Matatizo ya nchi hii chanzo ni ndugu Nyerere

Ebu tulia basi mke wa rem
Matusi, kutoelewa lugha ya picha vinadhihirisha hicho kichwa unatumia kuhifadhi makamasi tu. Endelea kuwalaumu Nyerere na mababu zako kwa ujinga wako. I rest my case.
y! Wewe unapoita wenzio wajinga unaona upo sawa?
 
Adui namba moja wa Tanzania ni NYERERE. Nyerere hakutaka kuachia madaraka lakini alipohidi kuwa anataka kupinduliwa akaachia ili kulinda heshima yake.

Adui namba moja wa taifa hili ni J. K. Nyerere.

Cc Monetary doctor
Hamjajibu hata hoja moja. Viwanda alivyojenga Nyerere zaidi ya 400 mlivipeleka wapi.

Mji wa Guangzhou China wenye viwanda maelfu umejengwa kwa miaka 10 tu. Lakini tangu Nyerere afariki imepita miaka 26, mmejenga nini kwa muda huo. Hata madarasa na vyoo vya shule mnatembeza bakuli.

Madini, mbuga, bandari, gesi ambavyo Nyerere hakuuza ,, ninyi mmeuza,, pesa mmepeleka wapi.
 
Adui namba moja wa Tanzania ni NYERERE. Nyerere hakutaka kuachia madaraka lakini alipohidi kuwa anataka kupinduliwa akaachia ili kulinda heshima yake.

Adui namba moja wa taifa hili ni J. K. Nyerere.

Cc Monetary doctor
Nyerere kajenga msingi wa umoja na amani, vitu ambavyo vimeweza kuifanya familia unayotoka wewe ikakulea mpaka ukaweza kuandika hayo maandishi yako ukiwa huna presha yoyote ya kulipuliwa mabomu au kupigwa risasi.

Nyerere alipewa shahada za heshima na vyuo vikuu zaidi ya 40 dunia nzima enzi za uhai wake, hao wote ni wajinga kiasi cha kumpa heshima lakini wewe na wote wenye mawazo ya aina yako ndio wenye akili timamu!!.
 
Watoto wa 2000 hawa, wamepata akili na kuanza kujitegemea wamekutana na maisha magumu wanatafuta nani wa kumtwisha mzigo wa lawama.

Nyerere kaondoka 1985 wamekuja marais wanne na kuondoka, hao wote kaacha kuwalaumu kakimbilia kwa rais ambaye pengine wakati akiwa ikulu mama yake mzazi alikuwa hamjazaa bado!.
 
Wakati jaribio la mapinduzi lilipotokea nahisi ulikuwa embryo ama wazazi wako hakuzaliwa kabisa. Hapa Tanzania hata usome Vipi huwezi ukafundishwa jinsi Nyerere alivyokuwa mtu mbaya, pia huwezi kusikia kama alikuwa hapendwi na baadhi ya watu hapa Tanzania.

Kua uyaone maisha 😎.
 
Tumekuwa na Marais huyu wa 5 baada ya Mwl.Nyerere,Udhaifu wake ulikosa Akili za wa
 
Barikiwa. Tangu uhuru mpaka leo tuna miaka 64. Nyerere alitawala miaka 24 tu kati ya hiyo 64. Ndani ya miaka yake 24 wote walisoma na kutibiwa bure, ajira za kumwaga na kuchagua.

Tueleze Miaka 40 ambayo Nyerere hakuwepo na hayupo, mmefanya nini zaidi ya kujisifia kuuwa watu, kuteka kuchinja na kufunga.
 
Founder wa haya yote yanayofanyika Leo hii ni Nyerere.
Uwoga wa watanzania umetengenezwa na Nyerere, uonevu unaotokea aliusuka Nyerere, umalaya unaotokea umeasisiwa na Nyerere, umasikini ambao umetamalaki umeasisiwa na bwana Nyerere.

Nyerere hafai kuigwa na jamii.
 
Amani inayobatana na hofu na umasikini ni umalaya umalaya tu.
Hata hivyo vyuo vilivyompa Nyerere shahada ya heshima vingi ni vya nje ya Afrika na walimpa Ili kutupumbaza kiakili na unafiki kama kuna vyuo vya ndani vilivyompa hiyo heshima basi walimpa kwa sababu nao ni wajinga kama wajinga wengine.

Kwa nini shuleni wanafundisha mazuri tu ya Nyerere kwa nini upande wa mabaya aliyoyatebda haufundushwi?

Nyerere ni tapeli mkubwa sana kupata kutokea hapa nchini.
 
UKujibu hoja na maswali japo moja tu nitaendelea kukuelimisha. Tofauti na hapo utakuwa na tatizo kichwani na unapaswa kupuuzwa.

1. Viwanda alivyojenga Nyerere mlivipeleka wapi.

2. Maliasili zote mbuga za wanyama, gesi, nk mapesa yake mmefanyia nini.

3. Miaka 40 baada ya Nyerere kuondoka nani amewazuia kufanya mnavyotaka. ?
 
Chizi
Wewe,ukoo wako na familia mpumbavu mkubwa nenda kajiuze vizuri huko
Sasa nimekaa vizuri hapa, mkuu 'Makonde plateau', kwa ajili yako; tuuendeleze vizuri mjadala wako huu. Niambie, tuanzie wapi, huko kwa "kujiuza, au kwenye uumbavu", sema nio tayari kabisa kwa ajili yako, siku nzima ukipenda.!
 
Yeye angekuwa kiongozi mzuri aliyeunda misingi mizuri hivyo viwanda visingetokomea na Mali asili pia zisingetumika vibaya pia.

Mbona aliijengea CCM misingi mizuri kwa nini kwenye uongozi wa nchi ameshindwa?

Halafu mbona hamtuambii mabaya ya Nyerere ama Nyerere ni malaika?
Tunapofanya tathmini lazima tuangalie pande zote mbili.
 
Ni muda mrefu tangu Nyerere afariki. Tumeshindwaje kurekebisha hayo ''matatizo'' yake? Mbona tunazidi kurudi nyuma? Matatizo ya Tanzania yanatokana na raia wake kuwa ni watu wa kulaumu na kulalamika tu bila kuchukuwa action. Hakuna nchi inayoweza kupata mabadiliko kwa watu kulalamika na kulaumu. Mafanikio ya Nyerere yanapimwa kwa kulinganisha nchi nyingine za Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara na nchi yetu. Je, zina hali bora kuliko sisi? Kipindi cha Nyerere je?
 
Nyerere alikufa aliacha Chuo Cha TANESCO Morogoro Mali ya serikali.
Sasa mali ya waislam, kinaitwa chuo kikuu Cha Waislam.
Kweli Nyerere alikuwa mdini..
 
Nyinyi mnamsifi sisi tunasema yeye ndiye chanzo Cha matatizo.
Ukiharibu msingi basi jengo lote huanguka.
 
Jibu maswali kwanza. Wapi mlipopeleka viwanda.

Miaka 40 ya peke yenu bila Nyerere hata sasa mnakwama wapi.

Hayo ya mabaya na mazuri hayasaidii.

Wewe una mazuri gani na mabaya gani,, tueleze.
 
Kusema kuwa hakujenga misingi mizuri ya viwanda na maliasili ni kutojua historia ya Tanzania. Mambo mengi yaliharibika baada ya yeye kuondoka. Hivi ukiachiwa urithi wa nyumba na baba yako halafu ukauza ile nyumba utasema kosa ni la baba?
Kuhusu eti hatuambiwi mabaya ya Nyerere nako ni uongo. Nyerere ana mabaya na wengi wamekuwa wanayasema. Kwa mfano ''kutikisa'' mfumo wa elimu yetu umefanya watanzania wengi kuwa vilaza na hali imekuwa mabaya zaidi sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…