Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

White drone

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2023
Posts
201
Reaction score
386
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

9ADBF5B6-1AAD-4AE6-ADF7-714647D88A52.jpeg
B63BEED2-96AA-4C9E-9F55-4F7A17DCCEE2.jpeg
 
Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Kuna mtu anasema alienda sheli na kidumu alikuwa anataka mafuta kwa ajili ya mashine ya kupulizia dawa akaambiwa aibebe akaweke mafuta kwenye mashine
 
Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Kuna galoni za chuma za kubebea mafuta zinaitwa JERRY CAN zipo hadi za lita hadi 20 japo bei zimechangamka hilo la 20L ni 120,000 hadi 100,000 ila ni galoni za chuma kwa ajili ya kazi hiyo.
 
Ukiona hivyo kuna biashara ya mtu ya kuingiza hizo metal jerry cans, hii nchi ni ya kipuuzi sana tena sana. Nchi inaongozwa na vichwa panzi. Eee Mwenyezi Mungu utulinde na utupe nguvu viumbe vyako dhidi ya viongozi wetu wasio na maarifa kwenye vichwa vyao. Mungu saidia taifa lako pendwa Tanzania linaangamia.
 
Unaweza kutoa sababu za kisayansi na kikemia kuzuia kubeba mafuta kwenye plastiki
Sifahamu masuala ya kemia Mkuu ila madhara yakimazingira ni pamoja na uwezekano wakulipuka au kuvuja hasa petrol ndio maana hata pipe za mafuta kwenye gari sio plastic ni mpira wenye nyuzi. Japo pump huwa ni plastic ila sio nyepesi ipo kama yakuvunjika.

Ukiuangalia mfuniko wa JERRY CAN hata ukiliweka ndani ya gari hautasikia harufu ya petrol, ila sasa chukua galoni la kawaida hata ulikaze vipi hapo ndani lazima msikie harufu ya petrol, maana yake ni kuwa huwenda inavuja maana ile ni kama gesi tu.
 
Kuna galoni za chuma za kubebea mafuta zinaitwa JERRY CAN zipo hadi za lita hadi 20 japo bei zimechangamka hilo la 20L ni 120,000 hadi 100,000 ila ni galoni za chuma kwa ajili ya kazi hiyo.
Lakini hii pia inaweza kuwa fursa kwa wale wanaotengeneza vyombo vya bati kama sufuria n.k naamini wanaweza kutengeneza jerry can za bei nafuu na size tofauti ....
 
Sifahamu masuala ya kemia Mkuu ila madhara yakimazingira ni pamoja na uwezekano wakulipuka au kuvuja hasa petrol ndio maana hata pipe za mafuta kwenye gari sio plastic ni mpira wenye nyuzi. Japo pump huwa ni plastic ila sio nyepesi ipo kama yakuvunjika.

Ukiuangalia mfuniko wa JERRY CAN hata ukiliweka ndani ya gari hautasikia harufu ya petrol, ila sasa chukua galoni la kawaida hata ulikaze vipi hapo ndani lazima msikie harufu ya petrol, maana yake ni kuwa huwenda inavuja maana ile ni kama gesi tu.
Asanteh kwa maelezo yako mkuu
 
Lakini hii pia inaweza kuwa fursa kwa wale wanaotengeneza vyombo vya bati kama sufuria n.k naamini wanaweza kutengeneza jerry can za bei nafuu...
😂😂😂 ule mfuniko wake utawatoa knok out Mkuu maana una kama matundu mawili ila moja huwa sijui linaishia ndani umbali gani. Ile sayansi pale sio yakubahatisha japo inawezekana pia.
 
Back
Top Bottom