Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Wananchi leo wanapiga kura kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo linaanza saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni na wale wote watakao kuwa kwenye foleni muda huo wataruhusiwa kupiga kura
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema Uchaguzi huo utafanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini isipokuwa Mikoa mitatu ya Katavi, Ruvuma na Tanga ambapo Wagombea wake katika vyama mbalimbali walipita bila kupingwa
Aidha, Waziri Jafo amewataka Wananchi kushiriki katika zoezi hilo bila kujihusha na vitendo vyovyote vya viashiria vya uvunjifu wa amani au kuvuruga uchaguzi huo
Amesema “Niwaombe Watanzania kwa umoja wao wahakikishe zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu kwa kuchagua viongozi watakaowafaa katika maeneo yao, wajiepushe na vitendo vya kupiga kampeni wakati wa kupiga kura, na kuvaa sare za vyama vyao"
****
Tujuzane yaliyojiri kabla, wakati na baada ya upigaji kura.
Hapa mtaani kwetu, hali bado ni tulivu hakuna kinachoendelea wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila jumapili. Amani imetawala na hofu pia.
Je kwako nini kinajiri?
****
UPDATE
Wananchi wa Mtaa wa Chihikwi, Kata ya Mbarawala, Dodoma Mjini wakiwa wamekusanyika katika kituo cha kupigia kura kuangalia majina yao kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo leo Novemba 24, 2019. AAFP na CCM ndio vyama pekee vinavyoshiriki uchaguzi katika mtaa huo.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni ya kumchagua mwenyekiti wa kitongoji cha Kiwanjani kata ya Tandahimba mkoa wa Mtwara. Wagombea wa vyama vinavyoshiriki ni TLP na CCM. Picha na Haika Kimaro
Wasimamizi wa uchaguzi wakisubiri wapiga kura katika kituo cha Maumba kilichopo mtaa wa Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ericky Boniphace
======
UPDATES: 25 NOV 2019
========
MATOKEO:
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: CCM YASHINDA KWA ASILIMIA 99.9
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo CCM imeshinda Vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9
Amesema kuwa pia chama hicho kimeshinda katika Mitaa 4,263 sawa na asilimia 100, huku kikishinda Vitongoji 63,970 sawa na asilimia 99.4
Amebainisha kuwa CHADEMA kimeshinda nafasi moja ya Wenyeviti wa Vijiji, hakikufanikiwa kupata Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji kimepata nafasi 19, Wajumbe kundi la Wanawake imepata nafasi 39 na Wajumbe kundi mchanganyiko imepata nafasi 7
Chama cha CUF kimepata nafasi moja ya Kijiji, Mitaa miwili, Wajumbe Kundi la Wanawake wamepata nafasi tatu, na Wajumbe kundi mchanganyiko wamepata nafasi 14