Sikiliza na hii:
Kuna jamaa hapa kazini alienda study tour Tanga. Huko akapata kimwana wakafika bei. Study tour ilipoisha huyu jamaa alikuwa kashanogewa, akaenda mpaka kwa wazazi wake akajitambulisha kiaina. Jamaa akarudi Dar, akaendelea kuwasiliana na kidemu chake. Wakakubaliana demu akaja Dar. Jamaa akampangia demu gesti maeneo ya karibu na kazini. (Ikumbukwe jamaa huyu anafanya kazi kampuni moja na mkewe, jamaa anafanya kazi za shifti, waifu office hours)
Jamaa likiingia naiti linafanya maarifa linachomoka linaenda gesti linapiga infidelity. Asubuhi waifu yuko job jamaa linaenda tena gesti linakula mzigo. Siku ikafika. Jamaa asubuhi linaenda gesti kupiga infidelity likakuta demu kalala kitandani wa baridiiii! Shughuli ikaanzia hapo.
Ila watu hawaamini mke wake hakujua, manake watu walipiga mchango kisirisiri (Ma-infidelitaz huwa hawaangushani, msisahau), watu wa kusindikiza maiti wakakodiwa na kulipwa maiti ikapelekwa Tanga kwa wawazi wake bila mke kujua! Jamaa lilicheza dili na bosi wake likapewa tripu ya uongo na ukweli kwenda Tanga, likasindikiza maiti likazika kwa heshima zooote.
Hakyanani infidelity we acha tu!!!