Matokeo ya Serikali kukataza kutumia vifaa vya plastiki kununulia mafuta kutoka Petrol Station

😂😂😂 ule mfuniko wake utawatoa knok out Mkuu maana una kama matundu mawili ila moja huwa sijui linaishia ndani umbali gani. Ile sayansi pale sio yakubahatisha japo inawezekana pia.
Wataweza tu naamini, kama jerry can haina Bluetooth, processor au circuit ina metal pekee naamini wanaweza...
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Kuna sheria nyingine zinatungwa ilimradi zinatungwa tu, sasa mtu kazi nikiwa na pikipiki kilometa 2 kabla ya sheli wanataka alikokote hilo kopo mpaka sheli wakati ni rahisi kuchukua kidumu, kufuata mafuta na kurudi; sababu gani kwanza kuzuia ?
 
Ukipata picha utuwekee mkuu tuuone tusije kutolewa lko out
Hizo hapo jerry can Mkuu, sasa hiyo iliyo wazi hapo huo mdomo kwa ndani una sehemu mbili. Kesho nitapiga picha langu kwa ndani ulione lilivyo huo mdomo.
 
Attachments

  • images (38).jpeg
    images (38).jpeg
    17.4 KB · Views: 2
  • 98bed677ed45cd35c1a9ce84b754a56e8fbae10b_2_PIA_53553_0_100.png
    98bed677ed45cd35c1a9ce84b754a56e8fbae10b_2_PIA_53553_0_100.png
    1.2 MB · Views: 2
Serikali yenu haikuwaza kuwa mafuta yanatumika pia kwenye mashine za kusaga,Engine za boti na mitambo mengine,ambapo pia kwenda na hivyo vitu petrol station ni kazi?!
Ogopa wajinga wakiwa wengi wanaweza kujitwalia madaraka au wakachagua Rais! Matokeo yake ni kuwa na viongozi na watendaji ambao licha ya kuwa na elimu ya darasani ni wajinga when it comes to the real life situation! Akili Yao ilikua tu ni mobile vehicles tu Ndio zinatumia petroleum!
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Mnajua kwa nini wamekataza?

Wamiliki wengi wa vituo vya mafuta ni mabosi serikalini. Kwa kuwa wamejipanga kuiba mafuta kupitia vipimo, itakuwa aibu kwa vidumu kujazwa lita tatu kwa malipo ya lita tano.

Jiulize, tofauti ya mfuta na oil zinazouzwa kwenye vidumu ni ipi?

Ndugu zangu, CCM ni janga
 
Kuna sheria nyingine zinatungwa ilimradi zinatungwa tu, sasa mtu kazi nikiwa na pikipiki kilometa 2 kabla ya sheli wanataka alikokote hilo kopo mpaka sheli wakati ni rahisi kuchukua kidumu, kufuata mafuta na kurudi; sababu gani kwanza kuzuia ?
Kuna galoni za hiyo kazi Mkuu mbona ni rahisi kabisa kuepuka ghasia
 
Sifahamu masuala ya kemia Mkuu ila madhara yakimazingira ni pamoja na uwezekano wakulipuka au kuvuja hasa petrol ndio maana hata pipe za mafuta kwenye gari sio plastic ni mpira wenye nyuzi. Japo pump huwa ni plastic ila sio nyepesi ipo kama yakuvunjika.

Ukiuangalia mfuniko wa JERRY CAN hata ukiliweka ndani ya gari hautasikia harufu ya petrol, ila sasa chukua galoni la kawaida hata ulikaze vipi hapo ndani lazima msikie harufu ya petrol, maana yake ni kuwa huwenda inavuja maana ile ni kama gesi tu.
Wameweka mazingira ya hizo Jerry can kupatikana kwa unafuu na Kwa wakati? Ukute Ndio waziri ameagiza sitakuja next moon
 
Mnajua kwa nini wamekataza?

Wamiliki wengi wa vituo vya mafuta ni mabosi serikalini. Kwa kuwa wamejipanga kuiba mafuta kupitia vipimo, itakuwa aibu kwa vidumu kujazwa lita tatu kwa malipo ya lita tano.

Jiulize, tofauti ya mfuta na oil zinazouzwa kwenye vidumu ni ipi?

Ndugu zangu, CCM ni janga
Anhaa, nakuelewa, ina maana hawataki vyombo transparent.. kwamba wataumbuka..
 
Kwanini wanazuia mkuu..
Kikemia hii ipoje mpaka wameamua hvo
Plastiki inaweza kusababisha umeme wa statiki, hasa ikiwa mvuke wa mafuta unajaa ndani ya chombo. Umeme huu unaweza kuchochea moto au mlipuko.

Mafuta kama petroli ni babuzi na yanaweza kuchochea kemikali kutoka kwa plastiki, jambo linaloweza kuathiri ubora wa mafuta.

Ova
 
Sasa hii ni sheria imepitishwa au ni TANGAZO mmoja wao kakerwa kaamua kutupasha wadanganyika?
Watwambie tutumie vyombo vipi/vya aina gani na ikiwezekana waambatanishe taarifa /tangazo hili na picha za vinavyo shauriwa.
 
Ni takribani miezi miwili sasa tangu serikali ipige marufuku matumizi ya vifaa vya plastiki (vidumu vya lita tano au madumu ya lita 20) kuchukulia mafuta kutoka vituo vya mafuta.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na hili jambo ambalo sasa watu wengi ambao wana uhitaji wa mafuta wanatumia njia hii ili kuweza kupata mafuta.

Wanachofanya ni kwamba wanaongea na dereva wa bodaboda anaenda sheli kuweka mafuta kwenye pikipiki halafu waotoa kwenye pikipiki na kuweka kwenye kidumu, wenyewe wanaita kunyonya.

View attachment 3154050View attachment 3154051
Huyo ni mtanzania, ukimzuia huku anatokea kule
 
Plastiki inaweza kusababisha umeme wa statiki, hasa ikiwa mvuke wa mafuta unajaa ndani ya chombo. Umeme huu unaweza kuchochea moto au mlipuko.

Mafuta kama petroli ni babuzi na yanaweza kuchochea kemikali kutoka kwa plastiki, jambo linaloweza kuathiri ubora wa mafuta.

Ova
Hii imegundulika sasa hv au toka zamani mkuu.?
 
Wameweka mazingira ya hizo Jerry can kupatikana kwa unafuu na Kwa wakati? Ukute Ndio waziri ameagiza sitakuja next moon
Jerry can zipo tangu enzi ya Hayati Mzee Ruksa, ni vile watanzania wengi hawajifunzi na kufuatilia mambo. Hii ni bidhaa iliyotumika tangu vita ya dunia.

Watu wafuate taratibu, tuache kuishi kwa mazoea. Kulalamika hakusaidii kitu. Mtu akimiliki chombo kinachotumia petrol basi anunue na vifaa vyake na sio kulalamika.
 
Plastiki inaweza kusababisha umeme wa statiki, hasa ikiwa mvuke wa mafuta unajaa ndani ya chombo. Umeme huu unaweza kuchochea moto au mlipuko.

Mafuta kama petroli ni babuzi na yanaweza kuchochea kemikali kutoka kwa plastiki, jambo linaloweza kuathiri ubora wa mafuta.

Ova
Kama vile ina make sense lakini wangetoa mwongozo ni aina gani ya vyombo vinavyotakiwa kubebea mafuta na kurahisisha upatikanaji wake nadala yake wametoa tangazo tu la kukataza
 
Back
Top Bottom