Matumizi ya ngano yawe mbadala wa ugali Afrika Ili kuondoa Ujinga

Mbona Israel hakuna Ujinga kama huku,

Yaani Ule ngano isiyokobolewa, saa ngapi uwaze kuongoza watu kimabavu Kwa kuiba kura?
Hapo kura kuibiwa ni viongozi kujijali wenyewe ......AFu pia sisi ukiangalia idadi kubwa ya wapumbavu ni nyingi kuliko wenye akili maana hatupendi kujifunza na kusoma vitabu kwahio ubongo hatuupi chakula chake
 
Chakula Cha ubongo ni kusoma vitabu sio ngano
 
Unauponda ugali wakati huo huo nimetoka kumuona Cardi B akiwa ame pack lunch box yenye mahindi ya kuchemsha kwa ajili ya mwanae shuleni
 
Ni umasikini wetu tu, lakini ugali hauna tatizo lolote. Hata hivyo vyakula mnavyodhani vinavirutumisho, huwa vinaongezewa viwandani. kama mtengenezaji ana claim kuna Carb, sijui Vit kiasi fulani, mara nyingi zinaongezwa.
hata kwenye unga unaweza ongeza hizo vitamins au nutrients unazotaka ukala ugali wako ukawa sawa na aliye kula vyakula unavyodai vinaleta akili.

Sisi vyakula yetu vingi tuna kula organic au unprocessed food, hivyo havina hizo label za content lakini vina virutubisho vingi tu, tena kushinda hata hivyo mnavyosema.

Tuna kula samaki fresh, tuna kula mboga toka shambani, matunda toka mtini moja kwa moja, tunalima kizamani, na siyo indor farms kama wazungu. hivyo naamini vyakula vyetu laba useme havian muonekano mzuri, lakini nutrients ni za kumwaga.

Tanzania Food Nutrition Center(TFNC) wanaweza kukujuza haya yote unayodharau hapa. Mnajali Protein added Value label bila kujua hizo added value zinatoka wapi, siyo natura zinatengenezwa. Lakini zakwetu ni natural.

Unataka Carbs, kula ugali wa Mtama mwekundu, utazipata carbs za kutosha, Ukitaka protein kula samaki, Nyama au kunywa maziwa.

Sisi tunaakili na ugali wetu huu huu, sema kuna wachache wanatuangusha, wanakula mbegu zetu za asili, halafu wanapiga pesa wana taka kutuletea GMO's. Nyie mnawaita wanasiasa, wanatuletea minazi mifupi sijui ya wiki mbili, tunapokea. Miche ya maembe ya siku 10, tunapokea, sijui Michungwa ya siku 3 tunapokea, halafu mnakuja humu mnatunanga soote hatuna AKILI kwasababu tunakula ugali.

Hatutaki ngano, tunataka unga wa Muhogo,Mahindi, Mtama ,Uwele, au Ulezi, Ngano kuleni nyie mnaotaka Protein.
 
Tunajilibwasa
 
Umetoa ushauri mzuri
Lakini kilimo ni pure science pia ni biashara.
Je jiulize mara ya mwisho kuyaona matikiti ya kienyeji ni lini, jale matikiti ya rangi nyuesi , haya matikiti ya zebra ni GMO.

Due to global population, tz ss ina watu 60 ml. Mashamba yetu ni heka kumikumi, utavuna kiasi Gani kwa mbegu za kienyeji kwa hii global warming and pollution.

Tunapoelekea ni kubaya Zaidi
Lazima tuambiane ukweli, zitumike njia salama za science kilimo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…