Matengenezo ya bomba kuu kupunguza maji kwa siku nne Dar es Salaam na Pwani

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
‎Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na upungufu wa huduma ya maji kwa siku nne kuanzia Novemba 3 hadi 6, 2026, wakati Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ikifanya matengenezo ya bomba kuu lenye kipenyo cha inchi 72 linalopokea maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini.
‎
IMG-20261102-WA0003.jpg

‎Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi Everlasting Lyaro imesema matengenezo hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha miundombinu yake ya majisafi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño.
‎
‎Kutokana na kazi hiyo, uzalishaji wa maji katika mtambo huo utapungua kwa asilimia 60 kwa kipindi cha saa 96, hali inayotarajiwa kuathiri upatikanaji wa huduma kwa wakazi wanaohudumiwa kupitia chanzo hicho.
‎
IMG-20261102-WA0002.jpg

‎Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Zinga, Kiromo, Dunda, Kisutu, Magomeni, Nianjema, Fukayosi, Makurunge, Kerege, Mapinga, Mbweni, Mabopwepande, Bunju, Kunduchi, Kawe, Mbezi Juu, Goba, Wazo, Makongo, Kijitonyama, Kinondoni, Makumbusho, Msasani, Mzimuni, Tandale, Ndugumbi, Kigogo, Magomeni, Kariakoo, Mchikichini, Upanga Magharibi, Gerezani, Upanga Mashariki, Kisutu, Mchafukoge, Jangwani, Kivukoni, Ilala, Mnyamani, Liwiti, Kilungule, Kilakala, Mianzini, Keko, Kurasini, Miburani na Chang'ombe.
‎
‎DAWASA imewaomba wateja na wananchi katika maeneo hayo kuvumilia usumbufu utakaoweza kujitokeza wakati wa matengenezo hayo, huku ikiwahimiza kupanga matumizi ya maji na kuhifadhi kiasi cha kutosha kwa matumizi muhimu kabla ya kazi kuanza.
‎
‎DAWASA imewaomba wakazi hao kuhifadhi Maji ya kutosha wakati kazi ya matengenezo itakapofanyika.
‎
 
Gridi ya Taifa ya maji iliishia wapi?
‎Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na upungufu wa huduma ya maji kwa siku nne kuanzia Novemba 3 hadi 6, 2026, wakati Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ikifanya matengenezo ya bomba kuu lenye kipenyo cha inchi 72 linalopokea maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini.
‎View attachment 3703122
‎Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi Everlasting Lyaro imesema matengenezo hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha miundombinu yake ya majisafi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño.
‎
‎Kutokana na kazi hiyo, uzalishaji wa maji katika mtambo huo utapungua kwa asilimia 60 kwa kipindi cha saa 96, hali inayotarajiwa kuathiri upatikanaji wa huduma kwa wakazi wanaohudumiwa kupitia chanzo hicho.
‎View attachment 3703123
‎Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Zinga, Kiromo, Dunda, Kisutu, Magomeni, Nianjema, Fukayosi, Makurunge, Kerege, Mapinga, Mbweni, Mabopwepande, Bunju, Kunduchi, Kawe, Mbezi Juu, Goba, Wazo, Makongo, Kijitonyama, Kinondoni, Makumbusho, Msasani, Mzimuni, Tandale, Ndugumbi, Kigogo, Magomeni, Kariakoo, Mchikichini, Upanga Magharibi, Gerezani, Upanga Mashariki, Kisutu, Mchafukoge, Jangwani, Kivukoni, Ilala, Mnyamani, Liwiti, Kilungule, Kilakala, Mianzini, Keko, Kurasini, Miburani na Chang'ombe.
‎
‎DAWASA imewaomba wateja na wananchi katika maeneo hayo kuvumilia usumbufu utakaoweza kujitokeza wakati wa matengenezo hayo, huku ikiwahimiza kupanga matumizi ya maji na kuhifadhi kiasi cha kutosha kwa matumizi muhimu kabla ya kazi kuanza.
‎
‎DAWASA imewaomba wakazi hao kuhifadhi Maji ya kutosha wakati kazi ya matengenezo itakapofanyika.
‎
Kumbe.kuna maji ya DAWASA
 
Kama TTCL nao wao wangebaki wenyewe bila kuruhu mashirika binafs kufanya kazi. Nakuahakikishia kuna siku wangetangaza ukosekanaji wa huduma ya mtandao kwa 2 au zaidi kwaajili ya maboresho ya mtandao.

Kifupi mashirika yenye mkono wa serikali ngumu sana kutoa huduma kikamilifu. Maana mikoni ya wengi ipo inayojiwazia wenyewe, Uzembe na kujua kuwa hakuna uwajibishaji
 
Back
Top Bottom