila utafiti?
 
Kwahiyo wamekaa ku-conspire kukuua wewe kwa gonjwa na chanjo lakini gonjwa likatapakaa na kuwaua na wao kwa bahati mbaya sio?!? Na chanjo wakaanza kujichanja wao ili kukutega wewe tu mkuu. Haya nita-wake up!
 
Very true and precise. Kuna jamaa m'moja ni dokta wa muhimbili tulikuwa na hii discussion. Namna umeilezea ni 80% ya nilichokuwa nakizungumza but niliongea zaidi.

Kilichoniuma kwa upande wa wasikilizaji walikuwa wana mfavour jamaa na kumsikiliza cheap argument yake sababu eti ni dokta na anajua anachosema. Mimi nikaambiwa nina fanya ubishi plus natoa hoja zangu mitandaoni.

Nikasema bongo ndio maana maendeleo ni kwa wachache sana. Watu wanaweza kusoma ila bado upeo ukawa chini sababu ya uwezo mdogo wa kujenga hoja na kuitetea.

So kwa nilichojifunza siku ile ni kuwa majority ya watanzania bado kuna ujinga mwingi sana na hii ina dhihirika kupitia namna watu wanayachukulia mambo mazito kirahisi na mambo marahisi kiuzito isivyo stahili.

So big up sana kwako kwa kuongea kwa kuchanganya akili za darasani na za kwako pia binafsi. Huu ndio usomi haswa unaovyotakiwa.
 
Hoja hapa sio mataifa ya magharibi kutudhuru tu, bali pia hoja iliyopo ni kwann tudeal na tiba za magonjwa kwa kutegemea dawa kutoka kwa watu wengine.

Kwa usalama wa taifa hii ni hatari sana. Ina maana tuna hela za kuwalipa CCM mishahara minono, wanajengeana majumba ya kifahari ya mabilioni baada ya kustaafu, kuwapa mamilioni kizembe tu ila hatuna pesa za kufanya tafiti zetu binafsi na kuja na dawa au kinga zetu kama Tanzania?!

Hapa ndio shida inaanza tunaona vya kupewa na kuletewa ni nafuu ila kuunda vyetu ni gharama.

Aiseee.
 
I agree mkuu.
 
Hivi before chanjo ya polio, unazo takwimu za kipindi hicho?!
 
Akiendelea kubisha atakuwa ana mgao wake katika hili swala la chanjo chanjo za covid. Si kila raia ni mzalendo.
 
Kuja kwa chanjo sio hoja hoja ni je tumejiridhisha?
Pelekeni upopomaa wenu huko? Unaweza kujiridhisha na kitu ambacho huwezi hata kujua kimetengenezeaje? Magufuli aliwajaza ujinga sana. Semeni basi na yeye ni hofu ilimuua.
 
Hivi before chanjo ya polio, unazo takwimu za kipindi hicho?!
Pitia

 
As a scientist sikukubaliana na narrative ya the mainstream media,Bill Gates,
Mkuu, ebu nisaidie kuelewa huyo Bill Gates anaingiaje kwenye issue ya Corona wakati yeye siyo mwanasayansi? Hainiingii akilini!
 
Mkuu as much as napenda kukuunga mkono ila nashindwa kureason na wewe eneo moja tu. Mbona kama upo so convinced kuwa tunawahitaji sana kwa kila kitu.

Its true kama hatuwezi kuishi bila kusaidiana au kusaidiwa. Its obvious sisi ni taifa changa sapoti kwetu ni muhimu. Ila si muda wote utalegeza misuli unapopatwa na tatizo utegemee kusaidiwa.

Ngoja nikupe tu siri moja. Hivi unajua ni race ipi inaongoza kwa idadi kubwa ya watu.

Unajua waafrika tupo wa ngapi dunia nzima roughly??!

Hivi unajua one of the most virgin continent ni ipi duniani ??!

Umeshajiuliza kwann wachina na mataifa mengine wanajifunza kiswahili kwa kasi sana?!

Je unajua hizi device nyingi kama simu, decoder, router, laptops and desktops, etc kutoka china ni vifaa maalumu vya kukusanya taarifa zetu na kuzifanyia kazi?! Bila kusahau social social media na network kama Facebook , whatsapp, Instagram etc ni agency za kukusanya taarifa zetu?!

Huwa nasikitika sana ninapokutana na mwafrika anae jitoa ufahamu kuamini jamii ambayo miaka kadhaa nyuma walikuwa ni wakoloni kwetu leo ghafla watakuwa walinzi wetu.
 
Kwahiyo wamekaa ku-conspire kukuua wewe kwa gonjwa na chanjo lakini gonjwa likatapakaa na kuwaua na wao kwa bahati mbaya sio?!? Na chanjo wakaanza kujichanja wao ili kukutega wewe tu mkuu. Haya nita-wake up!
tumia akili mkuu.

kipindi tuko jkt kuna afisa mkuu wa kambi ulikuwa ukikosea,anaanza yeye kujigaragaza kwenye matope na kubebba magogo,lengo ni......

sasa nyinyi watu hamtaki kabisa kutumia akili.
 
Mkuu, wala sikupingi. Nachopinga ni unafiki wa watu kuchagua kupinga chanjo pekee kana kwamba ndiyo silaha kubwa wanayotumia wenzetu kutumudu

Hivyo ulivyotaja vyote kuanzia teknolojia ya mawasiliano hadi uwekezaji vinatumika na wenzetu kwa maslahi yao pia. Tunapaswa kujenga uwezo wetu wa ndani kama nchi au kikanda kwa masuala ya kimkakati ili kulinda utu wetu siku za usoni.

Tunachokishuhudia ni unafiki wa kisiasa na kelele tupu bila ufumbuzi wa kisayansi. Watu tulifikia hali ya kukataa tatizo kwa kuamini kuwa halipo huku dunia nzima ikituona kituko.

Tuna vingi vya kurekebisha hasa kuanzia elimu yetu . Huduma za maji, afya na tafiti. Hizo rasilimali ilizotaja afrika hatutanufaika nazo kwa aina ya misingi na wanasiasa tuliyonao. Sehemu kubwa bara la afrika, Wanatutawala kupitia hawahawa viongozi wetu wala hawana haja ya kurudi tena huku
 
Akiendelea kubisha atakuwa ana mgao wake katika hili swala la chanjo chanjo za covid. Si kila raia ni mzalendo.
si bora awe na mgao utatufaa kwenye mzunguko wa pesa.huyo mbuzi na mwenzake humu ni wapuuzi wa kiwango cha juu kabisa.

hakuna jambo wanajadili bila kuingiza hisia zao za kisiasa.
 
Nachotaka kusema kwa ufupi, matatizo mengi ya kwetu ni ya sisi wenyewe zaidi , tunajazwa hofu ya adui aliyeko nje kuliko kushughulika na adui ujinga na umaskini tulio nao ndani.

Leo, wanasiasa wetu afrika wanaishi maisha tofauti tena ya anasa kuliko wale wa nchi zilizoendelea. Huku wananchi wakiogelea umaskini wa kutupa. Adui yetu mkuu yupo ndani tupasafishe kabla ya kumkabili adui wa nje mwenye nguvu maradufu. Vinginevyo tutaendelea kuwa debe tupu
 
Hivi unajua kua Population ya India ni sawa na population ya watu waliopa bara lote la Africa? Wahindi wapo zaidi ya 1.3 Billion,

Sasa unajua ni asilimia ngapi ambao tayari wana chanjo ya Covid-19? Kutengeneza Vaccine na kuchanja watu 1.3B sio kazi ya muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…