Mawaziri akiwemo Waziri Mkuu, wanalipwa perdiem wawapo Bungeni kwa kigezo gani ili hali wanakaa katika nyumba za Serikali Dodoma?

Alafu huku wale wa Sensa wanaambiwa wajitolee ni uzalendo😅
Hii nchi hii
Baadhi ya watu sijui watamuambia nini Mungu siku ya kiama
Ukichunguza utaona kwamba hiyo bajeti ya serikali aslimia 70 ni matumizi ya rais, wabunge, mawaziri na spika na naibu spika halafu mfanyakazi anaengezewa mshahara 12000 ni unafiki mtupu tena ni baada ya miaka 6 bila ongezeko lolote juzi tu pia wameogezeana maposho ya safari ambazo kabisa hazimnufaishi mtumishi wa kawaida halafu waziri mkuu anaongea uongo kabisa eti mawaziri wameonezewa aslimia ndogo na wamekaa kimnya anategemea waseme nini na kila kitu wanalipiwa na serikali kuanzia usafiri wao na familia zao, kula, kulala, matibabu india tena wanaongozana na familia zao, masikini ukiumwa ujilipie au ujitangaze kwenye vyombo vya habari uchangiwe tulikuwa na matumaini na hii serikali lakini ndo yale yale lazima tuungane tupige kelele.
 
Perdiem ndo nini??
 
Kuna watumishi wa umma wenye mshahara mathalani milioni 1.5, hawa nao wameambiwa wana mshahara mkubwa kwa hiyo nyongeza wanayostahili ni elf 20. Kama mil. 1.5 inawekwa kwenye category ya mshahara mkubwa basi hii nchi imeshatopea kwenye ufukara wa kutisha.......mimi nikadhani mishahara mikubwa ni ile inayoanzia mil. 15 hadi mil. 40 ambayo mingine ndo walikuwa wanajilipa kule NHC, kumbe na hizi mil. 1.5 hadi mil. 4 na yenyewe inaitwa mishahara mikubwa......basi twafwaaa........waacheni wajilipe night pasipo kusafiri nje ya kituo cha kazi maana wao mishahara yao ni midogo sana kuliko ile ya watumishi wa umma.
 
Eti waziri mkuu unaulizwa wewe ni mzalendo? Kama ndio je unauhalali wa kulipwa padem wakati upo hapohapo kwako ?;Au unalala ndani ya bunge?
 
Mkuu, uko sahihi kabisa. Perdiem I atakuwa kulipa ukiwa nje ya kituo chako cha kazi. Waziri Mkuu, mawaziri na Spika Kituo chao cha kazi ni Dodoma. Kwa maoni yangu hawastahili kulipwa.

Pia huu mtindo wa kulipa a sitting allowance kwa kufanya kazi unayolipwa mshahara nao ni ufujaji wa mali za umma. Na hili nafikiri linafanyika Tanzania tu.
 
KATIBA MPYA
 
Hii nchi ina unafiki mwingi sana, Heche Kwa nini hahoji mishahara na marupurupu ya wabunge anarukia Kwa Waziri Mkuu?
 
Tupambanie KATIBA mpya.

Mzee Warioba ateuliwe na AAPISHWE kuwa mkt wa Tume amalizie KAZI aliyoianza. Kikosi KAZI wakae benchi.

Wanasiasa walipwe kiduchu Ili kuzuia wimbi la Wataalamu kukimbilia Vyeo vya kisiasa,

Mawaziri wasitokane na wabunge.

Wazalendo pekee ndo wagombee. Ameeeen
 
Si hayumo humo lazima aongee, wakiingia mule wanasahau ya huku nje
 
Wizi Kama kawaida
 
Ndio maana tunatozwa tozo za hovyo kabisa ili wao na familia zao wajineemeshe
 
340,000 kwa siku??
My, my, my......
Wakati Mimi juzi nilipandishwa mshahara wa mwezi kutoka 950,000 Hadi 990,000 na masimango kibao eti nimeongezewa asilimia 23.
Hivi MTU unaweza ku spend 340,000 kwa siku? Utakula nini?
Juzi Kati nikitoka out na familia ya watu 4 tulibeba 50,000. Tulijichana nyama pale kibaha Nida na chenji ya daladala ilibaki.
How do you spend 340,000 in 24 hours????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…