Kumuondoa Jaji ndio kuna hatua za kufuata mpaka kuunda Tribunal Board ifuate mchakato wote ila kumuondoa Jaji Mkuu hakuna mchakato wowote wa kufuata. Ibara ya 118 ya Katiba iweka wazi hapo.
Hata hivyo ibara ya 110 ya katiba yetu bado inatoa madaraka makubwa kwa Rais kuamua kumuacha kazini au kumfuta kazi,
Katiba yenyewe pia haimlazimishi Rais kuunda time ya kijaji, inasema "akiona inafaa" na hakuna wa kumuuliza, Sasa hapa utaona madaraka makubwa ya Rais katika kuamua Hilo! Ndio Mana katiba mpya Ni muhimu kumpunguzia Rais haya madaraka, ikitokea Judge Ni swahiba wake aweza kuamua kukaa kimya tu!