Matapeli wa kimapenzi mtandaoni kutoka west Afrika


Wazungu wametuibia sana, acha vijana wa kiafrika watumie taaluma zao kurejesha utajiri wetu nyumbani.
 
Sema kibongobongo hawajawekeza sana.
Wanapiga hela ndogondogo sijaskia ishu kubwa za kitapeli, au zipo mimi ndo sijui??
Zipo nyingi zinaendeshwa chini ya maji. Ukikomaa sana mnagawana nusu hasara. Unapita hivi.

Sasa wazee wa Goodmorning unawashtaki wapi ? Huku lazimishwa wewe mwenyewe umejaa upepo.
 
Sisi vijana wetu wanacheza chini bado wako kwenye style ya "ile pesa tuma kwenye namba hii"
Kuna lipumbavu limoja hapa limetoka kunipigia simu si muda mrefu kwa no ngeni likijitambulisha kuwa mi ni flani toka Airtel, karibu mteja niweze kukusikiliza na kukusaidia shida yako yoyote, nikalijibu "sihitaji huduma zenu zozote toka Airtel" likastuka na kukata simu ghafla [emoji12]
 
Siku akidakwa na yeye anaunganishwa kwenye tukio...ndo atajua hajui
Washalala wote ndani enzi hawajaona. Pesa kitu kingine.
Kuna mdada rafiki yangu kaolewa na jamaa flani, aliniambia wakati wana date alikuwa anahisi jamaa anauza unga maana alikuwa anatembea na mabahasha ya eka halafu anakutana na watu anawapatia au anapokea bahasha au mabegi ya pesa.
Sasa nikamuuliza kwanini hukuachana naye?
Jibu akawa hana ila bila shaka ni pesa ilikuwa inamchanganya.
 
Hata hapa TZ kuna mambo mengi na mauaji na kesi kama ingekuwa inaruhusiwa ma investigative journalists wafanye yao tungebaki kushangaa.
"Mohammed Ali: Jicho pevu" alikuwa anakuja vizuri sana, mwisho wa siku akaingia kwenye siasa/ kazi na kofia mbili.

Jerry Muro kile kipindi chake, si uliona kilivyomletea kelele.
 
Matapeli ni watu smart sana sana. Yani anakufanya unatoa pesa mwenyewe bila kushikiwa bunduki baadae unakuja jiona mjinga na signs zote zilikuwa wazi lakini hukushtuka.
Hiki ndo kinanishangaza sana [emoji848]
 
Huyu ni nomaz..

Kule insta kwenye page yake kumejaa maneno ya busara na hekima, motivation speaker fulani, ana ofisi eti kali (picha plus video) anakushauri jinsi ya kucontrol your money[emoji1787][emoji1787]

Jamaa amejipanga si kitoto asee
Siku hizi watu wanakutapeli unafahamiana nao kabisa,binadam wamebadilika jamani
 
"Mohammed Ali: Jicho pevu" alikuwa anakuja vizuri sana, mwisho wa siku akaingia kwenye siasa/ kazi na kofia mbili.

Jerry Muro kile kipindi chake, si uliona kilivyomletea kelele.
Hivi huyu mohamed Ally ndiye alitengeneza na ile ya west gate kuonyesha wavamizi waliondoka muda tu askari wako tu wanaiha biscuit ndani?
Tz ngumu maana hata polisi hawawezi kukupa ushirikiano
 
Kipindi kinaonyeshwa wapi?
 
Hivi huyu mohamed Ally ndiye alitengeneza na ile ya west gate kuonyesha wavamizi waliondoka muda tu askari wako tu wanaiha biscuit ndani?
Tz ngumu maana hata polisi hawawezi kukupa ushirikiano
Yes, ni huyo huyo naye mfuatilie kuna masakata ya madawa kulevya kenya mzigo ulishikwa mombasa. Ukakoswa mtu baharini, ila uliondoka na watu, kuna moja ya madalali wa kiroho.
 
Yes, ni huyo huyo naye mfuatilie kuna masakata ya madawa kulevya kenya mzigo ulishikwa mombasa. Ukakoswa mtu baharini, ila uliondoka na watu, kuna moja ya madalali wa kiroho.
Duh ngoja nizitafte. Hivi yule gavana wa kenya aliyemuua gf wake baada ya kupata ujauzito na kukataa kuutoa kesi yake iliishia wapi
 
Mara mia utapeli ila sio ujambazi wa kutumia siraha.

Ukitapeliwa sometimes ukikumbuka ulivotapeliwa unaweza ishia kucheka kwa ujuha ulioufanya ila ujambazi utalilia kiungo chako.
Walishawahi kumtapeli Mama yangu mzazi (Mwalimu) alikuwa kaenda kutoa pesa benki tarehe zao zile za mishahara, akakutana na wajanja wa mjini wakamdaka wakiwa wamepaki noa nyeusi pembeni kidogo eneo la NMB.

Wakamdanganya kuwa ni wafanyabiashara wa madini na wanakopesha pesa hadi zaidi ya M 50, lakini sharti la kuingia kwenye huo mfuko lazima uweke kianzio cha M 1.

Mama aliwaamini na kuwaahidi wamsubiri akatoe pesa benki kwanza ndipo arudi ajiunge na huo mfuko, cha ajabu walipopewa tu M 1 walimwambia ajaze fomu na akatoe nakala ili waweze kumwekea M50 kwenye akaunti yake, alipowaacha kidogo tu kwenda steshenari iliyopo karibu na benki kutoa nakala ndipo hapo hapo Jamaa walimwacha njia panda wakiondoa gari kwa kasi mno na hawakupatikana hata kwenye mawasiliano ingawa kabla hawajaondoka aliwapigia walikuwa tu hewani.
 
Kuna madawa wanatumia unapigwa njunje kwa sekunde. Ila pia mama kwa hiyo scenario aliuzwa huwa wanaenda sehemu ya uhakika. Hata mimi bi.mkubwa aliwahi kupigwa kwa namna hiyo sema style tofauti.

Na kuna picha za hao majamaa aiseehh ukiwacheki huwezi kuamini sema nao wana chain ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…