Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Ligazeti lote hili kumbe unamtetea mvamia nyumba za watu kama wewe [emoji23]

Ulivyokosa haya mtu mzima wewe unajisifia kabisa ulienda kwa Watu wana chumba na Ukumbi wakakupisha hukujua walienda kulala wapi, unajua jinsi gani walisononeka kuacha kitanda chao na kwenda kulala pasipojulikana???

Kama wewe muungwana mbona hukuwaambia ulale hapo ukumbini au mbona hukulipia lodge???

Mitabia yako ya kishenzi unaileta hadi kwa familia za watu eti diplomasia, diplomasia ni kwenda kuwabana watu katika nyumba zao???

Yaani imekuuma huyo Mvamizi mwenzio kulazwa Lodge kuliko kufikiria Usalama wa Mtoto wa miaka mitano!!,

Mjirekebishe, Dunia imebadilika kama una mishe zako tafuta lodge kabisa, huko kwa ndugu waenda kusalimia tu na kuondoka, mishe zako zisiwape wengine heka heka za nafsi.
 
Ulivyokosa haya mtu mzima wewe unajisifia kabisa ulienda kwa Watu wana chumba na Ukumbi wakakupisha hukujua walienda kulala wapi, unajua jinsi gani walisononeka kuacha kitanda chao na kwenda kulala pasipojulikana??
Watasononeka watu kama nyie mliolelewa kwwnye roho mbaya bila shaka.kulala siku moja kwa mtu aliyestaarabika sio ishu.
Kama wewe muungwana mbona hukuwaambia ulale hapo ukumbini au mbona hukulipia lodge???
Wao ndio walianza kuonesha uungwana kwangu.
Mitabia yako ya kishenzi unaileta hadi kwa familia za watu eti diplomasia, diplomasia ni kwenda kuwabana watu katika nyumba zao???
Ni roho mbaya tu hakuna nyumba wala nini,sisi tuliokulia kwenye familia zenye upendo tunajua thamani ya mgeni
Mjirekebishe, Dunia imebadilika kama una mishe zako tafuta lodge kabisa,
Huu upuuzi sifanyi,nitafikia kwa ndugu wenye upendo na nitaachiwa chumba nilale peke yangu,huu ndio ustaarabu.

Kwanza huweI kumlaza mgeni na mtoto mdogo awe wa kike au kiume,mtu mzima atalala na mtu mzima mwenzakw wa jinsia moja.
huko kwa ndugu waenda kusalimia tu na kuondoka
Ningekuwa na ndugu mwenye roho ngumu kama wewe ndio ningekuwa naenda kusalimia na kuondoka,pengine hata kuja kwako nisingekuja maana usingenipa hata huo ugali ungelionna nimekumalizia bajeti.
mishe zako zisiwape wengine heka heka za nafsi.
Nyie nndio mnamnyima mgeni chakula kwa kisingizio hakutoa taarifa,mnadhani kama taarifa yake inakuja na chakula.
 
Yaani mimi hata kumlaza na mwanangu wa kiume naogopa sembuse huyo wa kike!!! Akalale Lodge tu huyo mgeni. Dunia imeharibika mno.
 
Mpeleke Lodge af alipe mwenyew, mtu unaendaje kwa mtu mwingine bila taarifa mbaya zaid kulala[emoji850]

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Sheria katika vitabu vyote duniani hairuhusu
 
Kwani hamna sebule alale ili next time ajiongeze? Ila kuna watu ni wazito kweli wa kufikiri.
 
Uko sahihi sana,ila dah kumbe tuko wengi,mtoto kike anauma aisee,yani we acha tu...
 
Umetembelea mtu ana chumba na sebule

Umelala chumbani comfortable na usingizi umepata.....


Hujui hata wenye nyumba wamelala wapi?

Una shida wewe!!
 
Umetembelea mtu ana chumba na sebule

Umelala chumbani comfortable na usingizi umepata.....


Hujui hata wenye nyumba wamelala wapi?

Una shida wewe!!
Hayo ndio maisha tuliyolelewa sisi.

Mgeni akija anakaa siku moja unampisha wewe utalala hata ukumbini lakini mgeni astarehe vizuri.

Nyie wageni wakija ndio mnawatesa,malezi ya ajabu haya
 
Ajabu ni mtu mzima unapotoa miguu yako kwa mtu mwenye chumba na sebule........

Miaka hii


Hayo ndio maisha tuliyolelewa sisi.

Mgeni akija anakaa siku moja unampisha wewe utalala hata ukumbini lakini mgeni astarehe vizuri.

Nyie wageni wakija ndio mnawatesa,malezi ya ajabu haya
 
Ajabu ni mtu mzima unapotoa miguu yako kwa mtu mwenye chumba na sebule........

Miaka hii
Watu wenye roho mbaya wanaona mgeni akilala kwao atafaidi na kudhani kama ataondoka na nyumba.
 
Mkuu ungemlaza sebuleni tu...either Mtoto alale sebuleni au Mgeni alale sebuleni...

Anko wa siku hizi wamekuwa wa hovyo sana,,, Niishie hapo
 
Mkuu ungemlaza sebuleni tu...either Mtoto alale sebuleni au Mgeni alale sebuleni...
Hii ni option nzuri sana.

Au yeye angelala na mgeni alafu binyi akalale na mama yake.

Au mtoto angelala sebuleni.

Kwa kufanya hivyo huyo anko angeona tabu kwamba hapa sehemu za kulala hamna mpaka wenye nyumba wanalala sebuleni,angejiongeza na kuondoka ila angetoka na dhana kwamba wenye nyumba ni wastaarabu.

Kinyume na alivyofanya yeye kumchana mgeni eti dunia imechange,dah kazingua ssna.

Ila sishangai kuna baadhi ya wstu hawajui thamani ya mgeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…