Toa watoto shule hiyo ya English Medium, peleka ya wastani za mil 2 ziko nyingi sana na nzuri
Nafikiri ungemhoji kwanza kujua mazingira anayoishi.. watoto 3 kwa ada ya milion 4 kwa mwaka kwa kipindi hiki ni resonable unless akitoka hapo awarudishe "mtakuja primary School"
Na wote tunajua shule za serikali zenye walau ubora wa elimu ni za kuhesabu.. shule watoto 60+ kwenye darasa moja..
Sawa pengine kuna shule nyingi private zenye ada nafuu na ni nzuri ila pengine ambapo yeye anapoishi hazipo
Sasa kama kuna shule nzuri bei nafuu ipo kimara na yeye anakaa bunju au kigamboni amhamishir mtoto huko
Nilihamisha watoto shule mbili za nafuu. Sababu ya ubovu wa Elimu wanayotoa ilibidi nipandishe budget maana ninaposhi shule zilizokuwa nzuri kielimu ada ilikuwa juu kias na zenye nafuu ndo hizo ambazo mtoto ukikagua madaftar unaona YES. Ukimuhoji unajiuliza ya kwenye daftari kafanyiwa au kafanya mwenyewe
Kuja kuchunguza nikagundua walikuwa kwa makusudi wanawafundisha vitu vyepesi mno over and over again ili kuwaridhisha wazaz tu. Wao wana focus kuwa ridhisha wazazi na vi tour vya ajabu ajabu na kufocus kwenye kingereza tena cha kukariri
Mtoto anayeingia darasa la kwanza anakuwa hajui kusoma na kuandika
Nikawatoa shule zote hizo.. kuwapeleka shule walizo sasa.. miez sita tu ya kwanza kwenye shule hizo ni kama walikuwa mwaka mzima unaona kabisa kuna kotu wamegain.. na wako vizuri hawana tour za kijinga za kila mwezi wala class party mara sijui leo
Birthday ya huyu kesho ya huyu kama walikotoka.. tour zote ni za kkumjenga mtoto na once or twice a year.. ni shule ya private ila mtoto wa kike aidha kunyoa au kusuka mnyoosho full stop wa kiume nywele fupi.
So ishu sio kupunguza gharama za ada kutafuta unafuu.. pia ubora wa elimu uwepo..
Bora nigharamie elimu kubwa kama watoto wanapata kitu.. maana ndio urithi wa kwanza ambao wanaupata toka wadogo.. mali nimurithi wa baadae sana.. na tena kama hakujengwa misingi mizuri ya Elimu na Discipline ya kutosha hizo mali watazipoteza kabla hata hujaoza huko kaburini.. so kuliko niwapeleke kwenye unafuu ambako miaka 10 baadae tunaanza kutafutiana vi crushing course wacha wasome kwa gharama inayostahilo ndo tulipofika kama Taifa
Msikariri jaman wote tumesoma kamumba ila Elimu ya Enz hizo sio sasa.. na hizo shule za Private washajua kasimba za wazaz wa kisasa..
HAKUNA MZAZ ANAEPELEKA MTOTO SHULE ZA GHARAMA KWASABABU AONEKANE ANA PESA .. kila mtu anapenda unafuu kwenye maisha ila kuna vitu huwez ku comprimise
ELIMU NA AFYA SIO VITU VYA KU COMPRIMISE.. maana usipokuwa makini jinsi utakavyopambana kupunguza gharama ndio unailimbikiza gharama huko mbele
Sasa hv serikali imeanzisha english medium zake za majaribio hawjafika hata darasa la 4 toka waanze kuna moja iko chamaz kuna kinondon na kwingine ila ziko chache sana..mwanzo mzuri ila labda 10years baadae huko
Jinsi shule za serikal ubora wa elimu unavyopungua ndio hawa wa private wanavyolegea kwenye ubora