Matatizo ya kiakili ndiyo yanayokufanya ukanushe uwepo wa Muumba

Hapana, Allah sio Jesus. Na tambua kuwa neno "ALLAH" ni kwalugha ya kiarabu tu ila kiswahili ni Mungu. Kama unavyosema jesus/yesu.Huo ni mtazamo wako sidhani kama muuliza swali alikua na wazo hilo.
Mi nimemjibu naamini amenielewa.
So allah/mungu ni yesu?
 
Kwahiyo unakiri waamini mungu hurogeka?? Why mungu asizuie nyie kurogwa ili kuwaepusha na madhara ya kurogwa?
Hata wewe unapenda familia yako (mke na watoto wako) wafuate misingi mizuri ambayo umewaekea. Hutarajii mwanao akupinge au aharibikiwe.
Lakin katika maisha hayo yote yanatokea na sometimes unamuadhibu mwanao kwakumchapa...! Kwanini unamuadhibu mwanao anapokosea?
 
Mfano mwingine ambao inaonyesha uwezo wa mungu ni kwamba kuna wadudu wadogo ambao matakoni mwao wakiruka hua wanawasha tea.Kwa waliowahi kuishi vijijini watakua wanawafahamu hawa wadudu,sasa jiulize taa inawakaje wakati hawana Betri,waya wala glopu matakoni?
Mkuu nawajua sana tulikuwa tunawaita mnyange
 
Siwezi Kuandika mengi hapa, ila nimekaa masaa matano najaribu kuilazimisha akili
yangu ipinge uwepo wa Muumba, akili imekataa kabisa. Haya ndiyo yaliyonifanya
nikiri kuwepo kwa MUUMBA wa kila kitu.

1. Nilianza kwa kuwatazama kuku ambao walikuwa mbele yangu. Hao wakanisafirisha
Kilomita kadhaa za fikra huku nikikusanya ndege Tofauti tofauti kichwani mwangu.
niliangalia Rangi na Tabia zao, lakini kilichonivutia zaidi ni Rani zao.
View attachment 798044
Hivi akili yenye utambuzi, akili iliyo salama inashindwa vipi kuona maajabu yaliyopo katika
Rangi za kuku? Tunafahamu kuanzia yai linavyokuwa mpaka kifaranga ambacho huzaliwa
Bila nakshi zozote? Ni upungufu tu wa akili ndio unaotufanya tusione kama huyo Kuku
na ndege wengine nitakaowaweka Hapa Rangi zao hazijaja kwa bahati, Ni wazi kuwa
hata hizo Rangi zimewekwa kwa Mpangilio, Ewe mpingaji wa Muumba huoni?
View attachment 798064
Upofu gani umekupata hata usione umaridadi, utaalamu tena wa kiwango cha juu
ambao umetumika kumpamba na Kumnakshi Ndege huyu? ni Upumbavu kusema
Huyu ndege amatokana na Bigbang sijui kitu gani... huko.

2. Wanyama, nilitafakari maumbile na Rangi za wanyama niagundua wazi kuwa
kukataa uwepo wa muumbaji ni dalili Kubwa ya Ukosefu wa akili.View attachment 798066

3.Wadudu
View attachment 798067
Hata wadudu wameshindwa kuifanya akili yako itambue Uwepo wa Muumba?

4.MIMEA
View attachment 798068
SHAABAAAAASH! AMETAKASIKA MOLA WANGU MBORA WA UUMBAJI
Kama unashindwa kuona maajabu ya mpangilio wa Rangi katika hili ua na
akili yako ikatambua kuwa Kuna MUUMBA Jihesabu wewe ni mwendawazimu.

AKILI SALAMA NI ILE INAYOTAFAKARI MAMBO, Usije kuwa na videgree vyako viwili mpaka
Vinne ukashindwa kutafakari mambo mepesi kama haya ukajiona mjanja, utakuwa ni mpumbavu tu ambaye umekariri mambo ambayo wametafakari wenzio.
Mimi kifo tu ndio kinanifanya naamini kuna Mungu
 
Unafahamu "logical non sequitur" ni nini?
Unaifahamu Grandiose Delusion?
Je unafahamu uhusiano kati ya Grandiose Delusion na Schizophrenia au Bipolar Disorder?

Mleta mada yupo sahihi.Upagani ni wazimu.
 
Hapana, Allah sio Jesus. Na tambua kuwa neno "ALLAH" ni kwalugha ya kiarabu tu ila kiswahili ni Mungu. Kama unavyosema jesus/yesu.Huo ni mtazamo wako sidhani kama muuliza swali alikua na wazo hilo.
Mi nimemjibu naamini amenielewa.
Kaka ngoja nikupe faida ya kiligha kidogo. Tamko "Allah" ni tamko la kiarabu lenye maana ya "Mwenye kuabudiwa" ,tamko hili kiasili halina wingi,Allah sio Mungu,sababu tamko Mungu lina wingi. Kutokana na hali hiyo,katika dini ya kiislamu kuna somo linaitwa AQIDA kwa kiswahili tunasema ITIKADI,hili ni somo maalumu kwalo linaelezea sifa Mola wetu muumba kama alivyojielezea yeye na vile alivyoelezewa na mtume wake Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.

Katika somo hili kuna vitu vikuu vitatu ambavyo mja anatakiwa kujifunza na kuvifanyia kazi kwa ukamilifu.Navyo ni

1. Kumpwekesha Allah katika ibada,yaani hakuna anaye paswa kuabudiwa kwa haki ila yeye pekee.

2. Kumpwekesha Allah katika uumbaji,yaani yeye ndio muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

3. Kumpwekesha yeye katika majina yake na sifa zake. Yaani lazima ujue ya kuwa Allah hafanani na kiumbe yeyote na sifa zake ni kamilifu,kadhalika lazima ujue ya kuwa majina yake yanaelezewa au kutafsiriwa kama yeye alivyoyatafsiri kupitia mtume wake.
 
kwanni Mungu amuache mwanaadamu amsemee wakati "" alisema kuwa nikiumbe dhaifu"....aoni kuwa udhaifu walionao kisha akawapa nafasi ya kumsemea itakuwa ni sababu ya mkanganyiko mkubwa mno baina ya wao kwa wao ""..je tukisema kuwa atakuwa anawaonea watu " atakao kuja kuwachoma moto tutakuwa tuna kosea "".... Maana kuna wengine hujikuta wanatenda dhambi kwa sbbu ya hizo contradiction zilizopo "",....
Kwanza Tukubaliane Muumba yupo au hayupo?
 
Baada ya kukosa majibu ya hao ndege na baadhi ya wanyama ndio ukafikia tamati kuwa kuna Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo, mjuzi wa yote na asiyekuwa na mwanzo wala mwisho sio?

Vipi huyo unaemdhania akaja mbele yako na akili zake na maajabu yake huoni lazima umhoji kaumbwa na nani? Nasema hivi kwa sababu haiwezekani mwenye akili kuliko sisi na wa utata kuliko sisi na viumbe vyote awepo tu pasiwe na aliempa hizo akili.
Kama umeweza kuyatazama mazingira ukayaona ya ajabu na ya utata hadi kufikia kuhalalisha kwamba lazima mazingira hayo yawe na muumbaji wake, kwanini basi tusiulize aliyemuumba huyo Mungu kwa kuwa ni wa utata kuliko mazingira yenyewe?

Mwanadamu mwenye akili timamu hawezi kusema Mungu wa namna hiyo yupo,
Bado tungali tunautafuta ukweli wa chanzo chetu na ulimwengu kwa ujumla.
Wale wanaohitimisha kwa kasema "tunalo tegemeo/ambalo ni dhana ya Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo na anaetujua na kutujali" hao ndio wanaotusababishia kuchelewa kuufikia ukweli Kamil, uhuru kamili na ukamilifu wa 100%

Asilimia 99 ya watu waliopata kuishi kwenye Dunia hii na waliomo kwa sasa, wamefikia kumuumba Mungu kwwnye akili zao baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu.

Walimuumba Mungu na bado wangali wakendelea kumuumba karne na karne kwenye akili zao.
Ndio! Wameumba tegemeo kivuli. Tena wamelifanya tegemeo hilo kuwa sheria.
Wamekuwa vutuko kwa kuzipack akili zao pembeni huku wakilitegemea tegemeo kivuli

Laiti wanadamu wangelitambua na kuondoa huu uchafu ndani ya uzima wao, basi Dunia ungekuwa mahali salama sana pa kuishi.

HAPO MWANZO PALIKUWEPO NA KISTULI, NACHO KISTULI KILIKUWAPO KWA KISTULI,,,, NACHO KISTULI KULIKUWA KISTULI.
 
Sawa umetafakari vizuri, muumba wa vyote yupo, kama maisha yapo baada ya kifo, tutamfikia kwa kutumia imani gani? Ukristu kuna mgawanyiko mkubwa na islamu kuna aina mbili, nishauri nitumie imani gani? Lakini uliposema wasioamini wana upeo mdogo, akina Karl Max walikua na upeo mdogo? Naona wanaotumia reason zaidi kuliko faith wana upeo mpana zaidi.
Kaka umeuliza swali zuri sana. Mimi sababu ni muislamu najaribu kujikita zaidi katika imani,sababu ni makosa na ni haramu kuzungumza jamno usilolijua.

Kwa nataka nijue uliposema "....na islamu kuna aina mbili" ulimaanisha nini ?

Sio kweli wenye kutumia uhojaji ndio wana upeo mkubwa zaidi. Kwanini nasema sio kweli ? Tofauti yetu na wao ni kuwa wao walikosa msingi kwahiyo ingewafikisha katika ule ukweli mkuu,kaka huwezi kutegemea kitu kisicho kamili kupata ukamilifu. Akili ya binadamu haijakamilika na hii ndio sababu kubwa iliyowafanya wale wajiitao "WAFIKIRIAJI WAKUU" wapotoke.

Wafikiriaji wakuu hawakuwa na mipaka katika kufikiria kwao ndio maana walikuwa wanakosea kosea sana. Pia watu hawa walikuwa na wasi wasi wa shetani,yaani shetani wa kijini alikuwa anawatia wasi katika akili zao.

Akili iliyo salama yaani ile ambayo haijaingiliwa na fikra chafu na potofu huwa ni nyepesi kuujua ukweli pindi ikipata misingi au njia itakayo ifikisha katika lengo.
 
Sawa umetafakari vizuri, muumba wa vyote yupo, kama maisha yapo baada ya kifo, tutamfikia kwa kutumia imani gani? Ukristu kuna mgawanyiko mkubwa na islamu kuna aina mbili, nishauri nitumie imani gani? Lakini uliposema wasioamini wana upeo mdogo, akina Karl Max walikua na upeo mdogo? Naona wanaotumia reason zaidi kuliko faith wana upeo mpana zaidi.
Swala la Imani ipi hilo ni jingine, kwanza ilikuwa kuthibitisha hakuna kilichojitokeza
Chenyewe..... Baada ya hapo kaa chini usome ikiwezekana zipitie dini zote kwa
umakini, UKWELI UTAUJUA.
 
Kaka ngoja nikupe faida ya kiligha kidogo. Tamko "Allah" ni tamko la kiarabu lenye maana ya "Mwenye kuabudiwa" ,tamko hili kiasili halina wingi,Allah sio Mungu,sababu tamko Mungu lina wingi. Kutokana na hali hiyo,katika dini ya kiislamu kuna somo linaitwa AQIDA kwa kiswahili tunasema ITIKADI,hili ni somo maalumu kwalo linaelezea sifa Mola wetu muumba kama alivyojielezea yeye na vile alivyoelezewa na mtume wake Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.

Katika somo hili kuna vitu vikuu vitatu ambavyo mja anatakiwa kujifunza na kuvifanyia kazi kwa ukamilifu.Navyo ni

1. Kumpwekesha Allah katika ibada,yaani hakuna anaye paswa kuabudiwa kwa haki ila yeye pekee.

2. Kumpwekesha Allah katika uumbaji,yaani yeye ndio muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

3. Kumpwekesha yeye katika majina yake na sifa zake. Yaani lazima ujue ya kuwa Allah hafanani na kiumbe yeyote na sifa zake ni kamilifu,kadhalika lazima ujue ya kuwa majina yake yanaelezewa au kutafsiriwa kama yeye alivyoyatafsiri kupitia mtume wake.
Ahsante kwa elimu nzuri.. Nimeelewa vizuri sana.
Lkn hapo kwenye Allah sio Mungu kwahoja ya kwamba neno Mungu lina wingi!? Hapana, hapo sijaelewa. Kwani nikweli neno Mungu lina wingi? Sio kama ni waswahili tu ndio wanalazimisha?

Anyway! Kwahiyo kwenye maombi lazima tutumie lugha ya kiarabu? Au tukitumia lugha nyengine kwenye neno Mungu lazima tutamke Allah!?
Mfano:
"ewe Mungu naomba nisaidie" natakiwa niseme "ewe Allah naomba nisaidie"!!
Hapo ni kwakiswahili Kama nikitumia kizigua,kichaga,kihehe na nk itakua hivyo hivyo?
Maana Mungu (Allah) naamini anaelewa na kukubali maombi kwa lugha yoyote
 
Baada ya kukosa majibu ya hao ndege na baadhi ya wanyama ndio ukafikia tamati kuwa kuna Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo, mjuzi wa yote na asiyekuwa na mwanzo wala mwisho sio?

Vipi huyo unaemdhania akaja mbele yako na akili zake na maajabu yake huoni lazima umhoji kaumbwa na nani? Nasema hivi kwa sababu haiwezekani mwenye akili kuliko sisi na wa utata kuliko sisi na viumbe vyote awepo tu pasiwe na aliempa hizo akili.
Kama umeweza kuyatazama mazingira ukayaona ya ajabu na ya utata hadi kufikia kuhalalisha kwamba lazima mazingira hayo yawe na muumbaji wake, kwanini basi tusiulize aliyemuumba huyo Mungu kwa kuwa ni wa utata kuliko mazingira yenyewe?

Mwanadamu mwenye akili timamu hawezi kusema Mungu wa namna hiyo yupo,
Bado tungali tunautafuta ukweli wa chanzo chetu na ulimwengu kwa ujumla.
Wale wanaohitimisha kwa kasema "tunalo tegemeo/ambalo ni dhana ya Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo na anaetujua na kutujali" hao ndio wanaotusababishia kuchelewa kuufikia ukweli Kamil, uhuru kamili na ukamilifu wa 100%

Asilimia 99 ya watu waliopata kuishi kwenye Dunia hii na waliomo kwa sasa, wamefikia kumuumba Mungu kwwnye akili zao baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu.

Walimuumba Mungu na bado wangali wakendelea kumuumba karne na karne kwenye akili zao.
Ndio! Wameumba tegemeo kivuli. Tena wamelifanya tegemeo hilo kuwa sheria.
Wamekuwa vutuko kwa kuzipack akili zao pembeni huku wakilitegemea tegemeo kivuli

Laiti wanadamu wangelitambua na kuondoa huu uchafu ndani ya uzima wao, basi Dunia ungekuwa mahali salama sana pa kuishi.

HAPO MWANZO PALIKUWEPO NA KISTULI, NACHO KISTULI KILIKUWAPO KWA KISTULI,,,, NACHO KISTULI KULIKUWA KISTULI.
Kaka napinga hoja yako kwa asilimia zaidi ya mia moja. Kaka kiasili binadamu yeyote binadamu yeyote yule ameumbwa na silika ya kumtafuta Mola wake aliyuumba,hii haikuachwa hivi hivi ndio binadamu akapewa nyenzo madhubuti za kufikia hatua hiyo nazo ni akili,moyo na milango ya fahamu. Hili utalipata kwa wewe mwenyewe kujipa muda na kufikiria kiukweli huku ukijiacha huru juu ya kufikiria kwako.

Pili,si kweli ya kuwa wanadamu baada ya kukosa majibu ndio wakaamua kumuumba yeye. Bali kinyume chake ndio ukweli wenyewe.

Lakini nina swali kwako kabla sijaendelea,je mwanadamu mwenye akili timamu anaweza kumsema Mungu gani yupo ?

Tatizo kubwa la wakana Mungu sio kwamba wana mkana Allah,bali wanamfikiria vibaya Allah sana.

Hata wewe kwa kauli zako na fikra zako unamfikiria Allah katika upande hasi na wala si katika uoande chanya ndio maana unapotoka.
 
Kwanza Tukubaliane Muumba yupo au hayupo?
hakuna Mwenye Uhakika na hilo "" so inabaki kuwa ni coincidence tu "" kukosa kwetu kujibu maswali magumu haiwezi kuwa sabbu ya sisi kukimbilia " kusingizia uwepo wa Mungu ""....
 
Baada ya kukosa majibu ya hao ndege na baadhi ya wanyama ndio ukafikia tamati kuwa kuna Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo, mjuzi wa yote na asiyekuwa na mwanzo wala mwisho sio?

Vipi huyo unaemdhania akaja mbele yako na akili zake na maajabu yake huoni lazima umhoji kaumbwa na nani? Nasema hivi kwa sababu haiwezekani mwenye akili kuliko sisi na wa utata kuliko sisi na viumbe vyote awepo tu pasiwe na aliempa hizo akili.
Kama umeweza kuyatazama mazingira ukayaona ya ajabu na ya utata hadi kufikia kuhalalisha kwamba lazima mazingira hayo yawe na muumbaji wake, kwanini basi tusiulize aliyemuumba huyo Mungu kwa kuwa ni wa utata kuliko mazingira yenyewe?

Mwanadamu mwenye akili timamu hawezi kusema Mungu wa namna hiyo yupo,
Bado tungali tunautafuta ukweli wa chanzo chetu na ulimwengu kwa ujumla.
Wale wanaohitimisha kwa kasema "tunalo tegemeo/ambalo ni dhana ya Mungu muumbaji wa vyote, muweza wa yote, mwenye upendo na anaetujua na kutujali" hao ndio wanaotusababishia kuchelewa kuufikia ukweli Kamil, uhuru kamili na ukamilifu wa 100%

Asilimia 99 ya watu waliopata kuishi kwenye Dunia hii na waliomo kwa sasa, wamefikia kumuumba Mungu kwwnye akili zao baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu.

Walimuumba Mungu na bado wangali wakendelea kumuumba karne na karne kwenye akili zao.
Ndio! Wameumba tegemeo kivuli. Tena wamelifanya tegemeo hilo kuwa sheria.
Wamekuwa vutuko kwa kuzipack akili zao pembeni huku wakilitegemea tegemeo kivuli

Laiti wanadamu wangelitambua na kuondoa huu uchafu ndani ya uzima wao, basi Dunia ungekuwa mahali salama sana pa kuishi.

HAPO MWANZO PALIKUWEPO NA KISTULI, NACHO KISTULI KILIKUWAPO KWA KISTULI,,,, NACHO KISTULI KULIKUWA KISTULI.
Ha hahaha "" HAPO MWANZO
 
Ahsante kwa elimu nzuri.. Nimeelewa vizuri sana.
Lkn hapo kwenye Allah sio Mungu kwahoja ya kwamba neno Mungu lina wingi!? Hapana, hapo sijaelewa. Kwani nikweli neno Mungu lina wingi? Sio kama ni waswahili tu ndio wanalazimisha?

Anyway! Kwahiyo kwenye maombi lazima tutumie lugha ya kiarabu? Au tukitumia lugha nyengine kwenye neno Mungu lazima tutamke Allah!?
Mfano:
"ewe Mungu naomba nisaidie" natakiwa niseme "ewe Allah naomba nisaidie"!!
Hapo ni kwakiswahili Kama nikitumia kizigua,kichaga,kihehe na nk itakua hivyo hivyo?
Maana Mungu (Allah) naamini anaelewa na kukubali maombi kwa lugha yoyote
Mola wetu anazisikia lugha zote sababu yeye ndio ameumba kugha,hizo ika nachotakiwa ni kuweka majina yake badala ya jina la Mungu. Na yeye ana majina zaidi ya 100 na amesema tumuombe kwayo na yeye amesema ana majina mazuri.

Kaka naendelea kukupa faida,mathalani katika ibada yaani sala tunazo sali sisi waislamu,yaani sala 5 pale hutumika lugha moja tu ya kiarabu,sababu katika sala kuna masharti na kuna nguzo za sala.

Hapa ndio utakapo ona ya kuwa kuna umuhimu wa kila muislamu kuijua dini yake.

Nje ya sal zile tano tumia lugha utakayo tumia wew utakayo yeye anaisikia ila katika majina yake ndio unatakiwa kutumia yale aliyojiita yeye na aliyoitea na mtume wake amani ya Allah iwe juu yake.
 
Dah! Umenifanya nitafakari upya, hakika hivyo vitu havipo kwa bahati mbaya.... Natangaza Rasmi kuhama kwenye kundi lile kweli kabisa ndugu yangu maana nilishaanza kupotoka hasa baada ya kuona Post za baadhi ya wachangiaji wakimtukana Mungu waziwazi na hakuna linalowakuta, basi itakuwa anawasubiri tu.
Anawalia timing
 
Mola wetu anazisikia lugha zote sababu yeye ndio ameumba kugha,hizo ika nachotakiwa ni kuweka majina yake badala ya jina la Mungu. Na yeye ana majina zaidi ya 100 na amesema tumuombe kwayo na yeye amesema ana majina mazuri.

Kaka naendelea kukupa faida,mathalani katika ibada yaani sala tunazo sali sisi waislamu,yaani sala 5 pale hutumika lugha moja tu ya kiarabu,sababu katika sala kuna masharti na kuna nguzo za sala.

Hapa ndio utakapo ona ya kuwa kuna umuhimu wa kila muislamu kuijua dini yake.

Nje ya sal zile tano tumia lugha utakayo tumia wew utakayo yeye anaisikia ila katika majina yake ndio unatakiwa kutumia yale aliyojiita yeye na aliyoitea na mtume wake amani ya Allah iwe juu yake.
Noted!
 
Back
Top Bottom