Wadau mm nasemaje, CO na MD wote madaktari.. CO ni msaidizi wa MD sasa huwezi kuwa msaidizi wa MD kama wewe umesomea Ualimu au nyadhifa nyingine. Kama hautaki bas andamana..
Hawa ndio madaktari wetu kwenye dispensary Level na kwenye vituo vya Afya na wanaupiga mwingi sana. Maisha ya watanzania wengi hatuwezi kwenda muhimbili, mloganzila, KCMC, Bugando etc labda tatizo likiwa kubwa sana. Ko tunaishi nao na wanafanya kazi kubwa sana..
Wanangu COs nyie ndo madaktari wetu popote mlipo kunyweni soda..
Hawa ma MDS wengi wao wapo shallow sana, wanapenda title kubwa ni sawa, miaka mitano sawa hatujakataa but most wako Empty headed in real practical na katika taaluma ya kutibu haya magonjwa Popular ya kwenye jamii.
Mara mia mtu wa kuheshimiwa ni Specialist, pathologist, Dentist, Dermatologist etc Hawa wengine wamesoma vitu vingi ila ni Basic(rasha rasha) sana