Matokeo Kidato cha Nne 2016 yatoka, Feza Boys yaongoza!

Matokeo Kidato cha Nne 2016 yatoka, Feza Boys yaongoza!

Meinkempf> ahsante sana kwa kuniangalizia matokeo ya mwanangu fasta na bure kabisa kuliko necta
 
Hapana sijui hilo, ninachojua ni kuwa watanzania wenye asili ya Asia ndio matajiri Tanzania.

Waislam weusi ni matajiri wa mboyoyo mingi mingi
Kaa jidanganye kazi kujisifu mumesoma tetemeko limewaumbua jengeni nyumba zenu kwa division one , ulishawahi kusikia bagamoyo kuna njaa, kwanza vijiji vingi tanzania ndio wanaishi masikini sasa waislamu wengi wanaishi kijijini, wafuate nini?
 
Kwa sasa suala la Elimu ya Msingi na ile ya Upili imekuwa ni jukumu la sekta binafsi
Sekta binafsi ndio inajenga mazingira bora ya elimu na watoto kufanya vizuri kuliko serikali.

Lakini "Social Contract" kati ya wananchi na serikali kila baada ya miaka mitano ya kuomba kura huwa ni malipo ya elimu bora,afya bora na huduma bora za maji na maisha.

Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kutokufuata masharti haya ya "Social Contract" kati yake na wapiga kura.Kuwepo na ukosefu wa shule za serikali ktk kumi bora,ni moja ya uvunjwaji mkubwa wa "mkataba wa kijamii" kati ya serikali na wananchi.Na hapa Serikali inapswa kuadhibiwa.

Unawekaje kipimo sawa kati ya mwanafunzi anayesoma kwa kibatari na chemli kule Iselamagazi Tabora na yule anafanya study Tour Uturuki huku akiwa na mazingira bora ya kusoma?

Na hili kudhihirisha hivyo,kwa sasa huwezi kukuta viongozi wa serikali wakipeleka watoto wao ktk shule za serikali kwa maana na wao hawaamini ktk ubora wa elimu inayotolewa na shule za umma.

Ilboru,Tabora Boys,Mzumbe,Kibaha,Weruweru,Tabora Girls,Kilakala,Msalato na Korogwe Girls zimebaki magofu ya historia ya elimu bora ya Tanzania.Majengo ni toka ya mkoloni.Hakuna jitihada za kimkakati za kurudisha ubora.

Elimu imekuwa biashara badala ya Huduma.Na hao watunga sera wanaopaswa kuirudisha elimu ktk mstari mnyoofu ndio wafanyabishara wa elimu.Waziri anamiliki shule,mbunge anayeisimamia serikali naye anamiliki shule au kuwa na hisa ktk biashara ya elimu.

Katika nchi zilizoendelea,Elimu ya msingi na upili sio biashara,bali ni huduma.Ni huduma kwa sbb ni haki ya kimsingi ya kila mtu kupata elimu ya msingi na ya upili.Ndio maana nchi kama Sweden ni fahari kuwa sehemu ya shule ya serikali kuliko binafsi.

Mazingira ya kielimu ya mtoto aliyeko Kwa Msisi Handeni,ambapo zaidi ya kuwaza masomo,anawaza wapi atapata maji ya kuoga na kunywa si sawa na Marian Girls,ambapo mpaka pedi mtoto anaikutq kati vyoo vya shule,hawa hawawezi kuwa sawa kieleimu na kimtazamo.

Hii ni sawa na kuwaweka ulingoni Dula Mbabe anyecheza ngumi za amacha na Myweather
Its like feather weight boxer vs heavyweight boxer!!Kwa hili tujitathmini upya
wanapaswa kujiuliza upya.Elimu ni bure ama ni gharama?hizo kumi bora hapo juu hakuna hata moja ambayo ni bure.
 
Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha nne 2016. Bofya link hii ili uone
http://41.188.136.77:8080/matokeo/2016/csee/index.htm
necta-logo.png
 
Seminary cku hizi hazifaulishi tena kama zawani

Maua,Uru, St James, USA Seminary......sizikiii tena, What went wrong? ....................................................What went What? What went Wrong
what wenti rongo
 
Kama kuna mtu hajacheck Tokeo alete index no nimchekie bila gharama yeyote ile.
 
Watoto wa DSM wanashinda instagram kupiga umbea na udaku na kutukana mitusi
In haki yao kuburuza mkia
Halafu Dar wanaongoza kwa tuition! Utakuta watoto hawaendi SHULE wanaishia mchikichini na MWENGE kwenye vituo vya tuition!
Wanaponda walimu wao na wanatukuza walimu wa tuition ambao wengi wao ni makajanja!
 
Back
Top Bottom