Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

“Wanashambulia hadi familia yangu, nimemposti mtoto wangu wa kwanza ilikuwa siku ya Birthday yake watu wanaandika ushambaushamba mpaka baba yangu akanipigia simu anasema ‘ni nini hiki mbona sio wewe wanaanza kuingia kwenye familia, nilichomjibu baba ni kuwa nilikosea kucheza Tanzania”

Fiston Mayele akizungumza katika mahojiano na Azam Tv.

Hili linaloendelea litufundishe jambo, kuna mambo ya kuongea na kutokuongea, ikumbukwe yeye ndie alieanza kuirushia maneno Yanga na bado anaendelea. Sidhani kama ataiweza vita na mashabiki (maneno, ushirikina) na kama ndio mtu wa kujali yanayoandikwa mtandaoni hali itazidi kuwa mbaya kwake.

Ushauri wangu ni bora akae kimya kuliko kuendeleza maneno.

View attachment 2960619
Unapokuja Yanga na Simba ujue umekuja kwenye siasa.

Kabla ya kuja Tanzania muwe mnauliza ,hii ni Nchi ya watu wenye mdomo kuliko kawaida
 
Mayele alikosea kucheza utopoloni. Sio tanzania .hao utopolo akili hawana. .mchezaji wao yeyote akiwa mzuri akiondoka lazma watamchukia .angalia Morriston,feisal na sasa mayele. Hyo timu ndo tabia zake.we timu inaandika barua kuomba wapewe goli wana akili hao?
Mjinga ni yeye hadi ana sign contract hakujua kuwa haikuwa sahihi yeye kucheza TZ? Umaarufu unamzuzua ila nahisi pia haya yote anayafanya ili SIMBA SC imsajili.
 
Unapokuja Yanga na Simba ujue umekuja kwenye siasa.

Kabla ya kuja Tanzania muwe mnauliza ,hii ni Nchi ya watu wenye mdomo kuliko kawaida
Hakika, hizi timu zimekaa kisiasa siasa sana, unayoyasikia nje na utakayoyakuta ndani ni tofauti kabisa. Wachezaji wanapaswa kuwa makini. Mashabiki ndio wenye timu na ndio wanaoumia timu ikisemwa vibaya n.k
 
maneno kama maji ya moto tu, ukiona makali lakini hayaunguzi nyumba.

ukishapigana guerilla war
desert war
biological war
na hata zile vita vya katkati ya jiji.

basi utaelewa nasema nini
Sio kwa mayele, anaonekana ni mtu ambae maneno yanamvuruga kabisa. Kama ni mtu wa hivyo auchunge sana mdomo wake.
 
Jamaa habari yake ndio imeisha hivyo...

Kwanza ashukuru kwa kucheza Tanzania maana ndipo kumemfanya awe maarufu na kuonekana kwa hizo timu nyingine...
Huyo ndio asahau kucheza vilabu vikubwa barani africa na hata akicheza aanzi 1st 11.

Anajutia kucheza Tz kulikomfanya aonekane Africa.
 
Yanga ndo yenye mashabiki bora kabisa. Wanawasaidia viongozi wao sana. Mchezaji akitoka yanga awe kajipanga ataandamwa kipropaganda Lengo asiwe na madhara kwao.Halafu wakipata mchezaji watampamba kupita uwezo wake. Inaitwa branding
 
Yanga na wanayanga wajifunze kupotezea... Msiwaandame mno wachezaji wanaotoka njee ya yanga.
Huu ni ushamba wa kiwango cha lami. Sijawahi ona jambo kama hili kwa simba na wanasimba kwa ujumla.
Anyway mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...
mayele aliondoka na tukampa heshima zote shida alijitokeza na kudai ametupiwa majini. Mbona yanga wametoka wengi tu na wapo huko wanaendelea na maisha yao
 
Yanga ndo yenye mashabiki bora kabisa. Wanawasaidia viongozi wao sana. Mchezaji akitoka yanga awe kanipanga ataandamwa kipropaganda Lengo asiwe na madhara kwao.Halafu wakipata mchezaji watampamba kupita uwezo wake.
Yanga wanajua kumpa mtu thamani(hii ni kazi ya management).
Mashabiki nao wanajua kumpora mtu ile thamani kwa kumuandama kama huyo mwenye majini.
 
Back
Top Bottom