Mawakili wa Mbowe waache maswali yasiyo na msingi, ulizeni maswali ya maana mteja wenu aachiwe haraka

Mawakili wa Mbowe waache maswali yasiyo na msingi, ulizeni maswali ya maana mteja wenu aachiwe haraka

Nadhani baadhi mmenisoma vibaya pamoja na kwamba nimeeleza mtazamo wangu kuhusu kesi hii ukoje. Angalia hata title ya uzi, nimetoa ushauri ili kesi iende haraka, Mbowe aachiwe huru mapema. Nikasema kwa uzito wa kesi, haiwezi kufutwa kwa sababu ndogo ndogo kama hizo za technicalities za ukamataji. Hii siyo kesi ya kuiba mayai.
Na Ndo unaelezwa pia kwamba kesi hushinda au kushindwa kwenye hizo hizo technicallities! Wanacho fanya kina Kibatala, ni kuonesha, kwa kupitia hizo minor technicalities, kuwa kesi ile ni batili, ya kutunga, yenye nia ovu ya kumuumiza Mwamba! Maswali yako ‘makubwa’ matatu hayana uzito kwenye wigo wa sheria! Mechi inapigwa kwenye details, small ‘magne’ of
Details ndugu yangu!
 
Watu wengi hawatakueleea ila kwa yale maswali tusubiri busara/maamuzi ya Jaji tu.
 
Wewe na mtoa mada hamna uwelewa wakutosha juu ya tasnia nzima ya sheria. Maswari yanayoulizwa sasa ni ya msingi sana juu ya case ndogo ndani ya case kubwa ya UGAIDI. Subiri wanaojua sheria wamalize then you can come up with your conclusion after the judgement.
Sio lazima tuone jambo sawa wote kwa angle flani kisa sijui ni sheria or blah blah
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.

Ningependa maswali yafuatayo yaulizwe, either ndani au nje ya mahakama.

1. Je, Serikali imewahi kumhukumu au kumtuhumu Mbowe kwa tukio lolote la ugaidi ambalo liliwahi kufanyika ndani au nje ya nchi?

2. Ni kawaida sana kuona vikundi vya kigaidi vikiwa na majina ya kujitambulisha. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, kikundi cha kigaidi anachodaiwa kuongoza Mbowe kinaitwaje?

3. Mbowe anajulikana zaidi nchini kama Mwanasiasa. Ugaidi kwa tafsiri ni lazima uwe na agenda fulani. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, nini ni agenda ya kundi ambalo analodaiwa kuongoza Mbowe?

Sitegemei kama upande wa Mashtaka umejiandaa kujibu maswali ya namna hii hasa kama yataulizwa mwanzoni kabisa wa kesi. Majibu ya haya maswali kutoka kwenye vinywa vya upande wa mashtaka yana implications kubwa sana baada ya kesi, whether Mbowe amefungwa au ameachiwa huru.

Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.
Unaharibu jukwaa kwa utopolo wako
 
Mkuu, usidhani sikuelewi au sijui unachokisema. Nadhani tofauti yetu ni mtazamo wa kwa nini kesi hii imefunguliwa in the first place. Kwa jinsi mawakili wanavyokalia maswali ya namna hii, ndiyo adhma ya serikali inapotimia, ambayo kwa upande wangu nadhani ni kumtoa tu Mbowe kwenye ulingo wa siasa kwa muda fulani. Hawana nia ya kumfunga Mbowe, hilo mimi naamini kabisa.

Waachane na preliminary examinations hizo, kama maswali ya msingi kama niliyosema hayawezi kuulizwa wakati huu, waipe pressure serikali na upande wa mashitaka kwa kuomba kesi iende kwenye trial na judgement haraka halafu wakayaulize haya maswali huko. Hilo litawavuruga zaidi maana nia ni kuipeleka kesi taratibu kwa jinsi inavyowezekana.
Wewe unadhani maswali mahakamani yanaulizwa kama bungeni eeeh?au kama aina flan ya mabishano ya kijiweni.Maswali yanaulizwa kutokana na vielelezo na aina ya ushahidi ulioletwa.
 
Mwishoni wakili wa serikali anauliza- watu uliowakamata wako hapa mahakamani
shahidi- Ndiyo
wakili wa serikali- unaweza kuwa tambua
shahidi- ndiyo
wakili wa serikali- nenda kamguse kila mtuhumia na kutaja jina lake
shahidi- anaenda na kuwagusa watuhumia wote kwa usahihi
Mawakili wasomi wasio na UTU wao wanahangaika na PGO na character assassination

sasa kaka kama PGO ambayo ndo mwongozo wao wa kazi halafu unasema kuwa sio ishu kama haikufatwa.. nini maana ya kuwa na miongozo na miiko kwenye utendeaji... maana yake unataka watu wafanye kazi kwa hisia zaid .. ukiruhusu watu wafabye kazi kwa hisia zaid ndo matokeo yake itakuwa vurugu.. daktari afate, hisia, mwalimu afate hisia.l, hakimu afate hisia, polisi afate hisia...kuna utendaji hapo?

sheria , miongozo na taratibu vimewekwa ili kumkumbusha mtu kuwa asifanye kaz kwa hisia au kishabiki.. mwongozo mkubwa zaid ni katiba then miongozo na taratibu zingine zinazaliwa kutokea humo

sasa kama unasema kuwa PGO sio ishu maana yake unasema Polisi anaweza akaja kwako na kufanya anachotaka sababu yeye ni Polisi

ni sawa ba Daktari asifate miiko ya utabibu akaamu kufanya matibabu kwa njia anayoona inafaa yeye...kisa yeye daktari

Its all about common sense tu.... kuwa kila kitu humu dunian kina miongozo.. kuanzia kwenye nature na uumbaji.. iwe unaamin Dini ama huamini Dini.. ila tambua chini ya jua kula kitu kiko kwenye utaratibu...

its a circle of life... ili kubalance mazingira na viumbe hai... ndo maana binadamu anazid kuharibu hii dunia kwa kutofata utaratibu ..

Kuna msemo unasema ukiona kwenye utendaji wa jambo lolote hakuko sawa basi jua kuna mtu katika hiyo chain nzima ya utendaji hajatimiza wajibu wake... Maana yake hajafata miongozo na taratibu zilizowekwa
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe...
Uchambuzi wa masuala ya mahakama tuachie sisi mawakili wasomi.Wewe endelea na uchambuzi wa mechi ya simba na yanga.

Kwa kifupi hii ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na shabaha ni kuangalia kama kanuni za utendaji kazi wa polisi zilifuatwa wakati watuhumia wanawekwa mbaroni.
 
Nawashauri mawakili wa Mbowe ambao mara zote wamekuwa wakisaka kiki za mitandaoni waache hizo.
Kesi ya Mbowe ni kubwa yenye kuhitaji weledi.
 
Hebu tuambie ni lipi walipaswa kufanya na hawajafanya?

Hebu tuambie wewe ungekuwa kwenye Hilo jopo mfano Leo ungemuuliza maswali gani shahidi wa leo?

Weka maswali yako hapa tulinganishe na walichosema mawakili leo?

Huwezi sema hawana weledi wakati hata wewe mwenyewe hujui.

Ili ufanye cross examination lazima ujue ni issue gani zinaharibu credibility ya ushahidi hivyo unatikiswa.

Lakini Kuna ushahidi unaoletwa kisheria Kama was Leo Kama usipofuata Sheria husika Haina maana yeyote.

Ni hayo mheshimiwa bush Lawyer
 
Nawashauri mawakili wa Mbowe ambao mara zote wamekuwa wakisaka kiki za mitandaoni waache hizo.
Kesi ya Mbowe ni kubwa yenye kuhitaji weledi.
Waache wafanye mbwembwe ili washindwe kesi. Si ndicho tunachotaka?

Maana Terrorism kuwa maswala ya utalii inafurahisha sana...
 
Hebu tuambie ni lipi walipaswa kufanya na hawajafanya?

Hebu tuambie wewe ungekuwa kwenye Hilo jopo mfano Leo ungemuuliza maswali gani shahidi wa leo?..
Sasa mtu anajiita jingaletu maswali ya weledi atayajulia wapi?

We ukitaka jibu zuri toka kwake muulize Meko alikuwa ananyoa naniliu mara ngapi kwa mwezi? Hayo ndo maswali ya weledi kwake
 
Nawashauri mawakili wa Mbowe ambao mara zote wamekuwa wakisaka kiki za mitandaoni waache hizo.
Kesi ya Mbowe ni kubwa yenye kuhitaji weledi.
Mashahidi wenu ni waongo chini ya kiapo!
Hawajui ukubwa wa tuhuma za ugaidi!

Inavyoonekana hii kesi itaamuliwa kwa vitu viwili: 1. Maagizo toka juu 2. Maslahi ya Jaji!
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.

Ningependa maswali yafuatayo yaulizwe, either ndani au nje ya mahakama.

1. Je, Serikali imewahi kumhukumu au kumtuhumu Mbowe kwa tukio lolote la ugaidi ambalo liliwahi kufanyika ndani au nje ya nchi?

2. Ni kawaida sana kuona vikundi vya kigaidi vikiwa na majina ya kujitambulisha. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, kikundi cha kigaidi anachodaiwa kuongoza Mbowe kinaitwaje?

3. Mbowe anajulikana zaidi nchini kama Mwanasiasa. Ugaidi kwa tafsiri ni lazima uwe na agenda fulani. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, nini ni agenda ya kundi ambalo analodaiwa kuongoza Mbowe?

Sitegemei kama upande wa Mashtaka umejiandaa kujibu maswali ya namna hii hasa kama yataulizwa mwanzoni kabisa wa kesi. Majibu ya haya maswali kutoka kwenye vinywa vya upande wa mashtaka yana implications kubwa sana baada ya kesi, whether Mbowe amefungwa au ameachiwa huru.

Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.
Wewe hata kukaa darasani kusoma sheria hujawahi, na zaidi ya yote, hata ile akili ya kawaida tu (common sense) huna. Utaanzia wapi kufundisha watu wanaoielewa vyema kazi yao! Wewe unadhani hapo mahakamani wanafanya siasa? Hata siasa yenyewe hujui!

Watu wengine ni Bure Kabisa!
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.

Ningependa maswali yafuatayo yaulizwe, either ndani au nje ya mahakama.

1. Je, Serikali imewahi kumhukumu au kumtuhumu Mbowe kwa tukio lolote la ugaidi ambalo liliwahi kufanyika ndani au nje ya nchi?

2. Ni kawaida sana kuona vikundi vya kigaidi vikiwa na majina ya kujitambulisha. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, kikundi cha kigaidi anachodaiwa kuongoza Mbowe kinaitwaje?

3. Mbowe anajulikana zaidi nchini kama Mwanasiasa. Ugaidi kwa tafsiri ni lazima uwe na agenda fulani. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, nini ni agenda ya kundi ambalo analodaiwa kuongoza Mbowe?

Sitegemei kama upande wa Mashtaka umejiandaa kujibu maswali ya namna hii hasa kama yataulizwa mwanzoni kabisa wa kesi. Majibu ya haya maswali kutoka kwenye vinywa vya upande wa mashtaka yana implications kubwa sana baada ya kesi, whether Mbowe amefungwa au ameachiwa huru.

Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.
Kijana hii kitu watu wamesomea huji tuu naviswali vyako vyakwenye kahawa.
Unajua maana ya "beyond no reasonable dought"
Kuthibitika kuwa uu mhalifu inatakiwa ushahidi usiache mashaka yoyote kimsingi!! Wafanyacho mawakili ni kuonesha mashaka yaliyomo kwenye kesi husika,nahiyo ndiyo hushindisha kesi!

  • unasema ulikutana na MTU muda ambao MTU huyo alikuwa jela unaacha mashaka.
  • alikupokea nagari Fulani wakati hiyogari alinyang'anywa inaacha mashaka makubwa.
  • unaposema uongo mahakamani wewe sio mwanaccm alafu umeshiriki nao kikamilifu na kuvaa nguo zao unachekesha.
Yapo mengi yamsingi wewe hujui sheria tuliza tu kiherehere utajifunza mengi.
Haki isiposhinda hatua hii itashinda hatua ijayo ya rufaa hii ikowazi
 
Lawyers are the smartest people. They can make u feel like a fool. Their minds run very fast. They can reason very quickly and come out with something... hata hawa mawakili wa serikali si kwamba ni wajinga hapana ni vile ni kesi ya kubumba inawawia vigumu. Hii field mtu ambaye hajielewi ataona ni maswali ya kijinga lakini kimsingi wenye utimamu wanaelewa vyema

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom