Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Mauaji haya yanayo tekelezwa na Israel kwenda kwa viongozi wa makundi hasimu yanayo washambulia na kuharibu mipango yao yanafanana na mauaji yaliyokuwa yakifanywa na serikali mbalimbali dhidi ya viongozi wa vyama vya kisiasa vya kikomunisti vilivyo kuwa na vikundi(jeshi la mapambano) dhidi ya utawala.
Namna Israel anavyo wawinda viongozi wa haya makundi lengo ni lile lile kuzima kabisa vugu vugu la mabadiliko wanayo tafuta makundi haya katika ukanda wa ule na ni vugu vugu la kisiasa zaidi[ utawala].
Israel inafanya kazi nzuri ya kupambana na makundi haya kwa ajili ya usalama wa taifa lake.
Pia naweza kusema inafanya kazi bure kwa sababu moja tu ni ngumu kupambana na watu walio na vugu vugu la kweli la mabadiliko ndani ya mioyo yao hapa nita chukulia mfano ule ule wa mwanzo wa wakomunisti pamoja ya kwamba serikali nyingi duniani ziliwakamata wakomunisti na viongozi wao na kuwafunga, watesa wanyonga na wengine kuuawa kikatili lakini wakomunisti waliendelea kuchaguana kisiasa katika mtiririko ule ule wa kawaida pasipo kuharibu mambo ndani vyama vyao na vikundi vyao na kuendeleza vugu vugu la mapambano serikali nyingi zilianguka.
Na mbaya zaidi wakomunisti walikuwa na imani kuwa njia pekee ya mabadiliko kwao ni kwa njia ya mtutu wa bunduki basi kupitia mapinduzi waliitumia hiyo njia kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa.
Kwa nini basi wakomunisti walikuwa wana pambana na serikali zao ni kwa sababu ilifika waliona itikadi ya ukomunisti inakuja kuondoa mfumo wa kinyonyaji na kuondoa matabaka na watu wote kuwa sawa.
Hii iliwapa hali ya wao kupambana toka moyoni pasipo kujali madhara gani yatakuja juu yao.
Sasa Israel anakutana na upinzani mkali kwanza Hamas[ hawa ni wapalestina walioamua kupambana na Israel leo wanaweza kuitwa Hamas usishangae kesho wakaitwa Gaza au west Bank ila itikadi inabaki moja kupambana na Israel] hivi ni vita vigumu kwa sababu unapigana na watu toka moyoni mwao walio amua kupigana na wewe kwa sababu walizo nazo wao ndani ya mioyo yao.
Kuua viongozi wao kwa watu wa namna hii ni kazi bure fikiri kiongozi wa Hamas aliyefariki alifiwa na karibu ndugu zake wote, je aliacha kupambana ? Hapana hao wapiganaji wa Hamas wamefiwa na ndugu na watoto wao na kwa sababu ya Israel je, wameacha kupambana ? Hapana. Unafikiri vizazi vyao haivitaacha kupambana ?
Sioni kuwa vifo vya viongozi wao ni vya kuwatia hofu kabisa wapiganaji wa makundi haya hawa watu wa namna hii wameshaona maiti za kila aina zilizo pasuka vipande vipande na za kutisha iwe za wapendwa wao ama ndugu zao sioni kuuawa kwa viongozi wao kwao itawafanya warudi nyuma au waachane na vugu vugu la mabadiliko wanalotafuta.
Anakufa kiongozi huyu anachaguliwa mwengine hii ni kazi ngumu bila kutatua au kumaliza kile kinachowafanya wao wawe na hilo vugu vugu la mabadiliko utakuwa unafanya kazi bure hii pia naiona kwa Israel upande mwengine anafanya kazi bure kupambana na makundi haya.