tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Ni muda mrefu sasa (yapata miezi 3) tangu kifungo cha JF kifike tamati lakini bado wahusika hawajaiachia 💯 %. Tukumbuke kuwa JF ilipigwa ban ya miezi 3 tangu September 2025 na hiyo ban ilipaswa kuwa lifted by December 2025.
Ndugu wanaJF, an attack to JF is an attack to all JF members. Ninatumaini sote tumesononeshwa na kuhudhunishwa na kitendo hiki cha JF kuendelea kufungiwa wakati muda wa kifungo umefika tamati. Kwa mujibu wa sheria, hii sio sawa. Huu ni zaidi ya ukandamizaji wa uhuru wa habari na kujieleza. Na tunaozuiwa kujieleza ni sisi wanaJF. Kitakwinu, inaonekana bado members wengi hawajarejea humu ndani, baada ya kukatishwa tamaa na muenendo wa watu wanaopaswa kuifungulia JF lakini bado wanaendelea anazuia upatikanaji wake kwa ufasaha nchini Tanzania. Sitaki kuwachosha kwa maneno mengi. Naomba niingie kwenye mapendekezo moja kwa moja ili tujadiliane jinsi tunavyoweza kujinasua kwenye mkwamo huu. Napendekeza wanaJF tufanye yafuatayo:
1. KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI
Ijapokuwa hatujuani, nina imani humu JF kuna baadhi ya members waliobobea kwenye musuala ya sheria. Kwanini mzee Pascal Mayalla na wansheria wenzako mliomo humu msiungane kufungua kesi ya kuitetea JF isiendelee kudhalilishwa, kubagazwa na kubanangwa na hawa "watu wasiojulikana"?
2. MCHANGO WA GHARAMA ZA KESI
Wahenga wanasema "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu". Ijapokuwa wengi wa members wa JF hatuna uwezo mkubwa wa kiuchumi, tukiamua kuungana tunaweza kufanya jambo. Kwa idadi ya members tuliomo humu, ikiwa kila mmoja atatoa angalau kima cha chini cha Tsh 2000 tu, bila shaka tutakusanya mamilioni ya shilingi ambazo zitatosha kabisa kuendesha kesi hadi ushindi upatikane. Tena hii kesi ni nyepesi sana, haitachukua muda mrefu kabala ya ushindi kupatikana.
Kipekee ninaumia kumuona mwanaJF mwenzetu, Tundu Lissu, yupo gerezani yapata mwaka sasa. Kama angekuwepo uraiani angekuwa aneishafungua kesi kuitetea JF. Hata hivyo hatuna haja kukata tamaa. Mawakili waliomo humu JF akina @Lugemalilla Nshalla mnaweza kufanya jambo kuikomboa JF kutoka kwenye makucha ya mkoloni mweusi.
3. KUHUDHURIA KESI
Pamoja na kuchangia fedha za gharama ya kesi, natoa wito kwa wanaJF mliopo Dar na ukanda wa Pwani muwe mnahudhuria mahakamani kwa wingi pindi kesi itakapoanza kuunguruma. Hii sio tu kwamba itasaidia kuongeza chachu na msukumo wa ushindi bali itasaidia kuongeza publicity ili dunia nzima ione jinsi haki zinavyokanyagwa hapo nchini Tanzania.
MAONI
Je, wanaF wengine mna maoni gani juu ya hili jambo? Ni njia gani nyingine ambazo tunaweza kutumia ili tufanikishe ukombozi haraka?
Karibuni kwa maoni na ushauri