Cool running unaongea na mtu mzima tena mwenye busara sana kuliko unavyomfikiria. Ni vyema kama unaitaji elimu maneno yenye muelekeo ya kupotosha au kejeli yakaepukwa ili kuendeleza mjadala huu. Mimi nipo kitambo katika mjadala huu nafuatilia kwa makini na sipendi ufungwe bali nataka niendelee kupata ujuzi wa historia ya nchi yangu.
CHAMVIGA,
Tatizo liliopo si kwamba yakua,Bwana
Mohamed Said ati "anakimbia" masuali/hayawezi kuyajibu au mie nataka asiulizwe/asijibu,hasha abadan!
Itakua tunakwenda kinyume kabisa na
dasturi za taaluma,ati sisi kuzuia mwangine asijibu masuali ya kitaaluma!? Duuh!
Hivi
kimantiki weye hujiulizi...yakua huyo "
Bwana Mdadisi" mwenyewe ameshatujuza hapa yakuwa,yeye na Bwana
Mohamed Said ati "wanafahamiana" kiundani,na pia wanawasiliana kwa e'mails!?
Sasa tujiulize ni kipi kilichowafanza
Wanataaluma hawa waili wenye kufahamiana na kuwasiliana,ati washindwe kupanga au kufikia
muafaka baina yao,wa jinsi gani ya
kujibizana/kuhakiki shughuli zao za kitaaluma!?
Kwanini huyo
Udadisi hakuona haja ya kumfahamisha Bwana
Mohamed Said ati hiyo dhamira yake
"njema" alonayo ya kuhakiki hicho kitabu...na pia kumuomba/kumtaarifu yakua baada ya hapo majawaba yako yoote nitayachapisha rasmi au nitayaweka mitandaoni-
JF,ili
Wasomaji wangine nao wakusome na kupambanua/kujiamulia
ukweli au
"upotoshaji" wako!?
Sisi soote tunafahamu history ya
machafuko ya lugha,khasa matusi,kebehi,tashtit na
chuki zilizomo humu-
JF takriban penye thread/s zoote zinazomukhusu
Bwana Mohamed Said...na hata
Udadisi pia amekiri kufahamu hili!
Sasa,ndipo sisi wangine tunapojiuliza yakua...hiyo dhamira njema ya huyo "
Bwana Mdadisi",haikuwezekana popote pale au kwa njia nyangine,shuruti amletee mwenzie
msuto/cross examination humu-
JF,ilihali anafahamu
madhila na
tafrani zitakazotokea kwalo!?
Mie binafsi najitolea kuchapisha kwa
gharama zozote zile na kuzigawa copies zoote
bure,kijarida cha majawaba cha hayo masuali ya
Udadisi kutoka kwa Bwana
Mohamed Said...ikiwa tu yatapelekwa kwa tartib za
muafaka na
staha za kitaaluma!
Pana wakti huyo huyo
Udadisi,naliona baadhi ya post/s humu akilalama kiduchu yakua hajapatapo
access ya makabrasha ya
Sykes Family!? Sasa hajiulizi kwanini ilihali yeye ni mwanataaluma/mtafiti "alobobea"!?
Nimeona kwenye mojawapo ya bayana zenye hayo aitayo ati ndo masuali yake ya "kitaaluma" huyo
Udadisi...anauliza je
Bwana Kondo Kipatwa ndo kweli aliweza kuwa
Mwafrika wa awali kuwa na Radio hapo
Tanganyika kabla ya
Paul Bomani au
George Kahama!?
Sasa kama yeye
anayo majawaba tafauti au ana watu wangine kumbe akiwafahamu wa huko
mabara,ambao walokua ndo wenye hizo radio za awali kwanini asituwekee hapa jamvini!?
Naona pia
Udadisi ameweka hiyo link ya
Sheikh Mtoro Bin MwinyiBakari,labda kuzidi kumchachafya
Sheikh Mohamed Said!?...sasa anawafahamu
family/vizazi vya huyo Bwana,ambao waliopo mpaka kesho hapo nchini ni akina nani...na vyeo/shughuli zao Serikalini!?
Huyo hakuna
direct historical evidence yakua ati
Sheikh Mtoro Bin MwinyiBakari alikua na Radio hapo
Dunda wala
Bwagamoyo mjini wakti ule!
Huyo
Ngongo,ni mstaarabu
kiduchu...lakini kinachomharibia kwa Sheikh
Mohamed Said ni hizo lugha zake za
"ki-Arusha"/za kihuni! Na pia ninakhis labda ana
allergy na
"Wazee wa Gerezani"/Kariakoo!?...mtafanzaje jamaa zetu,na ukweli ndo huo yakua wao walitangulia kufika...na pia ndo
Wanamji!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!
Pana mangi ya kunena...lakini nakwacha maana vijisughuli vimenikinza hapa kibaruani!
Ahsanta.