Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Hivi hawa maprof wa bongo wana lakuhoji kwa mawaziri?

Nenda Mzumbe ya Dar uone vilaza kabisa wanaokota masters.

Kuna mtumishi mwenzangu ofisi ya zamani alipewa title ya research na the so called Mwaijande. Hajui hata "research gap" ni nini ila nasikitika kukuambia anagraduate mwaka huu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni sawa na Masters ya Aloyce Kwezi hapo Tumaini Iringa. Alikuwa anasoma jioni. Jamaa hawezi hata kuongea na kuandika jina lake anapewa na A tu. Maisha haya.
 
Wapo watu kazi yao kuandikia watu. India,Kenya,Nigeria ndio usiseme

Watu mnajua kuongea aisee, Kigezo cha kwanza kupata PhD lazima upublish paper/s kwenye journal inayotambulika duniani, Na kuna vyuo vingine hawakupi hiyo PhD mpaka upublish papers kuanzia 2 na kuendelea!! Sasa hiyo shughuli ya kupublish hizo papers kwenye reputable journals usimuliwe tu na watu, siyo ya kitoto, sidhani kama kuna mtu anaweza kukufanyia hilo kirahisi namna hiyo! Vyuo serious havina mpango na thesis report, huwa wanaichukulia kama formalities tu, mambo yote ni publications
Sasa kama unaweza kumlipa mtu hadi m5 akuandikie PhD thesis utashindwa kutoa m2 ili uandikiwe machapisho mawili tu? Mbona kazi rahisi sana hiyo!?
 
Kwa Tanzania au Africa PHD au proffesor ni title tu lakini hazinaga msaada kwenye ground..... muulize sasa PHD yake ina msaada gani kwenye jamii yake au nini amefanya kupitia elimu yake na kuisaidia nchi zaidi ya kuwa na kadi ya CCM...

Binafsi naona bora hata tuwe na viongozi masela au wenye elimu ya degree kuanzia second class kwenda chini....hawa wengi halafu ukakuta masela huwa wako real, wengi waliosoma vizuri hapa Tanzania huishia kuwa wapumbavu tu..

Tanzania hata nchi kama Nigeria zina watu waliosoma kweli na ni wana taaluma wenye skills za hali ya juu. Utawatambua vizuri ukikutana nao kwenye mashirika ya kimataifa (intergovernmental) au ya sekta binafsi au hata katika serikali za nchi kubwa kama US. Wasomi wazuri wapo hata hapa nchini: serikalini, kwenye mashirika ya umma na sekta binafsi. Lakini hawatambuliwi kirahisi.

Tatizo, serikalini wasomi wa kweli hawathaminiwi wala hawatakiwi katika uongozi. Wanaopewa fursa ni watu wenye janja janja za kisiasa, bootlickers, waimba sifa kwa viongozi na walio tayari kutumikishwa na viongozi kwa lolote. Na ukiwa kiongozi na una pesa unaweza kujipatia degree yoyote ya chuoni hata bila kusoma almuradi unaihitaji kwa mikogo tu. You don’t need the professional skills.

Enzi zile tulikuwa tunasoma kweli ukijua kuna mashindano makali ukitafuta kazi ya maana hasa nje ya nchi. Kupasi mtihani peke yake haikutosha kama kuna vitu hukuvimaster vizuri. Lazima uwe vizuri sana kwenye kupresent na kuelezea skills zako na thamani utakayoongeza kitaaluma ukipewa kazi hiyo. PhD haikuwa qualification ya kawaida kwa kila mtu: ilikuwa zaidi ni kwa academicians (lecturers) na researchers. Wachache sana walikuwa wanaitafuta. Inachukua miaka 3 (full time) hadi 6 (part time) hata huko nje. Na wengi walikuwa wanakwama kufikia vigezo vyake.

Sasa siku hizi mtu ana ajira kubwa na pesa ya mama tayari ndio anaanza kusoma ili apate title tu. Imefanya watu wengi kutoelewa thamani ya elimu nchini. Wanaona degrees hazina maana kwa sababu nchi haithamini input ya wasomi. Eti kiongozi bora hakai ofisini - kuangalia makaratasi!; yuko site muda wote anafuatilia kazi!

Ikija kwenye mambo ya utaalamu inabidi mtegemee wataalamu wa nje, software za nje, hata usimamizi wa miradi toka nje. Netgroup Solutions waliletwa kuisimamia TANESCO na kukusanya madeni yake yote kisha wakakatiwa mabilioni yao na kutoweka! Ndio Tanzania hiyo inayotaka maendeleo.
 
Nina rafiki Prof at Mzumbe UDSM wing.... a very close friend anafanya hayo..... watoto wetu can not write a thesis nakwambia. Nina mifano hai sana ni hivyo hatupashi kujuana humu ningelikutajia.. i vizuri mama D

Namfahamu huyo jamaa hata miaka ile ya mwanzoni mwa 2000 alikuwa analipwa kilo sita kwa dissertation moja kwa mujibu wa hao aliokuwa anawaandikia. Sisi akina pangu pakavu tia mchuzi tulikomaa wenyewe tukamaliza.
 
Mtu anayeamini katika kujifukiza anapewaje phd
Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.

Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.

Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.

Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.

Hongera sana Selemani Jafo, PhD.
 
Ph.D. siyo cheti boss! Anapoongea, hiyo Ph.D unaina au ni yule yule Jaffo wa NGO?
 
Mwingine

Screenshot_2021-11-26-12-26-00-477_com.facebook.katana.jpg
 
Kawashangae na kuwadharau wahaya,wachaga na wanyakyusa wasomi wa kufa mtu ambao wanaongea kiingereza kilichonyooka ambacho hata malkia wa uingereza anawapigia makofi kwa usomi na kiingereza kizuri lakini hawajawahi toa Raisi Wala waziri mkuu na usomi wao toka Tanzania ipate Uhuru miaka 60 iliyopita

Hawana vigezo vya kuwa Rais au Waziri Mkuu wa Tanzania. Bila shaka unavijua. Kuanzia, kigezo cha usomi hakipo.
 
Watu mnajua kuongea aisee, Kigezo cha kwanza kupata PhD lazima upublish paper/s kwenye journal inayotambulika duniani, Na kuna vyuo vingine hawakupi hiyo PhD mpaka upublish papers kuanzia 2 na kuendelea!! Sasa hiyo shughuli ya kupublish hizo papers kwenye reputable journals usimuliwe tu na watu, siyo ya kitoto, sidhani kama kuna mtu anaweza kukufanyia hilo kirahisi namna hiyo! Vyuo serious havina mpango na thesis report, huwa wanaichukulia kama formalities tu, mambo yote ni publications
Kupublish paper kwenye reputable journals hata sio kazi kivile tusitishane🐒
 
Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.

Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.

Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.

Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.

Hongera sana Selemani Jafo, PhD.
Rubbish
 
Wewe baba mzima ungekua unajua kitu usingekua hapa kuponda PhD ya mwanaume mwenzio

Ndio ushafeli hivyo😂😂😂😂

Halafu nitakualika usiku wa vyombo maana unayaweza kweli mwenzangu
Umenifurahisha Wallahi, maana hawa dharau kwa wenzao hawajambo!
 
Back
Top Bottom