Mawakili wa CHADEMA waghairi kuwahoji Halima Mdee na Wenzake 18

Mawakili wa CHADEMA waghairi kuwahoji Halima Mdee na Wenzake 18

Mmh......

Hii habari ni ya kusikitisha na ya kusitua sana!

Inaelekea Kuna kitu kinachoendelea chini ya carpet
 
Weka maelezo sasa mbona ni Picha na Caption bila maelezo ya ziada???
 
Hii kesi imeisha, inafutwa kama sii leo ni kesho!. Keshokutwa Jumatano Chadema inatangaza kuwasamehe!.
Update....
Nani kakwambia watasamehewa? Lini COVID-19 waliomba msamaha?? Hayo ni mawazo yako na sio msimamo wa Chama.

Ninachokiona huko mbeleni kuna baadhi watajitoa kisha kurudi chamani kuomba msamaha. Hao wanaweza kusamehewa. Wale Vinara ndio basi tena watafute pakukimbilia au waanzishe Chama chao cha "Strong Ladies Party"
 
Hii kesi imeisha, inafutwa kama sii leo ni kesho!. Keshokutwa Jumatano Chadema inatangaza kuwasamehe!.
Update...
kwa hio habar ya twita uliyopokea inaizid habar ya kuongea direct? ulimsikia mbowe akiongelea hao covid 19 wapi?

Acha kupotosha nilikushauri siku moja kwamba kwa kuwa wewe ni wakili kawawakilishe mahakaman na sio kuleta notes za administrative law humu jf huku ukirejea remedies available for one aggrieved the the decision of administrative body(Certiorari, mandamus etc.).

Kama ulishindwa kuwawakilisha mahakaman humu sisi waelewa tunakuona ni mpiga porojo tu kama vijana wa uvccm buku saba ambao huwa nawajibu kulingana na uwezo wao na wao kujihis kuwa kila mtu hana uelewa kama wao..

So bottom line nakupa taarifa kuwa mawakili wa chadema walishakipta walichokuwa wanakihitaji subiri baada ya kesi kumalizika hukumu itakavyowanyoosha hao wabunge wenu fake.
 
Hata ulambaji wake asali anaufanya kwa umakini mkubwa hadi manyumbu yameshindwa kuelewa. Nipo palee ninaangalia huu mchezo.[emoji23]
Bora hata hao walamba asali kuliko muzarendo katili ambaye Kabudi na Biswalo wamesha mchoma kwa uporaji wake na wizi wa kishamba kisha kupeleka China.

Hii aibu itakapowekwa hadharani hata mama Jeska a aweza kuomba talaka kwa marehemu ili apate haki ya kukataa kutumia jina la mtu anayelaaniwa kila kona kwa uuaji na wizi kwa kutumia ushamba wa madaraka.

Nanyi Suku gang kadhaa mnaweza kujitundika
 
Huu mchezo hauitaji hasira, sema Mbowe anawauza sana wenzake.
Chama cha kwake na alipewa na Baba mkwe wake...maamuzi ni ya kwake na Baba mkwe wake,CDM ni bihashara kutoka huko Machame nyie wa huko kwingine anzisheni cha kwenu,Juzi nasikia wameingiziwa mgao wa RUZUKU mln 800+.
 
Bora hata hao walamba asali kuliko muzarendo katili ambaye Kabudi na Biswalo wamesha mchoma kwa uporaji wake na wizi wa kishamba kisha kupeleka China.
Hii aibu itakapowekwa hadharani hata mama Jeska a aweza kuomba talaka kwa marehemu ili apate haki ya kukataa kutumia jina la mtu anayelaaniwa kila kona kwa uuaji na wizi kwa kutumia ushamba wa madaraka.
Nanyi Suku gang kadhaa mnaweza kujitundika
😂😂😂 PK kabwaga manyanga!

Zitto Kabwe alisema hata yeye aliwahi kumjazia Fomu ya kuomba Ubunge Halima James Mdee wakati akiwa Chadema
 
Hizo ninaziona kama sarakasi bado kwakua ningumu kuusemea moyo wa mtu
 
Mawakili wa CHADEMA wameondoa nia ya kuwahoji maswali ya dodoso Halima Mdee, Ester Bulaya na Ester Matiko juu ya kiapo kinzani walichowasilisha katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam katika kesi waliyofungua kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama hicho.

Mbali ya hao, wabunge wengine katika shauri hilo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Nursat Hanje, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Esther Matiko, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Felister Njau, Agnesta lambart, Asia Mohamed, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Styella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza na Naghenjwa Kaboyoka.

Hatua hiyo imefikiwa leo mbele ya Jaji Cyprian Mkeha baada ya wakili wa CHADEMA, Hekima Mwasipo kuieleza Mahakama hiyo kuwa wameamua kufunga maswali hayo baada ya kutafakari kwa kina na kubaini kwamba hawana maswali ya ziada kwa Wabunge hao.

Shauri hilo namba 36/2022 leo liliitwa Mahakamani hapo kwa ajali ya Mbunge Jesca Kishoa kumalizia kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa Chadema kuhusu malalamiko yake ya kufukuzwa uanachama kinyume cha Sheria, lakini wakili Mwasipo akadai kuwa wamefunga kumuuliza maswali hayo.

Baada ya kuwasilisha ombi Hilo, Jaji Mkeha alikubali ombi la kufunga maswali ya dodoso, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 9,2023 ambapo wajumbe watakaoanza kuhojiwa ni Dk. Lwaitama na Ruth Molel baada ya Mdee na wenzako kutaka Wajumbe hao wa Bodi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA nao wahojiwe
 
Ila mnafanywa wajinga kila siku. Mliletewa lowassa kwa sababu ya ujinga wenu huohuo, bahati mbaya hampati akili

Huyo Lowassa amewahi kuwa waziri Mkuu wa serikali ya Tanzania, hivyo sisi wote ni wajinga kukubali Lowassa awe Waziri Mkuu. Halafu jaribu kuelewa siasa zilivyo usikarili.
 
Siasa Ni utapeli

March 8 mama Samia anakwenda kuwaombea msaamaha hao wabunge

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

Taratibu mmeingia kwenye mtego wa CHADEMA. Siasa za nchi hii kwa Sasa zinashikiliwa na CHADEMA. Huku Lema, huku kesi ya Covid 19, kule BAWACHA Mara Ruzuku. CHADEMA Wana strategist mzuri Sana, kayapanga mambo yakapangika.
 
CDM Ni matapeli bwaana Niki wa pili chapa Kaz mm na wew Sina bifu tuko pmj had mwisho tuone hili lichma linakwenda na maji walagahi wakubwa matapeli wakubwa

Blah blah za maridhiano wkt wananchi hawna maji,umeme ,afya duni mfumuko wa Bei alfu mijitu inakwenda kuwa sifia ccm ,wacha ccm itawale milelee shenzi zao na njaa zao wapuuz San CDM

Nani aliwalog lkn

Punguza hasira, muichague CCM na kujaza wabunge wote was CCM halafu uililie CHADEMA haileti maji na umeme?. Huo ni unafiki walilieni CCM wenye serikali na Bunge.
 
Maridhiano at work.

Kungekuwa na maridhiano akina Mdee wasingetaka kuhoji wadhamini wa CDM na wanafanya hivyo kununua muda zaidi ili hukumu isitoke mapema!

Akina Kibatala kufupisha dodoso ni mbaya kwa akina Mdee sababu sasa hukumu itatoka mapema na ndiyo maana wao sasa akina Mdee wanataka wadhamini CDM waje mahakamani!

Uamuzi wa kuondoa dodoso ni mzuri kwa CDM sababu ya hukumu itatolewa mapema
 
Back
Top Bottom