Matapeli wa kimapenzi mtandaoni kutoka west Afrika

Matapeli wa kimapenzi mtandaoni kutoka west Afrika

Kuna kipindi kiko NatGeo channel 181 DSTV na pia Azam wanayo siko surr ni channel namba ngapi.

Hiki kipindi ni mwanadada anakuwa anafuatilia biashara flani haramu to the source anazungumza na clients na wauzaji au wale victims, na watendaji wa uharamia.

Ashahoji wauzaji madawa wa mexico, wezi wa magari US, clinic haramu za kuongeza makalio US yani anaenda to the source na akiwa anawahoji wanakuwa wamevaa masks japo wauza madawa hawavai masks wengi wao huko mexico.

Sasa wiki hii alikuwa nafuatilia hawa scammers wa mtandaoni wanao scam watu kupitia kujifanya wanawake au wanaume kupitia dating sites.
Hivyo alisafiri mpaka Ghana ambapo biashara hii imeshamiri. Anasema inaanza Nigeria then Ghana.

Aisee ni biashara kubwa sana na sio rahisi rahisi. Kumbe wana script za nini waandike na nini waseme, unakuta ni kikundi, wana wataalamu wa graphics, wana mtaalamu wa IT yani crew.

Na kuna boss ambaye wanawaita finisher. Huyu yeye ndiye anakuwa anatafuta potential clients akishawapata anawasukumia sasa hawa wa chini wa deal naye ela ikitumwa naipokea boss hawa wa chini wanapewa % kidogo.

Wanakwambia zamani ilikuwa rahisi kuwascam watu kwasababu mambo ya video call yalikuwa hayapo now ngumu. So, mtaalamu wa IT unakuta ametengeneza system anatumia video ambazo wanasema nazo wanazinunua yule mtu akiwa anachat na mtu via dating site anaona huyo mtu kwa video anatype so anaamini kweli ni mtu really kumbe ni video imesetiwa.

Wakioiga calls za kawaida wanaongea wnaume ila wana tune sauti kuwa za kike, ila kuna muda wanainvolve na wanawake.
Kilichonishangaza zaidi wanatumia pia black magic. Mtu wakiona hatoi pesa, wanaprint picha yake inapelekwa kwa mganga anaifannyia mambo, wanadai ela inatoka hata mtu aambiwe anataka dollar 20000.

Pia wengine wana guilty consciousness kuna mmoja anadai alimscam mwanamama mmoja pesa akajiua, mwingine anasema alimscam mwanamama ela ya nyumba.
Wanadai wanaume ni rahisi kuwascam kuliko wanawake.

Pia akatoka hapo akawahoji victims, na imegundulika wanawake ndio wakiibiwa hujiweka wazi wanaume hata.
Sema kuna watu wa kuwatrack. So kuna mmoja alikuwa anataka kumscam mwanamama kumbe mwanamama ashamshtukia, so akaendelea playa dumb. Jamaa alikuwa kaweka picha ya mwanajeshi wa US anadai yuko middle east so akamwomba amtumie dola 4000 via bitcoin.

Mwanamama alikuwa ashamwandaa jamaa ea kuwatrack, akamdanganya ametuna yule jamaa alikuwa amemtumia link flani amtumie huyo scammer yule scammet alipoclick tu ile link jamaa akadaka location yake kuwa yuko ghana accra.

Hao scammer wanakwambia kuna watu wakubw Ghana ndo viongozi wa hiyo kitu na ukijaribu kuwafuatilia you can end up dead.

Wazungu wametuibia sana, acha vijana wa kiafrika watumie taaluma zao kurejesha utajiri wetu nyumbani.
 
Sema kibongobongo hawajawekeza sana.
Wanapiga hela ndogondogo sijaskia ishu kubwa za kitapeli, au zipo mimi ndo sijui??
Zipo nyingi zinaendeshwa chini ya maji. Ukikomaa sana mnagawana nusu hasara. Unapita hivi.

Sasa wazee wa Goodmorning unawashtaki wapi ? Huku lazimishwa wewe mwenyewe umejaa upepo.
 
Sisi vijana wetu wanacheza chini bado wako kwenye style ya "ile pesa tuma kwenye namba hii"
Kuna lipumbavu limoja hapa limetoka kunipigia simu si muda mrefu kwa no ngeni likijitambulisha kuwa mi ni flani toka Airtel, karibu mteja niweze kukusikiliza na kukusaidia shida yako yoyote, nikalijibu "sihitaji huduma zenu zozote toka Airtel" likastuka na kukata simu ghafla [emoji12]
 
Siku akidakwa na yeye anaunganishwa kwenye tukio...ndo atajua hajui
Washalala wote ndani enzi hawajaona. Pesa kitu kingine.
Kuna mdada rafiki yangu kaolewa na jamaa flani, aliniambia wakati wana date alikuwa anahisi jamaa anauza unga maana alikuwa anatembea na mabahasha ya eka halafu anakutana na watu anawapatia au anapokea bahasha au mabegi ya pesa.
Sasa nikamuuliza kwanini hukuachana naye?
Jibu akawa hana ila bila shaka ni pesa ilikuwa inamchanganya.
 
Hata hapa TZ kuna mambo mengi na mauaji na kesi kama ingekuwa inaruhusiwa ma investigative journalists wafanye yao tungebaki kushangaa.
"Mohammed Ali: Jicho pevu" alikuwa anakuja vizuri sana, mwisho wa siku akaingia kwenye siasa/ kazi na kofia mbili.

Jerry Muro kile kipindi chake, si uliona kilivyomletea kelele.
 
Matapeli ni watu smart sana sana. Yani anakufanya unatoa pesa mwenyewe bila kushikiwa bunduki baadae unakuja jiona mjinga na signs zote zilikuwa wazi lakini hukushtuka.
Hiki ndo kinanishangaza sana [emoji848]
 
Huyu ni nomaz..

Kule insta kwenye page yake kumejaa maneno ya busara na hekima, motivation speaker fulani, ana ofisi eti kali (picha plus video) anakushauri jinsi ya kucontrol your money[emoji1787][emoji1787]

Jamaa amejipanga si kitoto asee
Siku hizi watu wanakutapeli unafahamiana nao kabisa,binadam wamebadilika jamani
 
"Mohammed Ali: Jicho pevu" alikuwa anakuja vizuri sana, mwisho wa siku akaingia kwenye siasa/ kazi na kofia mbili.

Jerry Muro kile kipindi chake, si uliona kilivyomletea kelele.
Hivi huyu mohamed Ally ndiye alitengeneza na ile ya west gate kuonyesha wavamizi waliondoka muda tu askari wako tu wanaiha biscuit ndani?
Tz ngumu maana hata polisi hawawezi kukupa ushirikiano
 
Hata hiyo imeongelea from the scratching point na ilikuwa sponsored na viongozi ila ilivyokuwa hatari na uchaguzi ulivyoisha amani ikapatikana. Ikabidi wauawe.

Aiseeh mfatilie huyo jamaa vipindi anaitwa Ross Kemp.... ni hatari mkuu. Inatufundisha namna ya kujua uhalisia wa vitu.
Kipindi kinaonyeshwa wapi?
 
Hivi huyu mohamed Ally ndiye alitengeneza na ile ya west gate kuonyesha wavamizi waliondoka muda tu askari wako tu wanaiha biscuit ndani?
Tz ngumu maana hata polisi hawawezi kukupa ushirikiano
Yes, ni huyo huyo naye mfuatilie kuna masakata ya madawa kulevya kenya mzigo ulishikwa mombasa. Ukakoswa mtu baharini, ila uliondoka na watu, kuna moja ya madalali wa kiroho.
 
Yes, ni huyo huyo naye mfuatilie kuna masakata ya madawa kulevya kenya mzigo ulishikwa mombasa. Ukakoswa mtu baharini, ila uliondoka na watu, kuna moja ya madalali wa kiroho.
Duh ngoja nizitafte. Hivi yule gavana wa kenya aliyemuua gf wake baada ya kupata ujauzito na kukataa kuutoa kesi yake iliishia wapi
 
Mara mia utapeli ila sio ujambazi wa kutumia siraha.

Ukitapeliwa sometimes ukikumbuka ulivotapeliwa unaweza ishia kucheka kwa ujuha ulioufanya ila ujambazi utalilia kiungo chako.
Walishawahi kumtapeli Mama yangu mzazi (Mwalimu) alikuwa kaenda kutoa pesa benki tarehe zao zile za mishahara, akakutana na wajanja wa mjini wakamdaka wakiwa wamepaki noa nyeusi pembeni kidogo eneo la NMB.

Wakamdanganya kuwa ni wafanyabiashara wa madini na wanakopesha pesa hadi zaidi ya M 50, lakini sharti la kuingia kwenye huo mfuko lazima uweke kianzio cha M 1.

Mama aliwaamini na kuwaahidi wamsubiri akatoe pesa benki kwanza ndipo arudi ajiunge na huo mfuko, cha ajabu walipopewa tu M 1 walimwambia ajaze fomu na akatoe nakala ili waweze kumwekea M50 kwenye akaunti yake, alipowaacha kidogo tu kwenda steshenari iliyopo karibu na benki kutoa nakala ndipo hapo hapo Jamaa walimwacha njia panda wakiondoa gari kwa kasi mno na hawakupatikana hata kwenye mawasiliano ingawa kabla hawajaondoka aliwapigia walikuwa tu hewani.
 
Walishawahi kumtapeli Mama yangu mzazi (Mwalimu) alikuwa kaenda kutoa pesa benki tarehe zao zile za mishahara, akakutana na wajanja wa mjini wakamdaka wakiwa wamepaki noa nyeusi pembeni kidogo eneo la NMB.

Wakamdanganya kuwa ni wafanyabiashara wa madini na wanapesha pesa hadi zaidi ya M 50, lakini sharti la kuingia kwenye huo mfuko lazima uweke kianzio cha M 1.

Mama aliwaamini na kuwaahidi wamsubiri akatoe pesa benki kwanza ndipo arudi ajiunge na huo mfuko kisha, cha ajabu walipopewa tu M 1 walimwambia ajaze fomu na akatoe nakala ili waweze kumweke M50 kwenye akaunti yake, alipowaacha kidogo tu kwenda steshenari iliyopo karibu na benki kutoa nakala ndipo hapo hapo Jamaa walimwacha njia panda wakiondoa gari kwa kasi mno na hawakupatikana hata kwenye mawasiliano ingawa kabla hawajaondoka aliwapigia walikuwa tu hewani.
Kuna madawa wanatumia unapigwa njunje kwa sekunde. Ila pia mama kwa hiyo scenario aliuzwa huwa wanaenda sehemu ya uhakika. Hata mimi bi.mkubwa aliwahi kupigwa kwa namna hiyo sema style tofauti.

Na kuna picha za hao majamaa aiseehh ukiwacheki huwezi kuamini sema nao wana chain ndefu.
 
Back
Top Bottom