Nilipohoji kuhusu uvaaji wa mchungaji Tony Kapola kuna watu hususan wanawake walinivaa kwa ukali kwamba nina wivu niwaachie mchungaji wao, kwamba uvaaji wake ni wa kawaida, kwamba uvaaji wa kisasa kwa Watumishi wa Mungu sio tatizo. Binafsi niwaambie UTUMISHI WA MUNGU ni mgumu na unahitaji usiriaz kuliko wengi mnavyofikiri, Yohana alijinyima hadi kuvaa magunia na kula nzige jangwani mnafikiri utumishi ni mwepesi?
Tunarahisisha mno utumishi wa Mungu miaka hii ndio maana wahubiri nao wanahubiri injili mpya nyepesi ya kisasa iliyopakwa maneno matamu ya miujiza, utajiri na mafanikio, hawaihubiri ile injili pure ya Ufalme wa Mungu, ile ya kukemea dhambi kwa ukali wake.
Ndio maana tunaskia Watumishi wengine wanasema hata dukani sigara weka biashara sio ibada, wengine wanasema ndoa sikuiz sio mwili mmoja, wengine wameenda mbali na kusema pesa za majini sio haramu. Utumishi wa Mungu umeonekana ni simple tu hadi kina Irene Uwoya wanataka kufungua makanisa sasa huku bado miili imejaa tattoo.
Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi anahitaji Watumishi VIELELEZO KWAO WAAMINIO. Katika uvaaji, unenaji, utendaji na mwenendo mzima wa maisha kwa ujumla
Kwa Mungu hakuna usasa, sheria zake ni zile zile WAACHE DHAMBI NA KUNIABUBU
Mahubiri ya utajiri, pesa, miujiza na mahusiano yasitutoe kwenye mstari, Mungu sio mrahisi kama tunavyoaminishwa na Watumishi hawa wa kisasa
Tunapaswa kusali kwa imani, kutubu, kufunga na kuomba, Tunapaswa kumuogopa Mungu na kumuabudu kweli. Tunapaswa kuyaheshimu madhabahu yake. Tunapaswa kutambua Mungu ni mtakatifu hadhihakiwi wala kuchanganywa na aina yoyote ya uchafu
Nawasilisha.
Simfahamu huyo Tony.ila mahubiri ya utajirisho ndiyo yanayoharibu imani za wengi
Iko hiv naona hatari ya watu kuasi imani ya kikristo hapo baadaye kidogo.
mfano mtu umemwambia afunge atoe sadaka ili kuondoa laana sijui ya mababu inayosababisha asiwe na mafanikio.
huyu mtu akifanya hivyo mara mbili tatu halafu asione matokeo isipokuwa anaona wewe mchungajaji unabadilisha magari mapya kila siku, anageneralize wachungaji wote ni matapeli
Turudi kule kwenye injili za wazee wetu akina kulola,kuhubiri habari za uzima wa roho siyo wa mwili peke yake.
Finally,tusome bible kwa msaada wa Roho Mtakatifu.Ili hata kiongozi wako wa kiroho akiingia chaka/akipotosha unamwacha mwenyewe huko.Yaani imefika mahali huwezi tofautisha Ibada na sessions za akina Mauki(motivational speakers).
Principle Mhimu,ni hivi sadaka yoyote lazima Roho matakatifu atakuongoza,utatoa kwa kutanguliza kumpenda Mungu toka ndani mwako.Na si ya moja kwa moja kwamba kwamba ukitoa tu sadaka basi mambo yananyooka ,viko vigezo na masharti mengine mengi ambayo hayazungumzwi sababu haya vutii.mfano kuacha kabisa dhambi.Wengi wanasahau kwamba Mungu hashawishiwi na aina ya sadaka ili kukubariki
Wengi wanazungumzia sadaka wanakurudishaga agano la kale ,watakuelezea kuhusu Ibrahimu kumtoa isaka(kwamba mtoe isaka wako) .Wanachosahau ni kwamba Ibrahimu aliambiwa na Mungu mwenyewe.kwanini wao hawataki wewe usubiri maelekezo ya Mungu,kwamba utoe sadaka gani na uipeleke wapi.Ukitoa sadaka kwa lengo la kupata kitu huo ni mchango wako kwa ajili ya kumtunza huyo mhubiri jambo ambalo siyo kitu kibaya,ila siyo kusingizia eti Mungu kasema.kuna zile sadaka za kiutaratibu wa kimadhehebu,nyingi ya hizo ni michango tuu ya kutunza shughuli za kanisa ni mhimu kufanya hivyo ili huduma za kikanisa ziendelee.na kwa makanisa ya watu binafsi hizo hizo wazoita sadaka ni fedha tuu wanakusanya kwa ajili ya kuzitumia watakavyo.
Ndiyo maana wengi wa wahubili binafsi wameingia kwenye kitu kinaitwa "CuLT" sijui tafsiri yake hasa .ila hii ni aina ya ulaghai wa kuteka fikra za watu kwa ustadi mkubwa sana hasa wanawake na kuwaaminisha matokeo ya miujizi ilihali ni "FAKE".nadhani mmeshaona wahubiri wanawachapa waumini,wengine wanalishwa majani,wengine wanakaliwa na nabii na mambo ambayo kwa hali ya kawaida ni ya kushangaza.
Boton line,Mambo ya Mungu yanaenda Kwa "Akili na kwa Roho" ukiacha kimoja umeliwa