Mawakili wa JF naomba tusaidiane kuikomboa JF

JF lipofungiwa Gerson Msigwa alipita katika media akieleza kwanini imefungiwa.
G.Msigwa anapaswa ku ueleza Umma kwanini imeendelea kufungiwa licha ya kumaliza kifungo.

Msigwa ni sehemu kubwa ya hili tatizo, aulizwe ni kwanini na kwa faida gani ya Umma!
 

Pasco.

JF inaweza shinda kesi dhidi ya serikali (TCRA), lakini je, amri ya mahakama itatekelezwa na serikali?

Ni kesi nyingi, serikali inashindwa na utekelezaji wake haufanyiki, au kuchukua muda sana au kukuza mgogoro husika kwa umafia.

Mbili, kesi ya Jamhuri vs JamiiForums inaweza, kwa makusudi kabisa ikacheleweshwa kwa miaka mingi, serikali ikatumia mwanya huo kutoifungua JF mpaka kesi ya msingi isikilizwe, tutajikuta tupo 2030.
Itakuwa ni upotevu wa muda na fedha, kushindana na dubwana ambalo limeiweka mahakama mfukoni.

Tatu, kwanini JF, isiendelee na utamaduni wake wa kutoshindana kwa uwazi na serikali? Sioni future ya JF, kama ikiingia "front" kupambana na watu kama akina Msigwa & Co.

Nawasilisha.
 
Wazonzuri sana hii platforms ni muhimu ila wasiiopenda mawazo mawazo
 
Kuna juhudi za kidiplomasia na kisheria zinaendelea
Sisi tumejikita hapo kwenye juhudi za kisheria mkuu. Ndio maana tumeanza mchakato wa kuanza kuchangishana gharama za kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…