Matumizi yangu ya mwezi

Matumizi yangu ya mwezi

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
318
Reaction score
1,597
Nna familia ya watu wazima 3, (mimi, wife, beki 3 na watoto 2)
Kula 15,000/siku - 450,000
Tv azam 35,000
Umeme 30,000
Maji dawasco 15000
Beki 3 - 50,000
Wazazi 80,000
Nauli job 4000/siku - 120,000
Ada 4m/mwaka = 330,000/mwezi
Silipi kodi
Total 1.1m
Income 1.3m
 
IMG_20241010_013700.jpg
Nipo kwenye umri wa kuangalia TV kwa style hii hata muda wa kukaa kupiga hesabu sina mimi bora sina nachodaiwa maisha yanaenda,ukipiga sana hesabu mwisho utaona kama unaibiwa.
 
Jaribu kupunguza Ada za watoto mzee.
Hutafanya kitu kwa mwaka. Angalia yafuatayo kama ni muhimu pia

1.Sadaka
2.Nguo kwa familia nzima hasa wife na watoto.
3.Kujipa starehe wewe mtafutaji.(Pombe kidogo)
4.Huchepuki bro.. (Sio lazima)
 
Nna familia ya watu wazima 3, (mimi, wife, beki 3 na watoto 2)
Kula 15,000/siku - 450,000
Tv azam 35,000
Umeme 30,000
Maji dawasco 15000
Beki 3 - 50,000
Wazazi 80,000
Nauli job 4000/siku - 120,000
Ada 4m/mwaka = 330,000/mwezi
Silipi kodi
Total 1.1m
Income 1.3m
Chakula muhimu Ila India mafutaTv
10000/=✓
Beki 3🔨🤷
Nauli ??? Ila Kama uko dar
 
Nna familia ya watu wazima 3, (mimi, wife, beki 3 na watoto 2)
Kula 15,000/siku - 450,000
Tv azam 35,000
Umeme 30,000
Maji dawasco 15000
Beki 3 - 50,000
Wazazi 80,000
Nauli job 4000/siku - 120,000
Ada 4m/mwaka = 330,000/mwezi
Silipi kodi
Total 1.1m
Income 1.3m
Mbona hujaweka na mengineyo? Maana hivyo vitu vyote ni vya lazima kila mwezi kwa mujibu wako..

Vitu kama maji, vocha, n.k. Ni lazima utatumia pesa kwenye mambo mengine ukiacha hayo uliyoyaorodhesha. Au huweki bando mzee?
 
Toa watoto shule hiyo ya English Medium, peleka ya wastani za mil 2 ziko nyingi sana na nzuri

Nafikiri ungemhoji kwanza kujua mazingira anayoishi.. watoto 3 kwa ada ya milion 4 kwa mwaka kwa kipindi hiki ni resonable unless akitoka hapo awarudishe "mtakuja primary School"

Na wote tunajua shule za serikali zenye walau ubora wa elimu ni za kuhesabu.. shule watoto 60+ kwenye darasa moja..

Sawa pengine kuna shule nyingi private zenye ada nafuu na ni nzuri ila pengine ambapo yeye anapoishi hazipo

Sasa kama kuna shule nzuri bei nafuu ipo kimara na yeye anakaa bunju au kigamboni amhamishir mtoto huko

Nilihamisha watoto shule mbili za nafuu. Sababu ya ubovu wa Elimu wanayotoa ilibidi nipandishe budget maana ninaposhi shule zilizokuwa nzuri kielimu ada ilikuwa juu kias na zenye nafuu ndo hizo ambazo mtoto ukikagua madaftar unaona YES. Ukimuhoji unajiuliza ya kwenye daftari kafanyiwa au kafanya mwenyewe

Kuja kuchunguza nikagundua walikuwa kwa makusudi wanawafundisha vitu vyepesi mno over and over again ili kuwaridhisha wazaz tu. Wao wana focus kuwa ridhisha wazazi na vi tour vya ajabu ajabu na kufocus kwenye kingereza tena cha kukariri

Mtoto anayeingia darasa la kwanza anakuwa hajui kusoma na kuandika

Nikawatoa shule zote hizo.. kuwapeleka shule walizo sasa.. miez sita tu ya kwanza kwenye shule hizo ni kama walikuwa mwaka mzima unaona kabisa kuna kotu wamegain.. na wako vizuri hawana tour za kijinga za kila mwezi wala class party mara sijui leo
Birthday ya huyu kesho ya huyu kama walikotoka.. tour zote ni za kkumjenga mtoto na once or twice a year.. ni shule ya private ila mtoto wa kike aidha kunyoa au kusuka mnyoosho full stop wa kiume nywele fupi.

So ishu sio kupunguza gharama za ada kutafuta unafuu.. pia ubora wa elimu uwepo..

Bora nigharamie elimu kubwa kama watoto wanapata kitu.. maana ndio urithi wa kwanza ambao wanaupata toka wadogo.. mali nimurithi wa baadae sana.. na tena kama hakujengwa misingi mizuri ya Elimu na Discipline ya kutosha hizo mali watazipoteza kabla hata hujaoza huko kaburini.. so kuliko niwapeleke kwenye unafuu ambako miaka 10 baadae tunaanza kutafutiana vi crushing course wacha wasome kwa gharama inayostahilo ndo tulipofika kama Taifa

Msikariri jaman wote tumesoma kamumba ila Elimu ya Enz hizo sio sasa.. na hizo shule za Private washajua kasimba za wazaz wa kisasa..

HAKUNA MZAZ ANAEPELEKA MTOTO SHULE ZA GHARAMA KWASABABU AONEKANE ANA PESA .. kila mtu anapenda unafuu kwenye maisha ila kuna vitu huwez ku comprimise

ELIMU NA AFYA SIO VITU VYA KU COMPRIMISE.. maana usipokuwa makini jinsi utakavyopambana kupunguza gharama ndio unailimbikiza gharama huko mbele

Sasa hv serikali imeanzisha english medium zake za majaribio hawjafika hata darasa la 4 toka waanze kuna moja iko chamaz kuna kinondon na kwingine ila ziko chache sana..mwanzo mzuri ila labda 10years baadae huko

Jinsi shule za serikal ubora wa elimu unavyopungua ndio hawa wa private wanavyolegea kwenye ubora
 
Hapo kinachokuumiza zaid ni ada za watoto...... Pia kwenye chakula hapo hauna dicpline sana 450,000 ni pesa nying sana kwa kula tu ndani ya mwezi mmoja......... Jaribu kununua vitu vya jumla kam unga kg25, mchele kg20, mafta ya kula lt5, maharage kilo10, dagaa kg3, sukar kg5, ukipiga hesabu hapo haifik hata 200,000
 
Kuja kuchunguza nikagundua walikuwa kwa makusudi wanawafundisha vitu vyepesi mno over and over again ili kuwaridhisha wazaz tu. Wao wana focus kuwa ridhisha wazazi na vi tour vya ajabu ajabu na kufocus kwenye kingereza tena cha kukariri
Nahisi Mtoto wangu wa miaka minne anapitia hii hali.
Anafundishwa ABCD wakati hajui kabisa AEIOU.

Na sasa hivi kuna pesa inatakiwa kwa ajili ya tour November.

Ni balaa sana!
 
Back
Top Bottom