Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Hii imegundulika sasa hv au toka zamani mkuu.?
Ni tangu zamani mkuu, nadhani tangu katikati mwa karne ya 20 si zaidi ya hapo. Wenye namba za uhakika watanisaidia.

Tafiti za kwanza za kuhusu usalama wa statiki katika viwanda za plastiki zilifanywa na mashirika kama National Fire Protection Association (NFPA) na American Institute of Chemical Engineers (AIChE),

Hao sasa ndio waliandika miongozo kadhaa kuhusu usalama wa vifaa vinavyohifadhi, kubeba au kusafirishia kemikali.

Miongozo hii iliangazia jinsi plastiki inavyoweza kusababisha umeme wa statiki na hatari zinazohusiana nayo, ikiwemo mlipuko wa kemikali zinazowaka kama petroli.

Ova
 
Kwanini wanazuia mkuu..
Kikemia hii ipoje mpaka wameamua hvo
Serikali ya awamu ya sita inaogopa maandamo yanaweza kutokea vijana wakuchukua mafuta sheli kwa vidumu na kwenda kufanya hujuma kwenye miundombinu ya serikali kama majengo au magari jambo ambalo si kweli..
 
Just use a Jerry Can. Tumezoea maisha ya kiholela sana. Sisi wakati tunakua hakuna mwenye gari alikuwa hana hili dumu maana ilikuwa marufuku kutumia gallons ambazo hazijaruhusiwa kubebea mafuta kitaalamu. And thats the fact so tutazoea tu.
 
Attachments

  • R (2).jpeg
    R (2).jpeg
    262.7 KB · Views: 4
Plastiki inaweza kusababisha umeme wa statiki, hasa ikiwa mvuke wa mafuta unajaa ndani ya chombo. Umeme huu unaweza kuchochea moto au mlipuko.

Mafuta kama petroli ni babuzi na yanaweza kuchochea kemikali kutoka kwa plastiki, jambo linaloweza kuathiri ubora wa mafuta.

Ova
Lugha ya ya AI kabisa hii.
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Badala ya kutatua tatizo wameongeza tatizo
 
😂😂😂 ule mfuniko wake utawatoa knok out Mkuu maana una kama matundu mawili ila moja huwa sijui linaishia ndani umbali gani. Ile sayansi pale sio yakubahatisha japo inawezekana pia.
Moja kati ya inventions ya NAZi scientists
 
Unaweza kutoa sababu za kisayansi na kikemia kuzuia kubeba mafuta kwenye plastiki
Hakuna sababu zozote za maana kwa sasa bali ni kukurupuka kwa wasomi wetu.
Fuso za japan zinakuja na main fuel tank ya plastic,
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.
Ukweli ni kwamba serikai iko sahihi kwenye hili,
Ajali nyingi sehemu za biashara na majumbani ni matokeo ya uwepo wa petrol kwenye vidumu.
 
Pale petrol station kuna mjaza upepo matairi, ana kidumu cha chuma anakupa (unakodisha) ukanunue mafuta halafu unahamishia mwenye kidumu chako cha plastic. Kama huna dumu la plastic anakuuzia yeye kwa buku mbili. Jamaa kaona fursa.
 
Back
Top Bottom