Mbeya: Askari Polisi afariki kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi

Mbeya: Askari Polisi afariki kwa kujipiga risasi kisa mgogoro wa mapenzi

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya J.2596 Konstebo Samwel Feston Kaziyote mwenye umri wa miaka 24 wa kituo kikuu cha polisi Mbeya amefariki dunia baada ya kujiua kwa kujipiga risasi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga, imeeleza kuwa kuwa mnamo Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku maeneo ya mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la benki na kisha kuondoka na silaha kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

#EastAfricaTV
FB_IMG_1696357105291.jpg
 
Mbeya tushazoea... hapo miezi michache iliyopita maaskari wawili walijinyonga, moja wa zimamoto
 
Dogo hana akili kabisa.

Kila siku tunawaambia vijana kwamba usipende mwanamke, mwanamke usimpe moyo wako, mpe hela sio moyo...
Tatizo unapoanza tu kumpa hela mwanamke baadae unashtuka moyo ushejipeleka wenyewe bila kuutuma.na hapo ndo pagumu
 
Back
Top Bottom