Mbeya: 40 Mbaroni tuhuma za wizi kwa kuingilia Mfumo wa TEHAMA

Mbeya: 40 Mbaroni tuhuma za wizi kwa kuingilia Mfumo wa TEHAMA

Haya mambo ya upigaji hayapo Mbeya tu bali halmashauri nyingi zinatakiwa kufanyiwiwa panel beating,na kibaya zaidi mwendo huu wa kubembelezana ni sawa na kucheza na nyani katika shamba LA mahindi.
 
Watu 40 wameiba sh milion 450 yaani kila mtu sh milion 11 tena tangu mwaka 2018 hadi sasa ni miaka mitano
Kugawa milion 450,000,000÷40= 11,125,000 kwa kila mmoja.
Kwa mwaka 11,250,000÷5= 2,250,000
Yaani kwa mwaka kila mtu aliiba 2,250,000.
Kwa mwezi 2,250,000÷12=187,500
Hivi nayo mnaita ufisadi ndani ya nchi hii iliyojaa ufisadi wa kutisha kila kona?

1): Ndege watu walikula cha juu (udalali) toka bilion 37 kuwa billion 85 wakaongeza cha juu 48 billion.
Na hakuna hatua walichukuliwa zaidi ya kuitwa "stupid "

2): Ngorongoro watu wamepiga mpunga mrefu Wamasai ardhi yao ikauzwa na safi tu, km hakuna kilichotokea.

3): Bandari na DP World tumeshuhudia watu wanakula Bata Dubai.
Leo wanapambana kuigawa bure bandari.
Nimengi mno yakukera na hatujasikia yakitolewa tamko lolote.

Hitimisho, hao raia wa mbeya kuna dalili zote za kuonewa na wanasiasa kutafuta kick za kijinga!
 
Siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaja ubadhilifu wa fedha mkoani Mbeya, watu 40 wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kuhusika kwenye wizi huo wa Sh450 milioni wa fedha za umma.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 28, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Denis Mwila amesema tuhuma zilizotajwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni za kweli ambapo watu 40 wakiwamo Madiwani, Wataalamu wa Tehama (IT), Watumishi na Watendaji wa kata wanashikiliwa na tayari baadhi yao wamefikishwa mahakamani.

Amesema hata kabla ya Rais kulizungumza, tayari walishaanza kulifanyia kazi tangu Julai 12, 2023 na kwamba mfumo huo wa ‘uchotaji’ fedha ulianza tangu 2018 na jumla ya Sh450 milioni zimeibiwa katika miaka mitano katika maeneo ya Mbeya, Njombe, Rukwa, Songwe na Ruvuma.

"Chanzo cha wizi huu ni mfumo unaotoka Dar es Salaam, ambapo kamati ya usalama Mkoa wa Mbeya tulifika huko na kumkamata mhusika na mfumo wake, lakini wamo Madiwani, Watumishi, Watendaji, Wataalamu wa Tehama na wakusanya ushuru na tayari baadhi wameshafikishwa mahakamani na wengine uchunguzi unaendelea chini ya Takukuru na wataendelea kufikishwa na wengine huko," amesema.

"Maagizo ya Rais tunayafanyia kazi hakuna atakayebaki salama, na waliokamatwa ni wale wa Wilaya ya Mbarali, Mbeya Jiji, Mbeya Vijijini, Rungwe, Tunduma, Ileje, lakini tunaendelea na uchunguzi kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria," amesema Mwila.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Takukuru ambao wanahusika na watuhumiwa hao, watafafanua kujua wangapi na kina nani hadi sasa wamefikishwa mahakamani na ambao wanaendelea na uchunguzi juu ya tuhuma hizo kwa hatua zaidi.

MWANANCHI
Mbona walikaa kimya mpk Rais aseme?
 
Wako 40,, ukipiga hesabu 450 gawanya kwa hao inakuja 11 ml,, je hiyo ni pesa kweli alafu toka mwaka 2018,,, duuu ,,, kuna mijizi mikubwa ipo tuuuu
 
KUFUATIA kauli ya Rais Dkt. Samia. Suluhu Hassan aliyoitoa jana juu ya tuhuma za wizi wa fedha za serikali kupitia mfumo wa mashine za kukusanyia mapato katika halmasahauri mbalimbali za nje ya mkoa wa mbeya na mikoa mingine jumla ya watu 40 wamekamatwa kufuatia wizi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Mkuu wa mkoa Mbeya , Kanali Dennis Mwila amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuhusu maagizo ya Mh. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yaliyotolewa jana na siku zingine za nyuma kuhusu upotevu wa mapato ambao umekuwa ukitokea katika mkoa wa mbeya na kuwa kuwa upotevu huo umekuwa ukifanyika katika mitandao ya Tehama katika halmashauri mbalimbali ndani ya mkoa wa mbeya na mikoa mingine .

“Kwanza kabisa nikiri kuwa wizi huo upo hadi sasa tumewakamata watuhumiwa 40 kutoka Jijini Dar es Salam ,Mbeya , Songwe, Ruvuma , Njombe katika wilaya za Ileje pamoja Tunduma Mji na kwamba chanzo cha wizi huo ni Dar es Salaam na mfumo huo umetengenezwa huko na timu ya wilaya ya mbarali ikishirikiana na mkoa kwa kupewa baraka na kamati ya usalama chini ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera ikaenda Jijini Dar na kukamata mtu huyo ,lakini vilevile kwa hapa mbeya na Songwe tumeweza kuwakamata waheshimiwa madiwani ,Watumishi wa halmashauri ,watalaam wa IT na wakusanya ushuru ambapo idadi yao kuwa 40”amesema Kanali Mwila.

Aidha Kanali Mwila amesema kuwa fedha zilizoibwa katika mfumo huo uliotenengezwa na wahuni hao ni shilingi million.450 ambazo zimeibwa ni Mbeya , Ruvuma , Njombe , Songwe, Rukwa hivyo niwatoe wananchi wa mkoa wa mbeya kuwa mkoa wao si shamba la bibi na watu wote waliofanya udanganyifu huo wa mapato wamekamatwa na baada ya kukamtwa siku ya tarehe 25, baadhi yao walifikishwa mahakamani na leo hii Agosti 28 , hii watafikishwa mahakamani wengine jambo hili wanaowafikisha mahakamani ni wenzetu wa TAKUKURU ,hivyo maagizo ya mh. Rais Samia yanatekelezwa yote kwa asilimia 100 na hakuna mtu ambaye atabaki salama kwa kufanya udanganyifu huu “amesema Kaimu Mkuu wa mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali.

Akizungumzia wizi huo Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mbeya ,VangSada Mkalimoto amesema kuwa mashtaka hayo yanatokana na taarifa walizopokea kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mbarali am,baye aliandika barua kuwa kuna ubadhilifu wa fedha wa mfumo kukusanya fedha za serikali katika halmashauri na kushauri ufanyike uchunguzi na kuomba ufanyike uchunguzi na kutokana na untyeti wa suala hilo waliwasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya na kutoa maelekezo kuwa Mkuu wa wilaya ya mbarali aunde tume maalum ya kufanya uchunguzi wa suala hilo na kuundwa tum,we iliyoshirikisha , Takukuru ,polisi , usalama wa taifa na walipofanya ufatiliaji kwa utekelezaji kwa viongozi waliokuwa wameutoa katika kipindi hicho ikiwemo maelekezo ya Mh Rais Samia ya kipindi hicho na jana.

Aidha amesema kuwa katika wizi huo walibaini kuwa wizi wa aina mbili ambao ni uhujumu uchumi wa kuisabishia hasara serikali ,wakusanya ushuru katika halmashauri mbali mbali ambao walikuwa wakitumia simu zao za mkononi ambazo zilikuwa zimeunganishwa na printer wakiwa na mashine za kukusanya usghuru za serikali wanaacha kutumia mashine za serikali wanatumia za simu zao na kutumia simu zao ambazo zinatoa nembo za halmashauri zao.

Hata hivyo amesema kuwa leo wameweza kuwafijkisha mahakamani tena watuhumiwa 14 ambao walitengeneza Tovuti ambayo ilikuwa imeunganishwa na mashine mbali mbali za kukusanya mapato na mmiliki wa tovuti hiyo ni mwananchi wa kawaida tu ambaye aliwaajiri wataalam wa Tehama wa halmashauri wakishikirikiana na mtengeneza mfumo bandia Jijini Dar es Salaam Robert Mpeleta mmiliki wa mfumo bandia na kuanza kusghirikiana watengeneza ushuru wa halmashauri mbali mbali ambao wanawapa mashine hizo kila wakikata ushuru inasoma ushuru kwenye mfumo wake .
Mwisho
Kama jambo hilo la kiharifu limetekelezwa kwenye ngazi ya halmashauri inawezekana ngazi ya TRA nako kuna uharifu wa aina hiyo.Wahusika wafanyie uchunguzi mifumo yote ya ukusanyaji mapato.
 
Ndiyo maana vijana tunataka ingia serikali i hata halmashauri tu. Mirija kama hii
 
mfumo huo wa ‘uchotaji’ fedha ulianza tangu 2018 na jumla ya Sh450 milioni zimeibiwa katika miaka mitano katika maeneo ya Mbeya, Njombe, Rukwa, Songwe na Ruvuma.

Duuuh kumbe tangu enzi za NZIRANKENDE JIKONO JANDAMA watu walikuwa wanapiga kwenye mifumo? Si tuliambiwa kulikuwa hakuna WIZI kwasababu ya Control Number?

"NALO PIA MKALITAZAME " -SSH
 
Back
Top Bottom