Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Ni huzuni kwa kweli, na ukiachana na hivyo tu, haya gari langu limezima kisa wese nahitaji kufika sheli ila sina hayo mafuta nafanyeje sasa??

Kuna baadhi ya vitu hata kuwaza tu unaona jinsi tunavyoyumba
 
Tatizo mnafanya petrol kuwa siasa!
Madhara ya Petrol ni makubwa mno.
Fuateni Sheria za EWURA.
MTANIKUMBUKA
 
Ni huzuni kwa kweli, na ukiachana na hivyo tu, haya gari langu limezima kisa wese nahitaji kufika sheli ila sina hayo mafuta nafanyeje sasa??

Kuna baadhi ya vitu hata kuwaza tu unaona jinsi tunavyoyumba
Unatembea na gari hadi inazima hujui hayo mafuta yatakufikisha umbali gani?
Gage ya mafuta haisomi?
Hapo shida ni serikali au wewe?

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
Mbona yale magari yanayosambaza mafuta kwenye minara ya simu matank yake ni plastki au nayo yamezuiliwa?
Sina hakika kama yale ni mafuta ya petrol ila hata kama ni petrol lile tank ni imara zaidi ya hizi galoni tunanunua elfu 2 mtaani au sio sawa na hizi chupa za maji ya kunywa wanazotumia raia

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
Mbona yale magari yanayosambaza mafuta kwenye minara ya simu matank yake ni plastki au nayo yamezuiliwa?
Hapo sasa!!
Kama kweli wapo serious na hii issue kuna magari itabidi yaondolewe barabarani
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Grahams
 
Back
Top Bottom