Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Kinyume na alivyofanya yeye kumchana mgeni eti dunia imechange,dah kazingua ssna

Kumwambia mgeni Dunia imebadilika amefeli sana,,,, hakuna Busara ya namna hio.. unamfanya mgeni ni mtuhumiwa tayari.
Ujue dunia ya sasa imekuwa ngumu sana,, Zamani watu walikuwa wanafurahia wageni lakini leo ugeni imekuwa kero kwa wengi...

Option ya kulala sebuleni ilikuwa the best na familia zetu wengi, watoto tumeshawai kulala sebuleni ili wageni walale vyumbani.. (ni kawaida sana kwa jamii yetu).

Kizazi cha sasa hata ukienda kwa mtu ghafla utaonekana unamaliza Ugali hehehehehe.. Sijui ni kizazi cha hovyo au ndio wakati umetaka mabo yaende hvyo.

Niishie hapo...
 
Angelilala ukumbini mwenye nyumba huwenda huyu mgeni angeona haya kwamba anawabana angeondoka mwenyewe.
 
Mkuu kwanza huo ujasiri wa kumruhusu alale chumba cha watoto uliutoa wapi????
Aiseeee watu hampo serious kiasi hiki!!!
 
Habari ya leo.

Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume (miaka zaidi ya 30) na alilala chumba cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"

Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumbani. Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu

WANDUGU:

Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani. Nipo sahihi au inakuwaje?
Ww endelea kumlea mpka akamilishe anachokitaka alafu uje uandike uzi mwingine.

Ila sisi watanzania muda mwingine sijui tupoje!! Unaona kabsa mtu anapoishi panatosha yeye na familiar yake tu na hapaitaji wageni wa kulala ila bado unaenda! Hizi tabia za kipumbavu sana
 
Habari ya leo.

Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume (miaka zaidi ya 30) na alilala chumba cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"

Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumbani. Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu

WANDUGU:

Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani. Nipo sahihi au inakuwaje?
Mfukuze haraka Sana huyo
 
Wanaadamu mnakosea sana ku approach ishu kama hizi,hamuna diplomacy katika kusolve ishu zenu.

Kumbuka kutumia diplomacy kusolve matatizo kunawafanya muendelee kuwa wamoja,unaposhindwa kutumia diplomacy katika ishu kama hizo watu wanatone roho mbaya kwako na kuna siku itakutokea puani.

Kwanza kumlaza mgeni nje ya nyumba ni tabia mbovu sana na ni utovu wa adabu ni sawa mgeni aje alafu wewe ukamuombee chakula kwa jirani huku akiona.

Ustaarabu ni mgeni kumuachia nyumba alale nyie mtajua mnalala wapi,silazimishi kukubali ustaarabu huu.

Nakumbuka kuna mwaka nilienda kwa ndugu zangu pale mbagala wana chumba na ukumbi,walichofanya waliniachia chumba nikalala wao sijui walilala wapi asubuhi mapema nimewakuta wanaendelea na mambo mengine mimi nikaamsha nililala siku moja tu,hii ndio ustaarabu.

Nyie binadamu wengine sijui mumekulia wapi,mna roho za ajabu sana aisee.

Sijui ulishindwa nini kulala na mtoto wenu kisha mgeni akalala peke yake,sio ustaarabu huu.

Na namna ulivyokuwa na roho mbaya ukamuambia kabisa ati dunia imejaribika,maana yake umemuonesha kwamba humuamini.

Na sio k2amba humuamini kulala na binti yake tu bali hata kulala hapo nyumbani bila binti asilale ukaenda kumtupa huko gesti,angezidiwa usiku ?,angekabwa ?

Sio ustaarabu mkuu,ningekuwa mimi ndio anko hiyo lodge nalipa mimi mwenyewe maana umefanya ubwege sana.

Siku zote tumia diplomacy kusolve matatizo utaishi vizuri na jamii hata ndugu zako pia.
Uko sahihi.
Mtu mzima tena wa kiume kulala na watoto iwe wa kike au wa kiume,,sio jambo zuri,,

Lakin pia njia iliotumika kutatua tatizo kama ulivoeleza sio njia ya busara,,

Wangelala na mtoto chumbani ,,mgenini akalala peke yake kwenye chumba cha watoto_ a very simple solution

Mtoa maada ametumia nguvu kubwa saana kutatua tatizo dogo

Mtoa maada anaweza kua kweli ameshinda lakini hebu ajalibu kuvaa viatu vya mgeni wake,,kama angekuwa yeye angehisije tena unaambiwa kabisa kuwa "uenaenda kulala gest kwa sababu sikuamini kulala na watoto wangu,,"

Lazima kama mtu mzima ujisikie vibaya.
 
Onesha uhusiano wa miaka yangu na mada.

Mimi sikatai kuwepo kwa hayo matendo,hoja yangu mkuu ni kwamba mtu kama huyo wenu hajawahi kusikika na hivyo vitendo.

Sasa katika kusolve usimhukumu kwamba yeye tayari ni mhusika.

Sio ustaarabu kumlaza mgeni nje ya nyumba yako.

Hoja yangu kwa nini usilale na mwanao huyo mgeni akalala peke yake ?

Au ulihofia angekuja chumbani kwenu kuwalawiti wote nyie na huyo binti ndio maana ukampeleka gesti ?

Hujafanya poa kaka,huo sio uungwana

Hoja yangu mungelala na binti yenu alafu huyo anko angelala peke yake angemlawiti vipi huyo mtoto,au uliogopa asije kuwalawiti na nyie wazazi hapo nyumbani ?

Ulishasema kwamba huyo anko hakuamini,kwa maana ameshtukizwa na maamuzi yako,inshort haukufanya maamuzi ya kiume yenye akili,umefanya maamuzi ya kitoto ndio maana hata mkeo akakubali kishingo upande tu.

Au ungelala nae wewe kisha mtoto angelala na mkeo(mama yake) hii pia ulikuwa unaogopa kalawitiwa na shemeji yako ?
Mkuu uko sahihi,,

Uamuzi alioufanya haukuwa wa busara
 
MREJESHO

Kabla ya kupiga msos niliamua kumueleza wife kuwa "uncle" naenda kumlaza lodge na siwez kumuweka rehani cute girl wangu. Wife alikubali kwa shingo upande.

Fasta nikawacheki wadau wa boda waniangalizie chumba logde za uswazi.

Wakati wa kupiga msosi nikaamua kumchana "uncle" jinsi Dunia ilipofikia na maamuz yangu kwa wakat huo. Jamaa kwanza hakuamin kama nampeleka nje kulala kwa kuwa alijua tayar kafika.

Kiufupi, kalala logde ya kawaida sana (Bei kapuni) tofauti na kitambi kinavyomuonesha.

Nashukuru sana kwa msaada wa mawazo yenu. Linda familia yako bila kujali lawama zotakazo tokea
Wow hongera mkuu uamuzi mzuri Sana yaani suala la mtu mzimakulala chumba kimoja na mtoto usirudie kabisa kesi za unyanyasaji wa watoto zimekua nyingi Sana na takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya watoto wanaofanyiwa ukatili wa kingono wanaofanyiwa na watu wao wa karibu(wanafamilia).Malezi ya watoto kipindi hiki ni magumu Sana Mungu awasaidie wazazi wote.
 
Walimwengu roho zimetugeuka, heri nusu shari!
Akija tena mkaribishe, usiku apate dinner baada ya hapo nyumba ya kulala wageni...baaasi!
 
MREJESHO

Kabla ya kupiga msos niliamua kumueleza wife kuwa "uncle" naenda kumlaza lodge na siwez kumuweka rehani cute girl wangu. Wife alikubali kwa shingo upande.

Fasta nikawacheki wadau wa boda waniangalizie chumba logde za uswazi.

Wakati wa kupiga msosi nikaamua kumchana "uncle" jinsi Dunia ilipofikia na maamuz yangu kwa wakat huo. Jamaa kwanza hakuamin kama nampeleka nje kulala kwa kuwa alijua tayar kafika.

Kiufupi, kalala logde ya kawaida sana (Bei kapuni) tofauti na kitambi kinavyomuonesha.

Nashukuru sana kwa msaada wa mawazo yenu. Linda familia yako bila kujali lawama zotakazo tokea
Huna akili wewe!! Umevunja mahusiano mazuri na anko wako kwa akili za kuambiwa. Hujui kesho kama utakuwa umelala mauti ni nani atakulelea watoto wako. Labda huyo ulie mnyapaa kwa kumpeleka gest ya kunguni ndo anaweza kuwa msaada kwa wanao.

Hivi unawezaje na unaanzaje kumpeleka ndugu yako gest ili hali una pa kumlaza. Huo ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.

Umeshindwa nn kulala na mwanao mgeni ajihifadhi kwa hiyo siku moja au hata ingekuwa wiki kuna ubaya gani. Naweza kusema pia ww ni mchoyo umemfukuza kijanja.

Kingine nyie watu wa mjini acheni uzungu majitaka. Mbona mkija huku vijijini kwetu tunawakarim vizuri tu na nyumba hizi hizi za vyumba na sebule na wakati mwingine tunawapa hata magodoro yetu na wake zetu sisi tunabaki tumelalia mbavu za umbwa!?
 
Katu sitoruhusu mtu yeyote kulala na wanangu, hao wageni wakalale lodge huko, dunia imebadilika sana.
 
Huna akili wewe!! Umevunja mahusiano mazuri na anko wako kwa akili za kuambiwa. Hujui kesho kama utakuwa umelala mauti ni nani atakulelea watoto wako. Labda huyo ulie mnyapaa kwa kumpeleka gest ya kunguni ndo anaweza kuwa msaada kwa wanao.

Hivi unawezaje na unaanzaje kumpeleka ndugu yako gest ili hali una pa kumlaza. Huo ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.

Umeshindwa nn kulala na mwanao mgeni ajihifadhi kwa hiyo siku moja au hata ingekuwa wiki kuna ubaya gani. Naweza kusema pia ww ni mchoyo umemfukuza kijanja.

Kingine nyie watu wa mjini acheni uzungu majitaka. Mbona mkija huku vijijini kwetu tunawakarim vizuri tu na nyumba hizi hizi za vyumba na sebule na wakati mwingine tunawapa hata magodoro yetu na wake zetu sisi tunabaki tumelalia mbavu za umbwa!?
Jamaa ametumia hisia badala ya akili,,,anasahau kuwa kuna kesho.

Tena kibaya sana amemwambia wazi kabisa hamuamini kulala na watoto wake,

Yes,it is good usimuamini mtu,,lakini kulikuwa na ulazima gani wa kumwambia hili,,

Kama ingeshindikana kabisa kulala kwake basi angetafta excuse ya busara alafu angempeleka mgeni wake guest,,
Hii ya kumuhukumu Mtu kwa hisia ni mbaya sana,,sio kila mtu ni mbaya,

Kitachomuumiza mgeni wake sana sio kulala gyest,,ila ni sababu iliyofanya apelekwe guest,
 
MREJESHO

Kabla ya kupiga msos niliamua kumueleza wife kuwa "uncle" naenda kumlaza lodge na siwez kumuweka rehani cute girl wangu. Wife alikubali kwa shingo upande.

Fasta nikawacheki wadau wa boda waniangalizie chumba logde za uswazi.

Wakati wa kupiga msosi nikaamua kumchana "uncle" jinsi Dunia ilipofikia na maamuz yangu kwa wakat huo. Jamaa kwanza hakuamin kama nampeleka nje kulala kwa kuwa alijua tayar kafika.

Kiufupi, kalala logde ya kawaida sana (Bei kapuni) tofauti na kitambi kinavyomuonesha.

Nashukuru sana kwa msaada wa mawazo yenu. Linda familia yako bila kujali lawama zotakazo tokea

👏🏽👏🏽👏🏽
Copy na paste mrejesho post yako #1 chini ya uliyoandika..
Butua edit..
 
Habari ya leo.

Miezi kama 3 iliyopita alinitembelea shemeji yangu wa kiume (miaka zaidi ya 30) na alilala chumba cha watoto. Ikumbuke Nina Binti/mtoto wa kike miaka 5, wakati huo niliongea na mama watoto kuwa next time sitaki kuweka utu wa mtoto wangu rehani kwa watu wanaojiita "uncle"

Leo tena "uncle" kaja kwa mishe zake lakn bila ya kutoa taarifa, ninvyoona jamaa atalala hapa nyumbani. Sina chumba Cha wageni zaidi ya familia yangu tu

WANDUGU:

Nafikiria kumtafutia lodge akalale kuliko kulala na Binti yangu chumba kimoja maana Dunia imewekwa rehani. Nipo sahihi au inakuwaje?
Upo sahihi kabisa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom