Maswali ya kijinga wanayouliza wanawake wakitongozwa

Maswali ya kijinga wanayouliza wanawake wakitongozwa

Hakuna upuuzi na chukia sana kama mwanamke aniulize kwanini niliachana na mpenzi wangu aliyepita alafu hapo hapo anakuambia sasa uzuri wangu ni nini mpaka unipende?

Yani nachukia sana na akifanya mistake tuu akachanua naongeza single mother chapu

Ni maswali ya msingi hayo.. kama kweli upo serious na mtu..

But hayo maswali huwezi kuyauliza kwa siku ya kwanza hili swali la kwanini uliachana na ex wako ni la msingi… na hii si kwamba mtu anataka hiyo sababu hapana ni vile anataka kuthibitisha kama kweli mmeachana
 
Hio " mi nina mtu wangu "

Kuna dogo Under 18 huwa anashinda dukani, duka lao lipo karibu na clinic moja hivi so huwa naenda kupata bites na maji hapo, vikibaki vichenchi chenchi namuachia,mwishowe tukazoeana

Nikaomba namba siku mbili mbele nikashusha stanza. Akaniambia nina mtu wangu. Siku nyingine pia nikakumbushia akaniambia the same. Nikaachana nae.

Siku akaniomba hela amemiss kula kiepe, nikamtumia kumbe anadaiwa songesha, voda waka offset juu kwa juu

Badae analalam kuwa katoa hela kidogo, nikasema aache kukopa, akajibu Mimi sitaki nimechukia na bado njaa inaniuma, nikamkumbusha kuwa anabwana wake akasema wamegombana.

Nikasema bado anawajibu wa kukuhudumia si anakukula, akapotea.

Masaa kadhaa mbele naambiwa mambo, namjib poa, ananambia kichwa cha muuma, nikasema amwambie bwanake afu aache kunitafute kama ambavyo mimi simtafuti.

Ikaisha hivo

Katika kutongozwa kwangu sijawah kusema nina mtu Kama sikutaki nitatafuta uongo mwinginee tu

Niseme nina mtu nikose hela kama huyo binti hapo[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Utasikia unaomba namba yangu ya nini?

Sasa Kuna Yale mapumbavu unaomba namba linakupa namba ya mshikaji wake ,ukioiga unakuta mwanaume anapokea unaishia kusema nime wrong namba.

Akijifanya kiherehere anakula matusi yeye na Mwanamke wake mpumbavu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Huna hela tu

Ukiwa naZo tunatoa namba hadi za wazazi wetu
 
Wewe una bahati sana kuulizwa maswali ya kupumbavu! Sisi tunapewa majukumu kabisa😀😀 Kodi ya nyumba inakaribia kuisha huku unajua kabisa anakaa kwao! Ufala huu
Kuna maswali ya kijinga huuliza wanawake ukianza kumtongoza. Nasema ya kijinga kwa sababu anakuwa anajua majibu yake au anajua kabisa hawezi kuambiwa ukweli.

Anauliza
1. Mimi ni mwanamke wako wangapi?
2. Hivi kweli huna demu mwingine?
3. Hivi kweli hutonichiti?
4. Hivi kweli utanijali?

Hivi kweli kuna bwege atakutajia idadi kamili ya mademu aliogonga? Au kukuambia ndiyo ana demu mwingine?

Ongeza maswali mengine ya kijinga
 
Mideko kuna mashtaka yako nitafute upesi
ab14f899b6741f9ded0893eaa75c715c.jpg
 
Back
Top Bottom