Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

jafo kipindi cha mwendazake, kuna mzee alimbananisha arudishe pesa za ujenzi alikuwa ni mkandarasi

wakati anamhoji mzee kajitupa chini kazirai, sema alichoharibu yule mzee alipeleka mikono mfukoni huku kazimia,

jafo nae kashtuka ,kakomaa nae tuu mzee amka bhana, rudisha pesa. Akatoa agizo huyu mzee akiamka mumkamate aeleze ni wapi amepeleka pesa.
 
Mwambie huyo jamaa...hajui na ni mbishi hatari...huyo hata masters hana...nimemjibu hat haelewi maskini ya Mungu ubishi tu wa wabongo hat kama kitu hajui.
Wewe mwenye masters mbona unaonekana ngumbaru tu hapa!
Yaani hivyo vitu vichache ulivyokariri unaamini ndio kila kitu, umeshamaliza elimu yote iliyoko ulimwenguni? Umejifungia kwenye kashimo kako hako unajiona mjanja sana!
 
Which Management is mediating?
 
Niliposoma maelezo haya, nimeamini akili haikutoshi au una matatizo ya ufahamu. Unaamini kabisa UDOM ina maprofesa ambao ni wakubwa sana, wanajua sana hawawezi kutoa digrii za kishenzi, ni wataalamu sana! Huijui UDOM na hujui elimu ya vyuo vikuu na hujui elimu za wanasiasa.
 
tumemlipa sasa Phd yake kupitia Dk Msukuma...mwingine akipata Phd nasisi tunampeleka Kibajaji....mkiongeza Kishimba naye anakula Phd ...mkizingua tena Mbowe naye anakula Phd..
 
Kwa kusema hayo kuhusu chuo chetu cha UDOM unataka kutuaminisha nini? Kwamba wale madaktari waliohitimu UDOM na sasa wanahudumu katika mahospitali nchi nzima hawafai? Hujafa hujaumbika ndugu, utakabwa na mfupa wa samaki au utapata ajali ya bodaboda uvunjike kidevu ukakutane na madaktari kutoka UDOM halafu tuone kama utaendeleza matusi yako. Unamaanisha wale waalimu waliohitimu UDOM na sasa wanafundisha katika mashule nchi nzima, ya serikali na ya binafsi, unatuambia hao hawafai? kwani wanao wanasoma wapi mwenzetu, au bado kinda hujapata familia? Unataka kutuambia wale wanasheria waliohitimu UDOM na sasa wanahudumu katika mahakama zetu kama mawakili, waendesha mashitaka na mahakimu, kwamba ni wa hovyo? Utapata kesi hivi karibuni ukakutane nao. Usijiamini sana, hujui kesho yako. Acha dharau.
 
Usiombee watu mabaya ili umuhimu wako uonekane. Wengine tunaona ubaya na udhaifu wako kila siku! Jilani yangu hapa kijijini anatibu magonjwa sugu na hajawahi kupitia UDOM yako.
 
Basi Sawa!2025 atakuwa lecture huku Kisarawe tunakwenda na Mpendu.By wa Ukae.
 
Usiombee watu mabaya ili umuhimu wako uonekane. Wengine tunaona ubaya na udhaifu wako kila siku! Jilani yangu hapa kijijini anatibu magonjwa sugu na hajawahi kupitia UDOM yako.
Usifananishe sangoma na wataalamu waliohakikiwa
 
Mawaziri wawili wa Tanzania, ni miongoni mwa wahitimu 42 waliotunikiwa shahada ya udaktari wa Falsafa (Phd) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Mawaziri hao ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Selemani Jafo ambaye ni Waziri katika Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira.

Wawili hao wametunikiwa shahada hizo katika mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga leo Alhamis Desemba 16, 2021.

Wametunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho, Dk stergomena Tax. Kiongozi mwingine aliyetunikiwa shahada ya uzamivu ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde ambaye ametunikiwa shahada ya uzamivu ya umahiri ya mahusiano ya kimataifa.

Awali, Dk Stergomena alisimikwa kuwa mkuu wa chuo hicho baada ya kuteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan Juni, mwaka huu, baada ya aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Balozi John Kijazi kufariki dunia Februari, mwaka huu.

Hongera sana mawaziri najua haikuwa rahisi
Pamoja na majukumu yenu mazito ya uwaziri lakini mmeweza kuhitimu masomo yenu
 
Hongera sana mawaziri wetu najua haikuwa rahisi
Pamoja na majukumu yenu mazito ya uwaziri lakini mmeweza kuhitimu masomo yenu
 
PhD za mchongo zimekuwa nyingi sana.

Tukiwaambia waonyeshe thesis zao utakuta ni zakubumba bumba tu wala hazina impact yoyote hapa nchini hata kwa ngazi ya kijiji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…