M'bananga chake hana kondo (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Kwanza, kwa miaka 62 Watanganyika walipoteza nchi yao kwa ajili ya Muungano, hawakuwahi kuisema Zanzibar. Hoja ya Tanganyika imeletwa mezani na Wazanzibar kwa kisingizio kwamba Bara wamejificha katika koti la Muungano. Hivyo Utanganyika umeombwa na Wazanzibar. Mkandara hakuona hiyo kama chuki za kipumbavu.

Hapa JF kuna mjadala mkandara ukitetea hoja za Wazanzibar kwamba wasikilizwe. Leo unaita upuuzi na upumbavu kwa hoja zile zile ulizotetea wakati upuuzi na upumbavu ukiwa ''in the making'

Pili, Wakati Maalim Seifa na akina Jussa wakitukana Muungano na kumwita Nyerere LAANATULLAH, wakidai mamlaka kamili Mkandara alikuwa kimya hakuona upuuzi na upumbavu, leo anauona

Tatu, wakati Zanzibar inataka mgao wa kila inachotaka Mkandara ulisema '' ni wadogo'' wanastahili kusaidiwa. Mkandara hakuona upuuzi na upumbavu kwamba zilikuwa nyufa za Muungano, hatimaye amefunguka macho

Nne, wakati Wazanzibar wakiusema Muungano ilikuwa ni halali, Mtanganyika akisema muungano ni haramu.

Prof Kabudi akiwa bado 'mzima' alisema '' Watanganyika wana yao moyoni wakiyatoa na kuidai Tanganyika yao itakuwa tatizo'' . Mkandara alikuwa akimya kwasababu Zanzibar ina haki ya kusikilizwa, si Tanganyika

Tano, hoja ya Mkandara ya changu ni changu na chako ni changu haiwahusu Watanganyika. Tanganyika imebeba muungano 100% . Waeleze Z'bar si kuwalaumu waliobeba zigo la misumari mgongoni

Sita, wakati Zanzibar inaanzisha Taasisi mbadala wa zile za JMT Mkandara alikuwa kimya. Leo akilulizwa kwanini kuna Taasisi mbadala hana jibu anawalaumu Watanganyika wanaohoji.

Hizi taasisi zinazoitwa za Muungano kama TCRA ni za Tanganyika, Zanzibar wana zao. Wazanzibar wanazitumia wanapohitaji mafao. Ni kama kuwa na kitambulisho cha NIDA kwa ajili ya kufanya shughuli Tanganyika

Mfano, Makusanyo ya TCRA yatokanyo na mawasiliano, Zanzibar inapewa sehemu yake. Yaani Mkandara akimpigia simu ndugu yake Ukerewe kuna aslilimia inapelekwa Zanzibar.

Halafu Mkandara huyo huyo anasema sisi ni nchi moja Tanzania kwanini kuwe na double taxation! Hajiulizi kwanini simu ya Mtwara-Musoma iwe na asilimia inaypelekwa Zanzibar

Saba, Mkandara anasema hoja ya kudai kuona mchango wa Zanzibar katika Muungano ni ya kipuuzi.
Mkandara huyo huyo anatetea hoja za Wazanzibar kudai wapewe lakini hataki kusikia wakiambiwa wachangie.


Tumefika hapa kwasababu tlifumbia macho upuuzi wakati unajijenga! Hatukuambina ukweli kwa kisingizio cha Muungano ni tunu yetu. Tuliwapa Wazanzibar kama Raia ''special'' wanaopaswa kuhudumiwa na kuamua hatma ya Tanganyika. Ule muda aliosema Prof Kabudi nadhani umewadia.

Mnyonge mnyngeni haki yake mpeni, Prof Kabudi alikuwa mbele ya muda miaka 12 iliyopita
 
Kwqnza sijui ulinisoma vizuri au Laa? Maana nimesema itekezaji wa Serikali zetu SIKU hizi haufanani kabisa na ule muundo alotuachia Mwalimu, nikasema toka 1995 kumekuwa na mabadiliko mengi ambayo yanaashiria kana kwamba tuna mfumo wa Serikali za mseto, kuna ya Serikali 3 na Jumuiya kinyume kabisa na Serikali 2.

Haya maswala ya kutofautiana Pension yamekuja miaka hii ni pamoja na TRA, Bandari, na taasisi nyingi zilokuwa katika mambo ya Muungano yameondolewa kinyemela. Kifupi naunhana na Mzee Warioba ku question haya yanayofanyika sasa hivi.

Niliendelea kusema siwezi kuilaumu Serikali ya Zanzibar kwa sababu TULIRIDHIA mabadiliko hayo yatokee (Bunge la Jamhuri)laa sitaki kuamini Zanzibar wanaweza jiamulia kufanya hayo kinyume cha Katiba ya Jamhuri.

Mabadiliko mengi wameyafanya baada ya Mwalimu hasa miaka hii ya elfu 2 na sijasikia Kiongozi hata mmoja wa Bara akiuliza, zaidi ya wakati ule Mheshimiwa Pinda alipambana nao waliposema Zanzibar ni NCHI wakati Muungano wetu ulilenga kuunda NCHI MOJA yenye Serikali 2 (Unitary States) sio Federation.

Na dhana hii ya Federation imetumiwa na wengi kuhoji Muungano wetu wasijue hatukuungana kama Federation. Kwa hiyo mkuu wangu sipendi kuwanyooshea kidole Zanzibar ikiwa wanapata baraka za Bara kwa maana hiyo CCM wanaridhia yote haya.

Kifupi Ukiukaji wa Katiba umekuwa jambo la kawaida kabisa na sasa imefikia hata baadhi viongozi kujiona Wananchi wanawatumikia wao. Hunishangaza sana napoona Kiongozi anawakaripia Wananchi.

Wewe na Uelewa wako umewahi msikia Trump akikaripia Wananchi? Atasema ovyo kwa nchi nyingine ama Watu wa mataifa mengine lakini hathubutu kuwakaripia Wamarekani. Utayaona haya nchi zetu maskini sio nchi zenye Demokrasia ya kweli.

Kuhusiana na Mambo ya Muungano unataka kufaidika kupi yaani? Yaani nikikuuliza wewe mkeo unafaidika nini kuwa na wewe, utajibuje?

Kwa pamoja tina ukanda wa zaidi ya maili 200 ya bahari, kufaidika kungetokea kama tungrkuwa na mipango madhubuti ya kimaendeleo kama NCHI MOJA. Kama huoni kufaidika kwa Tanganyika ni kutokana na Utawala wameshindwa kuwekeza Zanzibar kwa maslahi ya Tanzania.

Niliwahi andika humu miaka ile, kama Tungeiwezesha Zanzibar kuwa Free port na Free economic zone kama Dubai, biashara nyingi zingeshuka Zanzibar kwa ajili ya nchi zinazotuzunguka.

Watu wasingeenda Dubai, kwa sababu kila kitu kinapatikana Zanzibar na rahisi kuvushwa kwenda DRC, Zambia, Uganda, Rwanda Burundi na hata Zimbabwe. Pia tungekuwa busy zaidi kusafirisha Budhaa zetu nje.

Hii reli ya SGR ingekuwa busy sana na pengine Tanzania tungekuwa Hurmuz Strait ya East na South Africa. Biashara kubwa inatoka East Asia sio Marekani na Europe tena.

Kwa hiyo, Kufaidika kunatokana na mipango ya pamoja kuijenga NCHI moja na sii kugombania NCHI 2 utadhani ndugu wanagombania Urithi. Siku zote hakuna Mshindi mtagawana mali, lakini mmepoteza Undugu. Thamanibya UTU wenu imepotea..
 
Dunia ipi? Labda unazungumzia Afrika lakini Marekani wapo pamoja toka karne ya 18, Uingereza toka lini Ujarumani waliondoa tofauti zao leo nchi moja. Na historia ya nchi nyingi ziloendelea hazikuwa nchi moja.

Itazame China inavyosumbuliwa na Taiwan! Korea ya Kusini na Kaskazini. Maisha gani yale! Tazama upande wa pili yalowakuta USSR yamewafika nini? Russia leo wanapigana na Ukraine! Ukanda ule wore maadui. Tazama Yugoslavia walivyomalizana vita ya Serbia na Kosovo! Hakuna NCHI hata moja ya mfano nzuri wa kuvunja Muungano wakabakia salama.

Inakuwaje wewe unasema waasisi sio Mungu? Nani alosema wao ni Miungu, bali tunatazama mifano kama hii. Tukivunja Muungano unamkomoa nani? Una gain kitu gani maana kama Maskini utabakia Maskini hutanufaika na lolote zaidi ya CHUKI.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri sana. Wausome huu na kuuelewa wachangiaji mada hii bila jazba
 
Haya maswala ya kutofautiana Pension yamekuja miaka hii ni pamoja na TRA, Bandari, na taasisi nyingi zilokuwa katika mambo ya Muungano yameondolewa kinyemela.
Thank you! Kwanini unawaulumu Watanganyika? wangefanya nini kuzuia hilo ikiwa hawana serikali
JMT si Tanganyika. Kuna Waziri alipoteza kazi kwasababu hakukubaliana na sera fulani isiyopendelea kule!
Niliendelea kusema siwezi kuilaumu Serikali ya Zanzibar kwa sababu TULIDHIA mabadiliko hayo yatokee (Bunge la Jamhuri)laa sitali kuamini Zanzibar wanaweza jiamulia kufanya hayo kinyume cha Katiba ya Jamhuri.
Nakubaliana nawe katika hili
Sipendi kuwanyooshea kidole Zanzibar ikiwa hawapati baraka za Bara kwa maana hiyo CCM wanaridhia yote haya.
Wazanzibar walfanya kiburi tulichowajengea kwamba ni muhimu kwa Tanganyika. Kabla ya 1995 walikuwa na hoja '' msipofanya abcd tunavunja muungano'' wanatimiziwa. Mwaka 1995 na G55 ulibadilisha upepo, Tanganyika haiwahitaji! Wazanzibar wakaja na slogan ya ''kero za Muungano'' yaani madai hakuna kero ya wao kuchangia!
Tumeendelea na ujinga wa kero leo ''silent majority' wameacha ukimya, wanataka Tanganyika (Ref Prof Kabudi)
Kuhusiana na Mambo ya Muungano unataka kufaidika kupi yaani?
Hoja ni kwamba katika yale mambo 22 unayosema yaliongezwa , lipi ambalo Tanganyika imenufaika nalo?

Nitakupa moja ambalo Zanzibar wamenufaika, Elimu ya Juu. HESLB inadhamini Wanafunzi wengi wa Zanzibar kuliko ZHESLB! nje ya Muungano wapo Wazanzibar hawataenda shule kwa kuosa hii ''Grant'' si mkopo!

Nitajie moja tu katika yale 22 ambayo Tanganyika imenufaika! Hoja hapa ni kwamba kuongeza mambo 11 hadi 22 kulilenga kuiumiza Zanzibar! na wewe umeshadidia, sasa tupe moja tu unaloona limenufaisha Tanganyika!
Utawala wameshindwa kuwekeza Zanzibar kwa maslahi ya Tanzania. Tungeiwezesha Zanzibar kuwa Free port na Free economic zone kama Dubai, biashara nyingi zingeshuka Zanzibar kwa ajili ya nchi zinazotuzunguka.
Kwanza tumewekeza Sana Zanzibar! suala ni kwamba Wazanzibar wanajiongeza vipi? lakini pia kuna uchoyo.
Walipoambiwa kuna debe mbili za mafuta wakaondoa katika Muungano.
Wakaambiwa Bandari ina uchumi mkubwa wakaondoa katika Muungano. Ukiwapa free port unategemea nini!

Hata sasa hivi bandari yao ni free port kwa mujibu wao. Tatizo ni kutumia vibaya nafasi yao katika Muungano. Mwaka huu Madawa na Maziwa hovyo yaliingizwa Zanzibar kupitia ZBS. Haya soko lake ni Tanganyika

Licha ya Afya za watu, hatuwezi kuendesha nchi kwasababu tutoze kodi watu wetu ili bidhaa zisiozotozwa kodi ziingizwe nchini kupitia Zanzibar. Kumbuka hakuna kodi inayovuka bahari kuja Bara! uwape free port! my foot

Tumewekeza katika rasilimali watu, fikiria nusu yao wanaoishi Tanganyika wakirudi kule itakuwaje
Tumewekeza sana kwa kupunguza gharama za uendeshaji wa SMZ ikiwemo subsidy ya Bajeti
Hadi vitu kama umeme wanapewa bure! sasa unahitaji nini zaidi
Hii reli ya SGR ingekuwa busy sana na pengine Tanzania tungekuwa Hurmuz Strait ya East na South Africa. Biashara kubwa inatoka East Asia sio Marekani na Europe tena.
Itakuwa busy kwasababu kuna soko la watu Milioni 13 Burundi, Milioni 12 Rwanda, Milioni 90 DRC.Hatuhitaji bidhaa ziteremke Zanzibar! ikiwa free port ni muhimu tutabadilisha ya Tanga! By the way ipo ya Bagamoyo inayojengwa
Kwa hiyo, Kufaidika kunatokana na mipango ya pamoja kuijenga NCHI moja na sii kugombania NCHI 2 utadhani bdigu wanagombania Urithi. Siku zote hakuna Mshindi mtagawana mali, lakini mmepoteza Undugu. Thamanibya UTU wenu imepotea..
Hakuna mipango na Zbar, ubinafsi umewazidi. Tunaweza kuwa na mipango na DRC, Rwanda na Burundi kwa soko la watu Milioni 113 na ushee! hatuhitaji kelele na 1.8M na nusu wanaishi kwetu!
Mkandara hivi unaifahamu Zanzibar wewe! ni kaeneo tu
 

..Zanzibar ilipata UHURU tarehe 10 Dec 1963.

..Katiba ya Zanzibar huru ilitokana na muafaka wa mazungumzo yaliyofanyika Lancaster Uingereza.

..Katiba nyingi za makoloni ya Uingereza zilijadiliwa Lancaster.

..Mfumo wa utawala uliokubaliwa na wadau, ASP ikiwemo, ilikuwa ni Constitutional Monarchy.

..Zanzibar huru ilikuwa na Mfalme, Waziri Mkuu, Bunge la vyama vingi, na Mahakama.

..Mapinduzi ni UHAINI ulioondosha utawala wa kikatiba uliokuwepo Zanzibar.

..Baada ya Mapinduzi Zanzibar iliongozwa bila Bunge mpaka mwaka 1980, na bila mahakama ya kisasa mpaka mwaka 1985.

..Hicho ndicho kilichotokea Zanzibar. Ndio ukweli mchungu ambao CCM hawataki ujulikane.
 
Shukran kwa maelezo uloyapa UKweli wa hadith za kusadikika. Labda nikuulize hivi Utawala wa Zanzibar kabla ya hiyo Dec 10, 1963 ilitawaliwa na nani? Na kwa nini watu weusi walishiriki katika mauaji dhidi ya Waarabu na Wahindi badala ya viongozi wa Serikali. Siri nyuma ya Chuki zile ilikuwa nini haswa?

Ebu waulize hao WaZanzibar kina Jussa. Zanzibar kabla ya 1964 ilitawaliwa na nani? Je, wanakubali Zanzibar haikuwa Nchi Huru wakati wa USultan?

Je, Zimbabwe ilipata Uhuru wake lini? Kama unakumbuka wakati ule ikiitwa Rhodesia walipata Uhuru wao kutoka kwa Muingereza tarehe Nov 11, 1965 na Waziri mkuu akiitwa Ian Smith. Na baada ya Mapinduzi ya Wananchi Uhuru mpya ukatangazwa April 18, 1980! Hapo inakuwaje?

La mwisho, Hivi ikitokea Uingereza Ikapinduliwa, unaweza nambia ni nani alopinduliwa? Mfalme King Charles au Waziri Mkuu Andy Burnham?
 

..kabla ya 1963 Zanzibar ilitawaliwa na Waingereza.

..Ndio maana unaona Katiba yao ilijadiliwa na kuandikwa chini ya usimamizi wa Waingereza.

..Na umoja wa Mataifa uliutambua uhuru wa Zanzibar wa Dec 10, 1963.

..Zanzibar ya 1963 ni tofauti na Rhodesia ya kina Ian Smith, au Makaburu wa Afrika Kusini.

..ASP walishiriki majadiliano ya Katiba ya Zanzibar Huru. ASP vilevile walishiriki uchaguzi.

..Hii ni tofauti na Rhodesia, au Afrika Kusini, ambako vyama vya Waafrika vilipigwa marufuku, na wachache walijitangazia uhuru.

..kuhusu Uingereza kupinduliwa, huko utakuwa umekwenda mbali. Lada ungeuliza Swaziland ikipinduliwa. Je, Swaziland sio nchi huru?

..Hata mimi nilikuwa nayaamini MAPINDUZI lakini nimekuja kugundua labda ukweli ni 40% iliyobaki ni uongo.
 
Haitakuwa vema nisipo tolea maelezo yangu kuhusiana na Ulichosema maana Uongi ukisemwa sana hugeuka kuea Ukweli.

Nianze na hilo la kusema Mwalimu alitaka Serikali 1 ati Serikali 2 ilikuwa kianzio tu. Sii kweli kwa sababu alitaka Serikali 1 alikuwa Karume, hivyo ingekuwa rahisi sana kwake kupitisha maana upande wa Zanzibar ulitaka Serikali 1.

Yawezekana huelewi yq kwamba wakati ule Pan Africanism ndio zilitawala Siasa za Uhuru kwa nchi za Kiafrika kiasi kwamba walitaka Afrika nzima iwe NCHI MOJA kwanza na sii Serikali ngapi. Jariby kutenganisha NCHI na Serikali kuelewa mtiririko wa hoja zangu.

Hivyo, Mwalimu alisema ni bora kwanza tuanze na Kuunganisha NCHI kila zinapopata Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni na kwanauoande wetu kukaanzishwa Pan - African Freedom Movement for East and Central Africa (PAFMECA) Mwenyekiti akiwa Mzee Jomo Kenyatta.

Kwa hiyo, Muungano wa Nchi za Afrika Mashariki ulitakiwa kufanyika kutokana na makubaliano ya Pan-Africanism katika mkutano wa kwanza (Pafmeca) ulofanyika Mwanza mwaka 1958 wakishiriki viongozi wa nchi 5 - Tanganyika, Kenya, Uganda , Malawi na Zanzibar. Elewa hii ilikuwa mwaka 1958 hakuna Nchi wakati ule ilokuwa na Uhuru kamili.

Mkutamo mwingine ulofuata ulikuwa mwaka 1963 baada ya Kupata Uhuru ndipo wenzetu wengine wakachomoa tukabakia sisi na ndio swala la Serikali ngapi kujadiliwa.

Mwisho niseme hata maneno alosema Karume hayakuhusu Serikali ngapi bali Muungano wenyewe wapo Viongozi hawakuafiki Zanzibar kuungana na Tanganyika wakati Nchi nyingine zimejitoa. Ndio akatoa mfano wa Koti.

Yes, tunaweza kulivua KOTI la Muungano lakini kama nilivyowahi kusema huko nyuma. Tatizo sio Koti ulovaa bali Afya yako mwenyewe aidha umenenepa kupita vipimo vya Koti lenyewe ama Umekondeana kuliko koti lenyewe litakupwaya. Wa kujitazama ni Wewe sio Koti.

Matatizo yote ya Muungano yanasababishwa na Viongozi wetu ambao aidha kwa Ulafi wao wameshindwa kuliongoza Taifa katika kutuletea Amani, Haki, Usawa na Maendeleo.

Tutausulubu Muungano kwa makosa ya watu hawa hawa ambao wataendelea kutawala Nchi mbili tofauti kwa mawazo yao yale yale. Hiyo Amani, Haki na Usawa vitapatikanaje?

Maasalaam
 
Nitakwenda na wewe kwa kituo. Haya naomba nambie Muingereza alianza kuitawala Zanzibar mwaka gani? Kila kitu kina mwanzo au sio?

Ikiwa Zanzibar walipata Uhuru wao mwaka 1963 kwa nini Muingereza alisimamia uandishi wa Katiba yao? Isitoshe kama Muingereza alikuwa Mtawala kwa nini hakuingilia Mapinduzi ya mwaka 1963 ambayo yeye aliwakabidhi ZNP kuunda Serikali? Mbona kwa Tanganyika walikuja kuzuia Mapinduzi ya wale wanajeshi mwaka 1964? Kulikoni!

Mkuu wangu, ni NCHI gani Duniani mshindi wa 3 wa Uchaguzi Mkuu ndiye alochukua nafasi ya juu kabisa kuwa Kiongozi wa Nchi?

Tunaweza bishana juu ya jambo ambalo hakuna Mzanzibar atakwamba Zanzibar haikutawaliwa na Sultan toka mwaka 1856 hadi 1964. Na walikuwa na bendera yao kama NCHI.

Na hata kama unazungumzia Mkataba wa Ulinzi na Muingereza mwaka 1890. Yale yalikuwa makubaliano baina ya Muingereza, Mjarumani na Sultan, ambayo Sultan alikuba kuwapa hao wakoloni baadhi ya maeneo ili Muingerez amlinde.

He the Sultan sold us to Brithish and Germany. Huwezi nambia ati Sultan hakuwa Mtawala wakati alikuwa na uwezo wa kuuza sehemu ya Utawala wake kwa Waingereza na Wajarumani. Uwezo huo kaupata wapi kama sii Mtawala?

Mkuu wangu, hata TANU walishiriki sana vikao vya Muingereza, tena wengine walichaguliwa na kushirikiana na Utawala wa Muingereza, haina maana tulikuwa HURU. Like I said. NCHI HURU ni ile Wananchi wanajitawala wenyewe na Sultan alikuwa Mu Oman.

Hakuna tofauti yeyote kati ya Uhuru wa Zanzibar na ule wa Ian Smith na hata kama unachukulia kutambuliwa na UN nimesema zipo NCHI leo hii zinatambuliwa na UN kama NCHI HURU lakini zinaongozwa na Wakoloni. Wananchi wake bado hawajapewa mamlaka ya kuongoza NCHI YAO. Hizi nchi hazina UHURU kwa Tafsiri sahihi ya NCHI HURU.
 

..Zanzibar ilikuwa Protectorate ya Waingereza.

..Tanganyika ilikuwa trustee territory ya Waingereza. Hatukuwa koloni la Waingereza, ndio maana uhuru wetu tuliupata kwa " ku petition " Umoja wa Mataifa.

..Katiba za uhuru za Tanganyika na Zanzibar ziliandikwa kwa msaada wa Waingereza.

..Ilikuwa ni utaratibu wa Waingereza kabla hawajakabidhi madaraka ni lazima waandae utaratibu wa Kikatiba kwa nchi inayopata uhuru.

..Baada ya uhuru wa 1963 Sultani alikuwa Mtawala wa Zanzibar kama ambavyo Mswati ni mtawala wa Swaziland.

..Zanzibar walikuwa na Bunge, mahakama, na serikali iliyoongozwa na Waziri Mkuu.

..Katiba ya Zanzibar ilikuwa inaruhusu vyama vya siasa kuungana na kuunda serikali.

..Chama kilichoshika nafasi ya 2 kwa viti vingi vya ubunge, na kilichoshika nafasi ya 3, viliungana na kuunda serikali. Katiba ya Zanzibar ilikuwa inaruhusu.

..Sasa nadhani ASP walikuwa wanalalamikia hila ktk ugawaji na uundaji wa majimbo. Nadhani ukihesabu kura moja moja walikuwa wanapata nyingi lakini majimbo wanashinda machache.

..Kuna hoja ya HIZBU umekuwa ukiirudia rudia. Nadhani ulitaka kujenga hoja ya Waafrika vs Waarabu[ Hizbu].

..Historia ya Zanzibar imejaa uongo na fitna nyingi. ASP inawashutumu wenzao kwa Uarabu. Lakini ASP maana yake ni Afro Shirazi Party. Sasa hao Washirazi si ni jamii isiyo ya Kiafrika?

..Katika muktadha wa siasa za Zanzibar, SHIRAZI ambao ni Waajemi, wana tofauti kiasi gani,U na HIZBU ambao ni Waarabu?

..Uhuru wa Zanzibar wa 1963 una tofauti kubwa na ule wa Ian Smith wa Rhodesia [ zimbabwe] kwasababu Zanzibar ilikuwa na mifumo ya kidemokrasia, ikiwemo Bunge, Mahakama, na executive.
 
Haitapendeza kama nitakuacha pembeni bila majibu ya hija zako kwa sababu unachofanya mkuu wangu ni reaction baada ya kusikia. Sawa na kwamba umesikia mkeo kasema hana maana basi wewe unaamya kuandika taraka.

Hizi Kero za Muungano kama nilivyosema ni Tofauti za Wazanzibar wengi wanaojiita Wanasiasa wakati hawajui Siasa haswa katika miundo ya Serikali. Na bahati mbaya sana Bara tunarudhia vitu ambavyo ni Kinyume cha Katiba.

Kama nivyosema makosa hayawezi kuwa ya Wazanzibar ikiwa wanaweza fanya mabadiliko ndani ya Katiba yao ambayo yanakinzana na Katiba ya Jamhuri. Hata katika ndoa zetu, ikiwa utamuacha mkeo akalale nje arudi asubuhi, halafu anakulalamikia wewe ujue mwenye tatizo ni wewe sio yeye! You the one who let that happened in first place..

Hizi ndio sababu zangu za kuweka lawama zaidi kwa Serikali (Dola) ya JMT ambayo zaidi ya asilimia 80 ni Watanganyika. Na kibaya zaidi hata wao wanakiuka Katika wakiiona kama nu Kijitabu au karatasi.

Viongozi kama kina Kabudi ni viongozi wa Vitabuni yaani wasomi wanaojua tafsiri lakini on the ground hakuna kitu. Kama unashindwa kutafuta njia ya kuzuia mafuriko na mvua, unawezaje tishia watu kuhusu El Nino ilhali wewe ni Kiongozi tena mbobezi wa Sheria?

Lini umewahi msikia Kabudi akikemea Mabadiliko hayo na Ukiukaji wa Katiba unaoendelea nchini? What we need is Action based leadership sio reaction Leadership! Siasa zetu zote zinaegemea upande wa After math, yaani kitokee kitu ndio tuanze kujadili Bungeni badala ya kuzungumzia tunayotarajia kutokea na tufanye nini. Tumetoka wapi na tunatakiwa kwenda wapi sio kurido nyuma kusahihisha yalokwisha tokea.

Kwa hiyo, narudia kusema hao kina Maalim Seif, Jussa na wengineo hawa wote walikuwa HIZBU wakaingizwa katika mfumo wa Chama kimoja cha CCM bila kubaguliwa. Maalim seif alikitumika Chama cha CCM na mamlaka alipewa kule Zanzibar akiwa Waziri. Hakulaani Muungano hata siku moja infact alikuwa karibu sana na Mwalimu. Matatizo yameanza pale tulipoanzisha Vyama vingi wale wa HIZBU wakapata mwanya wa kujitenga Upya kupitia CUF na sasa hivi ACT-Wazalendo. Sasa utawezaje Walaumu Wazanzibar ikiwa toka zamani Hizbu ilikuwa na Wafuasi wake, tena kibaya zaidi hao ASP walimkataa Salim A Salim kugombea Urais wa Tanzania sio Zanzibar kwa sababu ni HIZBU japo Salim A Salim aliendelea kuwa mwanachama halali wa CCM.

Kwa hiyo, tatizo lipo kwenye Utawala sio Wazanzibar na hata Watanganyika wanadai nchi yao sii kwa sababu wanaitaka kweli isipokuwa nchi yetu haina tena MWONGOZO (Katiba). Kila rais ajae anakuja na Kitabu Chake. This is very wrong na alotupotosha ni rais Mwinyi aliposema maneno hayo japo yeye alimaanisha kuja na SERA zake sio KATIBA.
 
Mkuu unazungumza vitu vingi vinavyojulikana lakini havina uthibitisho wa HAKI isipokuwa kwa mtazamo wako mwenyewe umeshindwa kunijibu nani alikuwa Mtawala wa Zanzibar kabla ya Uhuru. ukisema mwanzo ni Muingereza halafu sasa unasema Under British Protectorate! - Which is which? Mtawala alikuwa nani? Na kama ni Muingereza yeye alianza kutawala Zanzibar toka lini?

Umesema Katiba ya Zanzibar ilikuwa inaruhusu Vyama vya Siasa kuungana na kuunda Serikali, Katiba ipi na ibara gani ya Katiba hiyo? Kumbuka African Association na Shiraz Party waliungana kabla ya Uchaguzi wakasimamisha mgombea mmoja.

ZNP na ZPPP hawakuungana kabla ya Uchaguzi, kila chama kilisimamisha mgombea wake na matokeo yakawa ZNP mshindi wa 2 na ZPPP mshindi wa 3. ASP msindi wa kwanza, nambie nu sheria hani inamuondoa mahindi wa kwanza kwa kuchukua mshindi wa pili na tatu waunde Serikali?

Sheria za Uchaguzi sii sheria za kila nchi kujiamulia, kawaida kama nilivyosema Chama kilichoshunda ndio huunda Coaliton wapate Majority rule, wakishindwa kupata Coaliton basi hulazimika kuunda Serikali ya Minority (Umoja wa Kitaifa). Kiongozi hutoka Chama kilichoshika nafasi ya kwanza (on their case ASP) Laa kuna njia nyingine hutumika yaani Mshindi wa kwanza hushindana na wa Pili kupata atakae pata Majority, huyo ndio ataunda Serikali. Process hizi zinatumika kote duniani.

Njia zote halali za Kidemokrasia, hazikutumika ila Wakafanya yao kinyume cha Sheria, wewe unasema Katiba yao inaruhusu? Ndio nakuuliza Katiba Ipi?

Mwisho umezungumzia Zanzibar ilikuwa na Mtawala, Bunge na mahakama, Sijui Zanzibar ipi? Kwa sababu hata kabla ya Uhuru walikuwa na vyombo hivyo. Tanganyika kabla ya Uhuru ilikuwa na vyombo vivyo lakini bado tumetawaliwa. Unajaribu kuhalalisha kitu gani?

Kuwa na Serikali, Bunge na Mahakama sio hitimisho la kuwa huru na Serikali halali ila kwa mtazamo wa Watawala haijalishi ni Wakoloni au Nchi yao wenyewe. Hata hap Wakoloni Ukipingana nao utaitwa MHAINI lakini tunachojadili hapa ni Uhalali wa Mapinduzi ya Zanzibar kuuondoa Utawala wa Sultan ambao mimi nasema Ulikuwepo hata kabla ya Uhuru mwaka 1963.

Kilichofanyika ni kuuhalalisha tu kama Utawala halali wa Wananchi wa Zanzibar wakati Ukweli wakiwa bado wametawaliwa na Sultan yule yule. Na neno HIZBU linamaanisha wafuasi wa ZNP haijalishi rangi ya mtu.

Maasalaam
 

..Dec 9, 1961, hapa Tanganyika, bendera ipi ilishushwa, na ipi ilipandishwa?

..Dec 10, 1963, Zanzibar, bendera ipi ilishushwa, na ipi ilipandishwa?

..Bendera iliyoshushwa ndio ya mtawala. Na bendera iliyopandishwa ndio ya UHURU.

..Suala la nani alishinda uchaguzi Zanzibar, na jinsi serikali ilivyounda hulitendei haki.

..Nashauri ueleze ASP walishinda viti vingapi, ZNP, na ZPPP. Na ueleze walishinda maeneo gani.

..Katiba ya Zanzibar ya 1963 ndio iliyoruhusu vyama vya ZNP, na ZPPP, kuungana na kuunda serikali baada ya uchaguzi.

..Sina taarifa kama ASP waliikataa Katiba ya 1963. Na ushiriki wao ktk uchaguzi unaweza kuwa uthibitisho kuwa waliiunga mkono.

..Narudia tena, Znz iliyopata uhuru mwaka 1963 ilikuwa na bunge, mahakama, na serikali iliyochaguliwa.

..Zanzibar baada ya Mapinduzi haikuwa na bunge wala mahakama ya kiraia mpaka miaka ya 80.

..Serikali ya Zanzibar baada ya Mapinduzi imeuwa watu wengi kuliko serikali waliyoipindua.

Cc Nguruvi3
 
Katika yale yaliyo ongezwa tutajie moja ambalo Tanganyika imenufaika nalo, na moja tu lililoidhooifisha Zanzibar
Mwaka 2020 niliwahi kuandika hivi.

 
Narudia hizi ni dhana tu ambazo qatu wametunga hadith zao ili viongozi wale waonekane walikuwa na agenda zao binafsi ili hali naweza sema hakuna Kiongozi mwingine alowahi fanya makubwa kwa NCHi hii kwa kuelewana kuliko wao, iwe upande wa Tanganyika au Zanzibar.

Mpango wa Muungano haukutoka baada ya Mapinduzi ulikuwepo toka 1958 na September 1963 ndio ilijukana nani ndani nani kajitoa kwa tamaa tu za watu kuwa marais wa nchi zao. Nyerere na Karume walitaka NCHI moja, wakatofautiana kwenye Serikali ngapi.

Nyerere akitaka Serikali 2 kwa vigezo, na Karume Serikali 1. Hapo Mapinduzi wameingiaje kuwa sababu ya kutaka Serikali 1. Tena ni baada ya kuunda Serikali 2, Karume akapata mwanya wa kuwadhibiti wale walotofautiana naye kina Kassim Hanga. Ingekuwa Serikali moja asingekuwa na Mamlaka hayo kabisa.

Isitoshe kundi ambalo lilijadiliwa kuwa agaist Karume walikuwa viongozi wenye mrengo wa Kijamaa (Socialism) kina Hanga, Abrahman Babu na wengineo, kitu ambacho mkisema ndio sababu ama kichocheo cha Nyerere kuchagua Siasa ya Ujamaa 1967 pengine ningewaelewa.

Binafsi hainishangazi hata msisitizo wote wa Kujitenga ni wa Kisiasa ili kupata fursa za kuongoza nchi. Na ndio ubaya wa Siasa zetu badala ya Kiongozi kufikiria Kuongiza Wananchi anafikiria nafasi yake yeye kuwa Mtawala badala ya Kiongozi.

Na wanasema wazi wazi mpaka leo ati lengo kuu la Chama cha Siasa ni Kushika DOLA, halafu viongozi wa CCM wakisema wameishika DOLA ni kosa kubwa kwa mujibu wa Katiba. Akili ile ile wanatofautoana kwenye tukio.

Narudia tena, hii habari ya Zanzibar kujitenga ni Siasa za Viongozi walokosa nafasi ya Kutawala wakitumia ile formula ya divide and rule. Ndio hulka za Binadamu wanajua ukiwagawa watu.wanakosa nguvu ya Umoja wao, rahisi kuwatawala.

Tanzania ni NCHI moja yenye Serikali 2, mkitaka mabadiliko ya Serikali 3 au 1 tusiwasingizie Mwalimu na Karume kwa mapungufu tulokuwa nayo sisi. Tukubali kwanza Tumeshindwa kuongoza NCHI 1 yenye Serikali 2, twende tukajaribu muundo mwingine lakini tufahamu hatutaweza sote kufanya maamuzi ya pamoja. Wapo wanaopinga Serikali 3 na wapo wanaopinga Serikali 1. Whichever road we might take kuna mabonde na mashimo! Tukavae KOTI la Kuazima..
 
Mie nikisoma km hivi napatwa na hasira, jamani Mchonga na yeye Elimu yake ya Makerere ndio aliishia kuingizwa chaka na mvuvi wa samaki au baharia???
😒😒😭😭
 
Nahisi uchungu mie, 😒😒😭😭
 
Nimeipenda hii. Natamani watu wote waione hii hadi watanganyika walioko huko CCM na machawa wao.
Tanganyika irudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…