Matumizi yangu ya mwezi

Toa hiyo elfu 80000 ya wazazi peleka kwenye mahitaji mengine ya msingi km vile mawasiliano,usafiri kwa mke,dharura aidha michango n.k...Inshu ya ada kaweka wastani kwa watoto wawili.......Hiyo nayo ipeleke labda kwenye kununua mavazi ya familia na mahitaji mengine ya msingi ambayo kayaacha
 
Sijajua umri wako, ila roughly utakuwa unacheza kwenye 35-45s

Ni hatari sana Kwa umri huo kukosa kuweka akiba

Kama mna nyumba kubwa, hao Wazee walete uishi nao hapo kwako, then hiyo 80,000 unayotuma ifanye akiba.

Pia anza kulipia kifurushi cha 28,000 Azam badala ya hiyo 35,000

Hujaweka matumizi yako ya simu pia/Bando n.k

Anza kufikiria kuhusu ujasiriamali binafsi, huo mshahara hautoshi brother
 
Chakula ukiwa kazini, vocha, nguo na viatu kwa watoto, emergency cash
 
Chakula nunua in bulky Kila mwezi, hiyo pesa itapungua na uwaambie watumie vizuri...pia shule tafuta za 1.5mil kwa mtoto mmoja, maana maisha yenyewe mafupi utakosa pesa za kuenjoy bure
 
kwahiyo yaani kimsingi beki tatu haajiriwi, anapata sehemu ya kuishi vizuri, analipia kwa kusaidia kazi za ndani.

hizo 50k 50k zinaweza kumsaidia mtu kweli?
 
Kianzishwe chama cha mayaya tanzania, wawe na vibali, wapate mafunzo, na njia bora za kuwapatia maslahi zijadiliwe.
 
kwahiyo yaani kimsingi beki tatu haajiriwi, anapata sehemu ya kuishi vizuri, analipia kwa kusaidia kazi za ndani.

hizo 50k 50k zinaweza kumsaidia mtu kweli?
Assume unafanya kazi ofisini kwa mwezi unalipwa Laki 3.5.
Unalipa kodi, unanunua chakula, mavazi n.k
Hiyo pesa inatosha hayo mahitaji? Je, utabakiwa hata na hiyo 50k anayolipwa beki 3.
 
Hapo kuweka saving ngumu. Maana kuna vitu vingi vinavyokula pesa kwenye maelezo yako havipo.
 
Kuna chai na chakula cha mchana, bando la simu. Mengi hujaandika hapo unabaki na deficit mkuu. Vipo vingi kwa downgrade hapo kulingana na kipato. Ada iwe nusu ya hiyo uliyoandika ikiwezekana
 
Hela yako ya Kula kila siku kazini ni hapo kaka?
 
Kuna watu wanaumia kny budget za watu😂😂
Mtu yeyote mwenye akili timamu hupanga budget at a maximum. Inawezekana kwa mwezi asitumie hiyo 450K as kuna vitu vinaweza tumika hata miezi miwili. Nauli kuna siku anaweza kupata lift au hajaenda kazini.

Kwa haraka haraka kubaki na 200k kwa mwezi sio mbaya. Kuna watu wengi sana wanabaki na -200K kwa mwezi hapa na wapo kukucheka na kukudhihaki mtoa mada. Wengine mpaka wanawakopa wadada wao wa kazi au hawawalipi mshahara kwa vile budget imekaba
 
Akiongeza idadi ya wazee wawili nyumbani kwake gharama za maisha zinapanda.

Kwa bajeti yake mtu mmoja kwake anakula 3,000 kwa siku jambo ambalo linashangaza kwa gharama kubwa za maisha hapa mjini.
Akileta wazazi inaongezeka 6,000 kwa mwezi ni 90,000 kwenye kula tu. Haijaongezeka bajeti ya maji, umeme, sadaka, kuumwa maana wamebadilishwa mazingira na umri wao umeenda, zawadi. Na bado stress na kukosekana uhuru kwake yeye na mke wake.

Bora alipe hiyo 80,000 wabaki kwao.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu

Kwa hizo gharama za maisha, vyema ajikite kufanya ujasiriamali kidogo ili kujiongezea kipato

Kipato chake hakitoshi, kulingana na idadi ya wategemezi alionao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…