Mawakili wamkataa Jaji Biswalo, wamuandikia barua Rais Samia

Kwanini aitwe mheshimiwa kwa tabia hizo alizoonyesha?
Kama uheshimiwa ndiyo huo basi hii nchi imebaki mifupa
Niliwaza hilo hilo pia. Kwa vile anatuhumiwa wizi akiwa na tai shingoni basi anaitwa mheshimiwa. Kina John na Juma wanaopora wanaitwa majangili.

Ifikia wakati mijizi yote itambulike kwa sifa zao husika. Haya mambo ya kuitana mheshimiwa huku ni mijambazi ni ujinga tu.
 
Hadi mahakama imuite mhalifu ndo Neno Mheshimiwa litaondolewa.
 
Kesi ya tumbili inenda kwa nyani unategemea nini?
 
Kwa hiyo bado Rais ana uwezo wa kumuondoa jaji bila 'tribunal board' akiona inafaa ?...
Umeenda kusoma au umekurupuka?
Aisee kazi tunayo Tena kubwa sana
Kasome ibara 110 ibara ndogo ya 6 na ya 7 kwa pamoja na ibara ya 120 ibara ndogo ya 5 mbona mnakuwa wazito hivi enyi watu? Kuundwa kwa hiyo tribunal board kunategemea na utashi wa Rais .
halazimishwi na katiba Wala mtu yeyote.
ndio maana katiba ikasema "rais akiona inafaa"

Nimebold ili angalau wewe na wenzio muelewe, acces katiba soma hizo ibaraka katika katiba halafu uje!
 
Hivi tofauti ya lawyer na advocate ni ipi? Je, anayekuwa na muhuri ni lawyer au advocate?
Maswali mengine ujiongeze hata huko mtandaoni!
Mtu yeyote aliyesoma Sheria Ni lawyer au mwanasheria na anatoa msaada tu wa kisheria wakati advocate Ni mwanasheria au lawyer ambaye ameidhinishwa kufanya kazi za kisheria mahakamani Kama uwakili nakadhalika! Mfano ukimaliza chuo kikuu pale mlimani Sheria wewe Ni mwanasheria Ila ukienda kusoma pale school of law ukimaliza tutakuita advocate! Au wakili


The difference between an advocate and a lawyer is that the advocate is a licensed professional who has the right to practice law. Lawyers can only provide legal assistance to clients, while attorneys can represent clients in court. Generally speaking, anyone who has a legal education is considered to be a lawyer.27
 
Bibi amelikoroga, kama alikuwa anaongea tu kuchangamsha genge bila concrete evidence hapo ndio itajulikana. By the way, ina maana kweli Rais hakuona umuhimu wa kutengua uteuzi wake mpaka afundishwe na mawakili?.
Sidhani kama ni rahisi kutengua kama kumtoa DC Kwa nafasi ya Jaji.........
 
Nashauri hiyo tume ya Haki Jinai iliyo teuliwa na Mh. Rais ichunguze pia tuhuma nzito zinazo elekezwa kwa huyu Jaji kwani tuhuma dhidi yake ni nzito na kamwe hazifai kupuuziwa kwani zina haribu taswira ya mahakama kwa kiasi kikubwa sana.

Lakini pia ni wakati muafaka wa Tume hiyo ya Haki Jinai kuchunguza taratibu nzima za upendekezwaji wa majina ya Majaji ili kuepuka kuteua Majaji wasio wadilifu wenye kashfa nzito, huyo ni mmoja tu hatujui kama kweli wengine ni waadilifu kwa viwango vinavyo kubalika
. inaonekana wazi kuna tatizo kubwa sana tena sana.
 
Inashangaza sana yaaan kuna miaka flani wakati mikate imeadimika nchini wakati huo raisi ni Nyerere alimpigia simu usiku kumuuliza mkurugenzi wa Usalama tatzo nini. Lkn kwa sasa TISS kama vile hawaoni nahisi kuna haja ya kufanyia marekebisho ili wajione nao wana wajibu wa kuzuia pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…