Wanaadamu mnakosea sana ku approach ishu kama hizi,hamuna diplomacy katika kusolve ishu zenu.
Kumbuka kutumia diplomacy kusolve matatizo kunawafanya muendelee kuwa wamoja,unaposhindwa kutumia diplomacy katika ishu kama hizo watu wanatone roho mbaya kwako na kuna siku itakutokea puani.
Kwanza kumlaza mgeni nje ya nyumba ni tabia mbovu sana na ni utovu wa adabu ni sawa mgeni aje alafu wewe ukamuombee chakula kwa jirani huku akiona.
Ustaarabu ni mgeni kumuachia nyumba alale nyie mtajua mnalala wapi,silazimishi kukubali ustaarabu huu.
Nakumbuka kuna mwaka nilienda kwa ndugu zangu pale mbagala wana chumba na ukumbi,walichofanya waliniachia chumba nikalala wao sijui walilala wapi asubuhi mapema nimewakuta wanaendelea na mambo mengine mimi nikaamsha nililala siku moja tu,hii ndio ustaarabu.
Nyie binadamu wengine sijui mumekulia wapi,mna roho za ajabu sana aisee.
Sijui ulishindwa nini kulala na mtoto wenu kisha mgeni akalala peke yake,sio ustaarabu huu.
Na namna ulivyokuwa na roho mbaya ukamuambia kabisa ati dunia imejaribika,maana yake umemuonesha kwamba humuamini.
Na sio k2amba humuamini kulala na binti yake tu bali hata kulala hapo nyumbani bila binti asilale ukaenda kumtupa huko gesti,angezidiwa usiku ?,angekabwa ?
Sio ustaarabu mkuu,ningekuwa mimi ndio anko hiyo lodge nalipa mimi mwenyewe maana umefanya ubwege sana.
Siku zote tumia diplomacy kusolve matatizo utaishi vizuri na jamii hata ndugu zako pia.