Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Huo ni uwezo halisi wa mamlaka kubuni na kutengeneza ajira kwa Watanzania wasio na kazi.Kinachofuata ipo fursa nyingine yakuuza mafuta ya magendo.Ili kutoa huduma iliyokatazwa katika vituo halali kwa wahitaji..Wenye tumtaji twao msiseme hanma kazi za kufanya.
 
Kwa sie ambao Jerrry Can ni kipengele tutumie Tom Can zetu za mchongo hizi
images (7).jpeg
 
Just use a Jerry Can. Tumezoea maisha ya kiholela sana. Sisi wakati tunakua hakuna mwenye gari alikuwa hana hili dumu maana ilikuwa marufuku kutumia gallons ambazo hazijaruhusiwa kubebea mafuta kitaalamu. And thats the fact so tutazoea tu.
Kwa sasa zinapatikana wapi hapa Dar?
 
Wabongo tupunguze ubishi, hivyo vidumu mpaka siku vilete majanga ndo akili zikae sawa!
Inashangaza mtu anatoa utetezi watu wenye mashine wanunulie kwenye nini, ina maana maisha yenu yote hamjawahi ziona jerry can?
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Kama tatizo ni plastiki,

Basi twende na masufuria yenye mifuniko.

Lakini hiyo biashara Yao walioingiza ya madumu Yao ya vyuma hatutayanunua yatadoda.
 
Hatimaye kumekucha mapambano yanaendelea, huu uzi utatumika kuonyesha hali halisi ya huko mtaani baada ya katazo la kutumia vidumu vya plastiki kuwekea mafuta petrol station!
Yeyote atakaekutana na hali hiyo atuwekee hapa tuone
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Hii kali...
 
Ni tangu zamani mkuu, nadhani tangu katikati mwa karne ya 20 si zaidi ya hapo. Wenye namba za uhakika watanisaidia.

Tafiti za kwanza za kuhusu usalama wa statiki katika viwanda za plastiki zilifanywa na mashirika kama National Fire Protection Association (NFPA) na American Institute of Chemical Engineers (AIChE),

Hao sasa ndio waliandika miongozo kadhaa kuhusu usalama wa vifaa vinavyohifadhi, kubeba au kusafirishia kemikali.

Miongozo hii iliangazia jinsi plastiki inavyoweza kusababisha umeme wa statiki na hatari zinazohusiana nayo, ikiwemo mlipuko wa kemikali zinazowaka kama petroli.

Ova
Hapa sasa serikali haina makosa. Kumbe wamekazia aina ya vidumu vinavyoweza kununulia mafuta na siyo kuwa wamepiga marufuku?
 
Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Beba mashine yako ya kupasulia mbao kajaze mafuta sheli
 
Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Huwa ni mihemko ya wanasiasa kwasababu hawakumbwi na kadhia yoyote kati ya hizo
 
waliopo upande huo wanakurupuka sana, eti nenda na dumu la chuma alafu liwe ndani ya mfuko ndipo wakupe mafuta. Yaani tuna viongozi wenye uwezo finyu sana wa kudadavua mambo. Tunaumia na kuangamia kwakweli...yaani wamekosa mawazo mazuri ya kutatua hili....tunaamini hawa wakitumia magari mazuri wakala vizuri wakakaa kwenye ofisi nzuri na tukawalipa vizuri..watatuhudumia vizuri maana watapata utulivu wa akili zao...kumbe hakuna kitu MAPOYOYO TUPU YAMEJAA HUKO JAMANI
 
Google maana ya Cans kwanza usikurupuke
Hakuna can ya plastic

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
Idea ni kwamba vibebeo mafuta vya kisasa ni vya plastic huko first world na kuna magari kibao yanakuja na plastic fuel tanks.
Jery cans kilikuwa kibbeo mafuta maarufu enzi hizo ndo maana jina limehama na umaarufu wake,
 
Mbona yale magari yanayosambaza mafuta kwenye minara ya simu matank yake ni plastki au nayo yamezuiliwa?
 
Back
Top Bottom