UKUAJI WA SEKTA YA MAWASILIANO NCHINI
Namshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kunipa fursa ya kuchangia mawazo muhimu yatakayosaidia TANZANIA yetu katika miaka 5-25 ijayo, kupitia Jamii forums. Dunia ya sasa imetawaliwa na mifumo ya utandawazi kupitia teknolojia ya viwango vya juu ya matumizi ya mtandao. Ambapo taasisi zisizo za kiserikali na za kiserikali zinatumia fursa hii hasa kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii, na tovuti ili kuwasilisha taarifa na kuonyesha mipango na utendaji wao kazi,kuajiri, kujitangaza kimasoko na matumizi mengineyo.
Kuakisi hayo, Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 33.1 Mwezi Aprili,2023 hadi kufikia milioni 36.8 Mwezi Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 11.2. (Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2024/25). Hii inamaanisha kwamba tuna wastani wa watumiaji zaidi ya milioni 1.187 wa intaneti kwa kila mkoa kwenye nchi yetu.
MATATIZO YANAYOIKUMBA NCHI YETU NA CHANGAMOTO ZA TAARIFA (MAWASILIANO) YA UWAZI.
Ni bayana kuwa Tanzania bado ina safari ndefu ya kuhakikisha kila Mtanzania ana maisha bora kwenye Nyanja zote za Huduma za Kijamii, Kisisasa, na Kiuchumi. Mfumo wa Utawala kwenye jamii zetu kwa kiasi kikubwa unatawaliwa na Serikali za mitaa kwa kuanzia ngazi za Utendaji wa Kijiji mpaka Baraza la Madiwani kwenye halmashauri na wilaya zetu, ambapo kwa kiasi kikubwa hazipewi mamlaka ya moja kwa moja kuanzisha na kutekeleza miradi ya kutatua migogoro kwa wananchi, hii inaweza kutokana na ufinyu wa bajeti na mapato kwenye halmashauri zetu, ila kwa kiasi kikubwa inatokana na mfumo wa utawala na Katiba kwenye nchi yetu ambapo mamlaka na nguvu kwa kiasi kikubwa imepewa Serikali kuu.
Sisi sote ni mashahidi ya migogoro inayoibuliwa na kutatuliwa kwenye sekta ya Ardhi, ambapo Waziri wa sasa Mb. Jerry Slaa amejaribu kupambana nayo, Wote tulikuwa mashahidi Wakati Mkuu wa mkoa wa sasa wa Arusha Rc. Paul Makonda alipokuwa Katibu wa NEC (Itikadi na Uenezi) kwenye ziara zake ambazo aliibua migogoro kibao ya wananchi kwa viongozi wao, pamoja na matatizo yanayoikumba sehemu kubwa nchini ambayo hayazungumzwi. Pia tumekuwa mashuhuda kwa kuona jamii forums ikitoa fursa kama jukwaa la wana jamii wa Kitanzania kutoa kero zao na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Sote tumekuwa mashahidi kwenye jamii zetu ambazo watu wanatumia vyeo na madaraka vibaya kuwakandamiza na kuwanyonya watu wa chini. Tumekuwa mashahidi kuona biashara na shughuli zisizo rasmi kutendeka bila hatua za kisheria kutimizwa.
DOSARI KATIKA UWASILISHWAJI WA TAARIFA
Tunafahamu ya kuwa tunachaguzi za wabunge kila baada ya miaka mi 5, kutuwakiliska wanachi na matatizo kwenye chombo cha bunge ambao ni mhimili na nguzo kubwa kwenye serikali yetu. Tanzania tuna wilaya Zaidi ya 180, ina maana tuna wabunge zaidi ya 180 kwenye bunge letu tofauti na wa viti maalum. Nina hakika kuwa kwenye vikao vya bunge mda wa dakika 10-20 hautoshi kwa kila mbunge kuzungumza mambo yote yanayoikumba jamii yake, hii ina fanya kuwa na dosari kwenye njia ya kusikiliza wananchi kwa kupitia wawakilishi wao bungeni.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI YA SHIRIKA LA POSTA KAMA NJIA YA MAWASILIANO KATI YA SERIKALI KUU NA WANANCHI WAKE
Shirika la Posta limekuwapo nchini kwa muda mrefu likifanya shughuli za usafirishaji wa barua, rejesta, vipeto na vifurushi, na huduma nyingine kama fedha na uwakala, Biashara mtandao na nyingine nyingi. Napendekeza yafuatayo ili kuhakikisha kuna mawasiliano bora kati ya wananchi na viongozi wao:
1. Serikali irasimishe Shirika la Posta kuwa njia kuu ya mawasiliano kati ya wananchi na viongozi wao kwa mfumo wa Barua. Hili litatukwa na uwepesi kidogo kwa kuwa kila ofisi kuanzia mkuu wa wilaya, wa mkoa, za wabunge, mawaziri zina anwani ambazo zitarahisisha uwasilishwaji wa barua kutoka posta. Pia itakuwa ni msaada kwa watu wanaoishi mbali na ofisi za serikali za mitaa, serikali ya wilaya, mkoa, pia na ofisi za mawazirikwa kutumia Posta kiganjani.
2. Sheria ziwekwe katika mfumo wa utumaji wa barua tofauti na barua za kawaida. Mfano wa Sheria ziwe:
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI YA MTANDAO WA INTANETI KAMA NJIA YA MAWASILIANO KATI YA WANANCHI NA VIONGOZI.
Tovuti za ofisi za wizara, ofisi za wakuu wa mikoa, pamoja na halmashauri zimekuwa na sehemu ya huduma za mawasiliano kama kuwekewa namba za simu, barua pepe na anwani lakini kwa kiasi kikubwa hazina ufanisi wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, ambapo simu nyingine hazipokelewi na nyingine kutopatikana, au barua pepe kutojibiwa. Napendekeza lifuatalo ili kuhakikisha kuna mawasiliano thabiti kati ya viongozi na wananchi wake:
Kwa kuhitimisha, Moja ya nguzo kubwa ya maendeleo kwenye nchi ni kuwa na taarifa kamili juu ya matatizo tuliyonayo na wapi pa kuanzia kutatua matatizo hayo. Hili linaweza kutokea kama tuna mifumo mizuri na njia sahihi za wananchi kuongea na viongozi wake hasa wa ngazi za juu. Tanzania Tuitakayo inawezekana.

- Barua zinazotumwa kwa viongozi wa juu wa serikali ziwe za haraka,
- Sheria za uhakika wa usalama kwa wananchi mfano (Mwandishi atayeweka anwani yake yupo tayari kufahamika na kujibiwa, na yule asiyeweka anwani taarifa zake zifanywe siri.
- Muda wa kujibu Barua kwa Kiongozi aliyeandikiwa usizidi miezi 6.
- Mwisho wa mwaka kuwe na tathmini kwa viongozi wameweza kwa kiasi gani kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wa kazi yao zilizotumwa kwao.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI YA MTANDAO WA INTANETI KAMA NJIA YA MAWASILIANO KATI YA WANANCHI NA VIONGOZI.
Tovuti za ofisi za wizara, ofisi za wakuu wa mikoa, pamoja na halmashauri zimekuwa na sehemu ya huduma za mawasiliano kama kuwekewa namba za simu, barua pepe na anwani lakini kwa kiasi kikubwa hazina ufanisi wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, ambapo simu nyingine hazipokelewi na nyingine kutopatikana, au barua pepe kutojibiwa. Napendekeza lifuatalo ili kuhakikisha kuna mawasiliano thabiti kati ya viongozi na wananchi wake:
- Iundwe tovuti moja inayounganisha Ofisi za serikali kuanzia ngazi za wizara mpaka wilaya. Ambapo mwananchi atapata fursa ya kutuma ujumbe au taarifa kwa kiongozi husika moja kwa moja mtandoni, utaoweza kuhakikiwa na jopo la wataalamu kwa kuzingatia kanuni na taratibu.
- Mapato kwa nchi yetu, kulingana na gharama za kutuma barua
- Kufichua uhalifu, kama usalama utahakikishwa kwa mtoa taarifa.
- Utatuzi wa haraka wa matatizo ya wananchi kwakuwa na taarifa sahihi.
- Kuongezeka kwa uaminifu kwa Serikali tawala, kwa kuwa kuna uwazi na uwajibikaji wa moja kwa moja.

Upvote
19