Hivi watu wa usalama wa taifa huwa wanakuwa wapi mpaka tuhuma kama hizi kubwa zinapotokea katika ofisi nyeti za umma!? Hivi sheria iliyopelekea kuamzishwa kwa TISS, na uwepo wao katika kila idara nyeti ya serikali inatusaidia nini kama Taifa endapo kama karibu katika kila sehemu nyeti kuna upigaji, rushwa, ubadhirifu na ufisadi wa kutisha!?
Waziri mwenye dhamana ya utawala bora, Je! Uwepo wa ofisi yake yenye utitiri mkubwa wa wafanyazi ambao wapo chini yake, wenye dhamana kubwa ya kuwa "watching dogs" kwa rasirimali za nchi, hivi huwa wanakuwa wapi pale uozo wa kutisha unapotokea na kuliingiza taifa katika hasara kubwa!?
Kibaya zaidi habari za ubadhirifu huwa zinakuja na kuanza kufahamika kwa umma zikiwa zimechelewa sana, lakini jambo la kushangaza ni kwamba, hata zikiwekwa wazi viongozi wenye dhamana ya nidhamu kwa wahusika nao huanza kulalamika tu badala ya kuwachukulia hatua stahiki za kinidhamu. Kuna kila haja ya kujenga taasisi imara ya urais, ambayo inawajibika na haisiti kuchukua hatua stahiki kwa wanadhirifu, kuliko kuishia kutumbua, kuhamisha na kulalamika.
Inaudhi sana kusikia sijui mara zipo familia 12 ambazo hazigusiki, ambazo shughuli zao za kilimo zinaleta athari kubwa katika mabonde ya Usangu na Ruaha Kuu. Mara utasikia watu fulani wakiguswa nchi itatikisika, mara kiongozi fulani wa juu anahusika katika kashfa fulani, n.k.