Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Ni sawa na Masters ya Aloyce Kwezi hapo Tumaini Iringa. Alikuwa anasoma jioni. Jamaa hawezi hata kuongea na kuandika jina lake anapewa na A tu. Maisha haya.
 
Wapo watu kazi yao kuandikia watu. India,Kenya,Nigeria ndio usiseme

Sasa kama unaweza kumlipa mtu hadi m5 akuandikie PhD thesis utashindwa kutoa m2 ili uandikiwe machapisho mawili tu? Mbona kazi rahisi sana hiyo!?
 

Tanzania hata nchi kama Nigeria zina watu waliosoma kweli na ni wana taaluma wenye skills za hali ya juu. Utawatambua vizuri ukikutana nao kwenye mashirika ya kimataifa (intergovernmental) au ya sekta binafsi au hata katika serikali za nchi kubwa kama US. Wasomi wazuri wapo hata hapa nchini: serikalini, kwenye mashirika ya umma na sekta binafsi. Lakini hawatambuliwi kirahisi.

Tatizo, serikalini wasomi wa kweli hawathaminiwi wala hawatakiwi katika uongozi. Wanaopewa fursa ni watu wenye janja janja za kisiasa, bootlickers, waimba sifa kwa viongozi na walio tayari kutumikishwa na viongozi kwa lolote. Na ukiwa kiongozi na una pesa unaweza kujipatia degree yoyote ya chuoni hata bila kusoma almuradi unaihitaji kwa mikogo tu. You don’t need the professional skills.

Enzi zile tulikuwa tunasoma kweli ukijua kuna mashindano makali ukitafuta kazi ya maana hasa nje ya nchi. Kupasi mtihani peke yake haikutosha kama kuna vitu hukuvimaster vizuri. Lazima uwe vizuri sana kwenye kupresent na kuelezea skills zako na thamani utakayoongeza kitaaluma ukipewa kazi hiyo. PhD haikuwa qualification ya kawaida kwa kila mtu: ilikuwa zaidi ni kwa academicians (lecturers) na researchers. Wachache sana walikuwa wanaitafuta. Inachukua miaka 3 (full time) hadi 6 (part time) hata huko nje. Na wengi walikuwa wanakwama kufikia vigezo vyake.

Sasa siku hizi mtu ana ajira kubwa na pesa ya mama tayari ndio anaanza kusoma ili apate title tu. Imefanya watu wengi kutoelewa thamani ya elimu nchini. Wanaona degrees hazina maana kwa sababu nchi haithamini input ya wasomi. Eti kiongozi bora hakai ofisini - kuangalia makaratasi!; yuko site muda wote anafuatilia kazi!

Ikija kwenye mambo ya utaalamu inabidi mtegemee wataalamu wa nje, software za nje, hata usimamizi wa miradi toka nje. Netgroup Solutions waliletwa kuisimamia TANESCO na kukusanya madeni yake yote kisha wakakatiwa mabilioni yao na kutoweka! Ndio Tanzania hiyo inayotaka maendeleo.
 
Nina rafiki Prof at Mzumbe UDSM wing.... a very close friend anafanya hayo..... watoto wetu can not write a thesis nakwambia. Nina mifano hai sana ni hivyo hatupashi kujuana humu ningelikutajia.. i vizuri mama D

Namfahamu huyo jamaa hata miaka ile ya mwanzoni mwa 2000 alikuwa analipwa kilo sita kwa dissertation moja kwa mujibu wa hao aliokuwa anawaandikia. Sisi akina pangu pakavu tia mchuzi tulikomaa wenyewe tukamaliza.
 
Mtu anayeamini katika kujifukiza anapewaje phd
 
Ph.D. siyo cheti boss! Anapoongea, hiyo Ph.D unaina au ni yule yule Jaffo wa NGO?
 

Hawana vigezo vya kuwa Rais au Waziri Mkuu wa Tanzania. Bila shaka unavijua. Kuanzia, kigezo cha usomi hakipo.
 
Kupublish paper kwenye reputable journals hata sio kazi kivile tusitishane🐒
 
Rubbish
 
Wewe baba mzima ungekua unajua kitu usingekua hapa kuponda PhD ya mwanaume mwenzio

Ndio ushafeli hivyo😂😂😂😂

Halafu nitakualika usiku wa vyombo maana unayaweza kweli mwenzangu
Umenifurahisha Wallahi, maana hawa dharau kwa wenzao hawajambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…